Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
Na kuna hawa wa kizazi kipya nao usipokubaliana nao tu wanakuambia wewe CCM!!!!
Hatuwapotezei hawa sababu nchi kwanza vyama badae!!!!

Sera mfu kwa kasi mfu! Nchi kwanza vyama badae! Miaka Zaidi miaka 50 ya Uhuru Bado tunalima kwa jembe la mkono!
Ndo mjue kizazi kipya hatudanganywi! Ukileta zako Wewe watakuambia tu kua Wewe ni Ccm, mbona Nyie mnawaambia Cdm?
 
Ripoti kuipata sio mpaka uwepo kwenye kikao. Andikeni ripoti wapeni wanachama na viongozi wazione. Acheni porojo kwenye masuala ya pesa.
... kweli mkuu. Sijui kwa nini hawaigi wenzao CCM repoti zao za fedha mpaka kwenye magazeti ya udaku unazikuta.
 
Hata kupambana na CHADEMA nayomni kazi kama nyie mnavyopqmbana na CCM. Nikuulize, hivi Dr Slaa huwa anafanya kazi gani nje ya kazi ya siasa?
Hahahahaaa! Mwenzake Kinana kazi yake nje ya siasa sote tunaijua....Hivi sasa anatembelea mikoa iliyokaribu na ile mbuga.
 
ZZK bado nina imani nae ndani ya CDM sijui ni kwa nini ajahudhuria kikao hiki lakini ukweli tutaujua tu.
 
Tanzania daima sio gazeti la CHADEMA....Mbona unaropoka wewe? mbona hujiulizi wali choandika mwananchi? hata kama akili zenu CCM hakuna si mtumie tu hisia.......
Tatizo la watu wenye akili na upeo kama wako wakikosa hoja huwa wanakimbilia kwenye hoja za mitazamo ya kidikteta na kusema you're either with us, or against us kutaka kupenyeza na kulazimisha hoja zao hata kama hazina mashiko yoyote. Ulinikabidhi kadi ya uanachama wa CCM au chama chochote cha siasa cha Tanzania kamaa hujafanya hivyo, nani kakwambia mimi ni mwanachama wa vyama vya siasa.

Nimesema wapi kama Tanzania Daima ni gazeti la CHADEMA. Lazima ufahamu tofauti ya kusimama kwenye nguzo na kuwa nguzo yenyewe. Tanzania Daima kusimama kwenye nguzo ya kisiasa ya CHADEMA haina maana ni gazeti la CHADEMA.

Kama kweli Tanzania Daima ni objective kwa nini liseme Mh. Zitto amekacha wakati kati ya wajumbe 32, ni wajumbe 23 tu wamehudhuria. Hata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika naye hakuhudhuria kwenye kikao.

Kwa nini kukosekana kwa Mh. Zitto kwenye kikao cha kawaida kabisa ndiyo iwe hoja ya Tanzania Daima.

Gazeti la Mwananchi limeandika na kusema hivi,
Zitto na Mnyika wakosekana

Zitto na Mkurugenzi wa Uenezi wa chama hicho, John Mnyika walikuwa miongoni mwa wajumbe walioshindwa kuhudhuria jana.

Zitto yuko na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) huko Sudan Kusini na Mnyika pia yuko katika ziara ya kibunge Uturuki.

Kikao cha jana kilihudhuriwa na wajumbe 23 kati ya 32.

Hofu yatanda Kamati Kuu Chadema - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Kama mnaona Zitto, haendani na nyinyi CDM si mumfukuze... maana kwa mambo ambayo mnamtuhumu nafikiri hana sifa za kua mwana CDM, na kama mnaendelea kumkumbatia basi nyie CDM ni wanafiki sana mnaomchafua kwa manufaa yenu binafsi hasa ya kiuongozi.

hii ni sawa na kukumbatia bomu ambalo linataka kulipuka alafu wewe hutaki kuliachia ilihali unataka kuishi, sasa sisi tutakuelewaje hapo?
...kama una akili utajua adhabu ya kumfukuza ni nyepesi kuliko adhabu ya kumuacha ahukumiwe na consciousness yake mwenyewe. Yote haya ya kuikimbia ofisi yake na kukwepa sura za wanakamat kuu ni consciousness yake inamsuta.
 
Ngoja niendelee kutoelewa post zako,

Umesema wajumbe wangetoa dukuduku lako kwenye vikao vya chama mimi nikakuuliza kwani hao wajumbe walisemea nje ya kikao?... soma tena yaliyoandikwa na T. Daima..
Ndiyo maana nikasema hujanielewa kwa sababu kama wametoa dukuduku lao ndani ya kikao, kwa nini wanatoka nje na kuanza kuongea kile ambacho wamekisema ndani ya kikao kama kwamba hawajaridhika na kilichofanyika katika kuzifanyia kazi dukuduku zao, na hata kama hawakuridhika, kwa nini hawakusema huko huko kwenye kikao badala yake wanatoka nje na kuanza kulalamika na malalamiko yao yanatengenezewa habari na Tanzania Daima kutimiza malengo yake katika hii kadhia. CHADEMA kina official channel katika kuwasiliana na outside world. Kwa nini wasitumie hiyo channel kufikisha ujumbe wao.

