Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.

chitalula

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
1,302
Reaction score
416
WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiendelea na kikao chake jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, amekacha.

Zitto ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mjadala kwenye vyombo vya habari, hasa alipoingia kwenye malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amekacha kikao hicho na badala yake ametoa taarifa ya kusafiri nje ya nchi.

Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa iliyotolewa kwa wajumbe wa mkutano huo na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, ilisema kuwa Zitto yuko safarini nchini Sudan, lakini anatarajia kuhudhuria mkutano huo wakati wowote.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kinachofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe wameonyesha dhahiri kukerwa na hatua ya naibu katibu mkuu huyo kutoshiriki.

Waliolalamikia hatua hiyo walisema kuwa limekuwa jambo la kawaida kwa Zitto kutohudhuria vikao muhimu vya chama huku akijua fika kwamba yeye ndiye msaidizi mkuu wa katibu mkuu wa chama taifa.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho aliliambia gazeti hili kuwa moja ya ajenda zilizowasilishwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi ni kuhusu mapato na matumizi ya chama ambayo alidai ingefaa Zitto awepo kuisikiliza.

Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ajenda hiyo ilikuwa muhimu kwa Zitto kuwepo kwani akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), amekuwa akidai kwamba CHADEMA na vyama vingine hawana hesabu za mapato na matumizi ya fedha za ruzuku wanazopata kila mwezi.

Mkutano huo unaendelea leo.
 
SI BURE KUNA JAMBO poleni cdm AINA HII YA KIRUSI SIJUI MTAKIONDOAJE maana si cha ukimwi,pepopunda wala ebola, kibaya zaidi ukikikosea ktk utibabu wake hakikawii kuondoka na mgonjwa mwenyewe,""ebu mnafiki na mwongo tuzidi kumwongoze""
 
usaliti mbaya. sijui hajajifunza kwa kafulila alipo pigwa chini akaanza kulia na kudondosha kamasi zito. sasa huyu anapata faida gani kuwa kondom ya magamba
 
ripoti ya mapato na matumizi ni ya watanzani wote, sio zito wala kamati kuu. Haina ulazima wa kuhudhuria kikao ndio uipate. Ingetakiwa mpaka kwenye website ya chama iwepo ili watanzania waone kodi yao (ruzuku) inavyotumika.
 
ripoti ya mapato na matumizi ni ya watanzani wote, sio zito wala kamati kuu. Haina ulazima wa kuhudhuria kikao ndio uipate. Ingetakiwa mpaka kwenye website ya chama iwepo ili watanzania waone kodi yao (ruzuku) inavyotumika.
Kwa kuwa hicho kikao wamejaa vifaranga na mama zao, nina hakika hata hiyo taarifa ya mapato na matumizi haipo au imeandaliwa kivifaranga na mama zao
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom