Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Zitto akera wajumbe kamati kuu CHADEMA - Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
Kweli waTZ bado wagumu kutaka acha bebewa uwezo wao wakufililia na kutambua. CDM ni mamluki 2 hawana uchungu wowote na Taifa hili na wa2 wake. Ni mafisadi walio vaa kizuizi cha mdomo kwamaneno ya kizandiki na uchochezi pasina Uzalendo hata kiduchu. Big up great politician ZZK
 
Mwaka 2010, Sebastian Kasinge aliyeteuliwa
kugombea ubunge jimbo la Mpanda
Mashariki, alikwama kuwania nafasi hiyo.
Kisa?! Zitto.
Ilikuwa hivi, Kasinge alikwama kupata barua
ya utambulisho kutoka kwa viongozi wake wa
wilaya ya Mpanda kuwa ni mgombea.
Akaenda makao makuu ya Chadema jijini Dar
es salaam. Akakutana na Dk. Slaa, katibu
mkuu wa Chama chao, Akampa barua ya
uteuzi.
Lakini Zitto kwa kutumia kofia yake ya
unaibu katibu mkuu tena akiwa nje ya ofisi
na bila kushirikiana na wenzake wa makao
makuu, alimwandikia msimamizi wa uchaguzi
wilaya ya Mpanda kumjulisha Chadema
kutoweka mgombea jimbo la Mpanda
Mashariki. Msimamizi wa Uchaguzi mara
baada ya kupata barua ya Zitto alimwondoa
Kasinge kwenye kinyang'anyiro cha ubunge na
kumtangaza Mgombea wa CCM, Mizengo
Kayanza Peter Pinda kuwa AMEPITA BILA
KUPINGWA
Michael Makenji aliyekuwa mgombea wa
ubunge wa Chadema jimbo la Musoma
Vijijini, alijiondoa kwenye kinyang'anyiro
hicho dakika za mwisho. Nimrod Mkono wa
CCM ALIPITA BILA KUPINGWA. Hii ni baada
ya Zitto kumshawishi mgombea wa chama
chake kujitoa. Taarifa zinazomkhusu Makenji
zinasema kabla ya mgombea huyo kujiondoa
kwenye kinyang'anyiro, naibu katibu mkuu
wake alifanya mazungumzo ya kina na
Mkono.
Katika kuthibitisha hilo, Makenji alikabidhi
kwa viongozi wake wa chama ujumbe mfupi
wa sms ulioonekana umetoka kwa Zitto
kwenda kwake ukilenga kumshawishi kujitoa.
Miongoni mwa yale yaliyotajwa na Zitto
kwenye ujumbe huo ni pamoja na kwamba
Mkono yupo tayari kuongeza fedha iwapo
yeye Makenji atakubali kujiondoa kwenye
mbio za kuwania ubunge.
Josephat Isango, aliyejitosa kwenye mbio za
ubunge jimbioni Singida kupambana na
Mohamed Dewji aliwekewa pingamizi na
Wazael Nakamia, mwenyekiti wa Chama
chake, CHADEMA wilaya ya singida Mjini.
Katika pingamizi lake, Nakamia anasema
Isango hakupitishwa na Chama chake
kugombea nafasi hiyo. Alipoulizwa na
mkurugenzi wa sheria wa chama hicho,
Tundu Lissu kilichosababisha kuwekewa
pingamizi kwa ndugu Isango, Nakamia
alisema ..."ni maelekezo ya Naibu katibu
Mkuu..."
Zilitokea vuta nikuvute kadhaa ambapo
mwishowe Dk. Slaa ambaye alikuwa amelazwa
hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa matibabu
alimwandikia msimamizi wa uchaguzi barua
nyingine ya kuthibitishauteuzi wa Isango.
Rais Kikwete alipofika singida kumnadi
mgombea wa CCM Singida alimtangaza Dewji
kuwa amepita bila kupingwa, siku chache
baadae NEC ikamtangaza Isango kama
mgombea.
Tamthilia hii ya Isango, Zitto, Dewji, Nakamia
na Lissu imeelezwa mara nyingi na na Lissu
mwenyewe kwenye vikao vya CC mbele ya
Zitto wenyewe. Zitto Hakuwahi kukana.
Nakamia tayari amevulia uongozi.
Mgogoro wa Madiwani Arusha haukumalizika
bila ya kumhusisha Zitto. Kamati iliyoundwa
na chama chake kutfuta suluhu ya mgogoro
huo iligundua mkono wa Zitto katika suala
hilo. Mgogoro ule uliisha kwa kufukuzwa
madiwani watano.
Naibu katibu mkuu alishiriki kwa kiasi
kikubwa katika mgogoro huo kwa kushiriki
kuwashawishi madiwani kukiasi chama, ni
sehemu ya mkakati wake wa kupambana na
Lema na wanasiasa wenzake ndani ya chama
chake wanaoonekana kumpiku kwa umaarufu.
Uchaguzi mdogo ulipofanyika Zitto
hakushiriki hata mkutano mmoja wa
kampeni,Hkwenda Arusha siku ya
Maombolezo baada ya vifo vya wafuasi wanne
wa Chadema.
Mengi zaidi soma MAWIO, Toleo namba 0070
Alhamis November 21-27, 2013 Uk10-11
 