Wajumbe zaidi ya 9 hawakuhudhuria. Kwa nini kukosekana kwa Mh. Zitto ndiyo iwe habari ndani ya gazeti la Tanzania Daima wakati hata Mh. Mnyika ambaye ni high profile ndani ya CHADEMA naye ni mmoja wa wajumbe ambao hawakuhudhuria hicho kikao.
 
Zitto ni mkachaji sugu kama akibahatika kuwa mwenyekiti sijui vikao vitakuwa vinaongozwa na nani.
 
Tatizo la watu wenye akili na upeo kama wako wakikosa hoja huwa wanakimbilia kwenye hoja za mitazamo ya kidikteta na kusema you're either with us, or against us kutaka kupenyeza na kulazimisha hoja zao hata kama hazina mashiko yoyote. Ulinikabidhi kadi ya uanachama wa CCM au chama chochote cha siasa cha Tanzania kamaa hujafanya hivyo, nani kakwambia mimi ni mwanachama wa vyama vya siasa.

Nimesema wapi kama Tanzania Daima ni gazeti la CHADEMA. Lazima ufahamu tofauti ya kusimama kwenye nguzo na kuwa nguzo yenyewe. Tanzania Daima kusimama kwenye nguzo ya kisiasa ya CHADEMA haina maana ni gazeti la CHADEMA.

Kama kweli Tanzania Daima ni objective kwa nini liseme Mh. Zitto amekacha wakati kati ya wajumbe 32, ni wajumbe 23 tu wamehudhuria. Hata Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika naye hakuhudhuria kwenye kikao.

Kwa nini kukosekana kwa Mh. Zitto kwenye kikao cha kawaida kabisa ndiyo iwe hoja ya Tanzania Daima.

Gazeti la Mwananchi limeandika na kusema hivi,

Kubishana na vifaranga Mkuu inahitaji moyo na stamina ya hali ya juu katika kuvumillia uzuzu wao,

We si umeona huku page za nyuma Dr Slaa ametokea kama kawaida yake na kuja KU-LIKE POST moja yenye ukakasi inayomuhusu zitto??

Sasa sijui hii ni kwanini,Dr Slaa kila uzi unaomuhusu zitto humu ndan huwa hakosekani kutokea na kuja KU-LIKE POSTS ZA VIFARANGA,INASHANGAZA SANA,,,

DR SLAA TATIZO NI NIN HASA??KAMA KWELI ANA SUMBUA HUYO JAMAA KWANIN MSIMCHUKULIE HATUA NDAN YA VIKAO VYA CHAMA??

MITANDAO YA JAMII INAKUSAIDIA NINI KATIKA HILO??

UNAJIABISHA SANA,,,,
 
Ngoja Zitto awapishe labda mtakuwa na mengine ya kujadili, maana kila siku Zitto Zitto
 
Zitto hajahudhuria kwa dharura wanatukana Dr Slaa analike posts hizo,

Mnyika pia hajahuhduria kwa dharura Dr Slaa kimya na vifaranga wanashangilia,,DOUBLE STANDARD AT ITS BEST LEVEL...!!

KUNA AJENDA GANI INAYOFICHWA FICHWA??
 
Wajumbe zaidi ya 9 hawakuhudhuria. Kwa nini kukosekana kwa Mh. Zitto ndiyo iwe habari ndani ya gazeti la Tanzania Daima wakati hata Mh. Mnyika ambaye ni high profile ndani ya CHADEMA naye ni mmoja wa wajumbe ambao hawakuhudhuria hicho kikao.
Nafikiri umeanza kunielewa, dukuduku limetolewa ndani ya kikao, kuongea au kutoongea nje baada ya kikao si tatizo kwa sababu hatujaambiwa kama wajumbe walizuiwa kutoa maoni yao kwa waandishi baada ya kikao.

Kuhusu kutohudhuria kwa wajumbe wengine sambamba na Zitto,

Zitto amekuwa hahudhurii si vikao tu bali hata mikutano ya chama na huwa hafiki kabisa ofisini makao makuu vile vile amekuwa na mivutano na viongozi wake tofauti na Myika, kwa akili ya kawaida tu lazima mtu atahoji kutokuwepo kwa Zitto zaidi ya kutokuwepo kwa Mnyika.
 
Watu wanahangaika sana na mambo ya kijinga! Mbona hata Mnyika hayupo kwa kikao???
 
Binafsi nalishukuru gazeti la T. Daima kwa kuujulisha umma kuwa Zitto amekimbia kikao halali cha chama ambacho angekitumia kutoa dukuduku lake.

Nafikiri chama kinajiweka kwenye nafasi nzuri ili wananchi na wanachama wazidi kuzielewa rangi zote za Zitto kabla ya kuchukua hatua ili yasiwepo madhara makubwa baadae.
Vipi John Mnyika naye kakimbia tufahamishe kamanda.
 
Tanzania Udaku siku hizi! Source imetulia sana imetoka CDM ati ni source ambayo itakuwa huru?

Mwelevu amevimbua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom