Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), walikaa chini na wakafanya demokrasia ya uamuzi kwa kupiga kura, hayo yote sisi hatukuyajua na yalikuwa ni siri ya Chama, kama hayakuwa siri, Katibu ama mwenyekiti wa Chama angetueleza (Kupitia vyombo vya Habari),
lakini kitendo cha Zitto kwenda kwenye vyombo vya habari na kuiongea hiyo siri ya vikao vyao ni USALITI, MIMI hapa simpingi Zitto kwa uamuzi wake aliochukua wa kutokubaliana na hilo la kutoingia bungeni kabisa, hiyo ni Demokrasia na ndio maana Chadema walipiga kura, ninachomlaumu na kumwona Zitto kuwa msaliti iweje aende kwenye vyombo vya HAbari na Kuropoka, Chama kitamwamini vipi tena katika siri zingine za kichama,
Zitto inampasa kuelewa kuwa Chama kina viongozi na kuna wasemaji, Mwenendo wa Zitrto ndani ya Chadema ni wakutia mashaka sana, kwa nini anapenda kwenda kwenye vyombo vya habari bila baraka za viongozi wake, Angalia issue kama ya mwenyekiti wa kambi ya upinzani bungeni, nadhani kwake ilikuwa ni busara kusubiri maamuzi ya chama kupitia vikao vyao ili wapendekeze jina, lakini alikurupuka na kutangaza atagombea hiyo nafasi,
Ushauri kwa Zitto
ki ukweli kabisa siasa zako haziendani na Chadema kabisa, uko fast sana, una siasa za kipekeyako, za kibinafsi na sio za kichama, kama ukiwa kwenye Chama cha muhimu ni kufuata chama kinataka na kinasema nini, aina za Chama zinazokufaa ni kama TLP na NCCR, kwamba kila mtu anasema lwake