Zitto Zuberi Kabwe kwa sasa ni dhahiri kabisa inaonyesha ni tatizo ndani ya chama. Huu ni ukweli mchungu kwa Zitto lazima akubaliane nao na dalili zote zinaonyesha hivo!Ni kichekesho kama siyo kihoja kwa N/Katibu Mkuu wa CDM kutohudhuria kikao muhimu cha Kamati Kuu yeye akiwa kiongozi mwandamizi na Mjumbe muhimu wa kikao husika! Hili haliingii akilini hata chembe!!!!!!
Haiwezekani CC ya CDM ikae kwa ajili ya kujadili maswala nyeti na muhimu yanayohusu chama halafu yeye awe na Ziara zake binafsi ambazo hazihusiani moja kwa moja na CDM! Hii ni dharau na ni ishara mbaya sana kwa Zitto.
Zitto alishavimba kichwa kwa umaarufu ambao nina hakika unaenda kumwangamiza kisiasa. Tunajua kabisa yuko karibu sana na baadhi ya Viongozi wa CCM akiwemo rais Kiwete. Lazima kwa namna fulani kwa nyakati fulani Zitto anatumiwa na Serikali ya CCM kuivuruga CHADEMA, hili halina ubishi na Zitto analijua hilo kule ndani ya nafsi yake!!!
Chokochoko zote hizi za Zitto,sijui amechafuliwa sana,amepigwa mishale sana,amezushiwa sana na Viongozi ndani ya Viongozi wenzake ni vurugu za kutaka kukisambaratisha chama. Kuna mambo yako wazi kabisa kuhusu huyu dogo ambayo yana ashiria kuwa hayuko pamoja na Uongozi wa Juu wa chama:
- Kuna hili la kutaka KUGOMBEA kuwa Mwenyekiti wa CDM,ili hali chama kina Mwenyekiti anayeongoza vizuri tu. Hili ni tatizo. Kuna mawili hapa aidha ni TAMAA ya madaraka au ni NJAMA za kuvuruga chama.
- Kuna hili la POSHO za Wabunge.Kwamba Zitto hataki kupokea posho ambazo ziko kwa mujibu wa sheria na kanuni za Bunge. Sasa huwa simwelewi Zitto anapokataa posho ambazo ziko kisheria anataka kumfurahisha nani? Je,ni mbinu zake za kisiasa kutaka kujimbanua na viongozi wenzake ndani ya CDM au nini? Kwanini basi hapeleki muswada wa kupinga hizi posho kama anaona hazina umuhimu badala ya kulumbana na kina Lema kwenye mitandao?
- Kuna hili la RUZUKU ya Serikali kwa vyama vya siasa ambapo Zitto anasema vyama hivi vyote ikiwemo CDM hawajawahi kuwasilisha hesabu zilizokaguliwa na CAG tangu mwaka 2009. Zitto anadai hivo kama Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge lakini wakti huohuo yeye ni N/Katibu wa CDM. Swali ni: Yeye alikuwa wapi miaka yote hii kuhusiana na Mahesabu ya CDM??? Huu ni UNAFIKI wa Zitto kwa chama.
- Kuna matukio yanayohusu CHADEMA ndani na nje ya Bunge ambapo Zitto mara zote ameonekana kutoungana na Viongozi wenzake katika kupinga mambo hayo. Mosi ni hili la msimamo wa CDM kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya. Wakti viongozi wa CDM wakipinga uchakachuaji wa rasimu hiyo Zitto hakuwepo kabisa wala hakuwa na habari. Kuna mlipuko wa Bomu la Soweto kule Arusha, Zitto Kabwe hakuwepo wala hakuguswa na tukio hilo kwa vile hakuna mahali popote aliwahi kulizungumzia tukio hilo kana kwamba halimuhusu!!!Hili ni tatizo kwa Zitto.
- Mwisho ni hili la MABILIONI YA FEDHA zilizoko ughaibuni ambazo bila shaka zimetoroshwa na MAFISADI wachache wenye uroho na utajiri wa harakaharaka. Bwana Zitto ameligeuza swala hili kama swala BINAFSI na hataki kabisa kukihusisha chama. Sasa simwelewi huyu jamaa anataka sifa au ni mbinu zake za kisiasa za kujizolea umaarufu wakti akizidi kukididimiza chama!!! Mimi namkumbusha Zitto Kabwe kuwa kidole kimoja hakivunji chawa! Arejee kumbukumbu zake kuhusu isseu ya EPA. Swala la EPA lilitikisa nchi kwa vile kina Dr. Slaa na kina Mbowe waliungana pamoja kimkakati kwa kutaja ile LIST OF SHAME na ikazaa matunda!
Tunamshauri Zitto aache ulevi na tamaa ya madaraka na sifa kwani zitamporomosha vibaya sana kisiasa labda kama ana mpango wa kuhamia huko kwa watu wa Magamba-CCM.
Wasalaamu.