Wewe bora ungekaa kimya kuna mtu anawachukia Waislam kama wewe humu acha kujibaragua kauzu wewe.

ndio mi kauzu,na nakuchukia sana na magaidi wenzio,na wanajulikana.mnachukia sana kuona cdm ina wapiganaji wa dini zote,propaganda zenu zinakosa mashiko.Zitto anashikwa adabu na uislam wake fake,kama walivyoshikishwa madiwani wa Arusha wakiwmo christian
 
Taarifa ninayoitegemea na nitakayoifùrahia kimkakati ni kusimamishwa kwa Zitto nafasi yake ya unaibu katibu mkuu
 
Kukwamisha mipango ya serikali kivipi??

Ishu ya gesi ya mtwara ni pana sana,na haiko kisiasa,na haitokuwa ajenda ya kisiasa hata siku moja,haijaisha na bado inaendelea,kama unaona huu ukimya wa watu wa kusini ukahis game is over,we iulize serikali itakuambia ni kwa namna gani inaaathirika na passive resistance wanayokumbana nayo huku,kinana si alikuja huku juzi na msafara wake??waulize wameambulia nini huku,hoja ya gesi iko wazi kbs,ni kuitaka serikali kuwa na utaratibu unaoleweka wa uvunaji gesi kisheria na kwa maslahi ya taifa,hakuna anaetaka yaliyotekea huko buzwagi na kwingineneko kwenye rasilimali za taifa zivunwe na kuachwa mashimo huko wanacnhi wa kawaida na maeneo husika yakiachwa na umaskin wa kutupwa,iko wazi kbs

Na kuhusu udini,huwa mnamaanisha nin hasa??ni dhambi kwa mimi kuwa muislam au kujitambulisha na uislam wangu??ukitakaje sasa nijifiche niukane uislam kwa kukuogopa wewe au kwa kumuogopa nani??nitafutie post yangu yyte humu jamvin uliyoniana nahubir chuki dhidi ya wale wasiyo na iman sawa na mimi,unless otherwise niambie nin definition ya udini??ukiishiwaq hoja usilete viroja...


The Big Show........! Wewe ni mtu mkubwa sana na jina lako ni kubwa sana! Taratibu Mkuu na upunguze hasra!
 
Nimesema hivi huyo Double Agent wenu ameshakuwa-fixed amebaki kuwa boya hana say yeyote kwenye chama mwisho hafukuzwi mtu ila inatumika psychological torture hadi akimbie mwenyewe, nafikiri utanielewa safari hii, good bye.
Kamanda! Mbona kina Mwigamba, Chagulani, wale madiwani Arusha, kina Mwampamba, Juliana, Mchange hawa wote mbona mliwafukuza, kwa nini Zitto kawashinda mnamuogopa.
 
Wamfukuze chama Zitto.

Thubutu!
...endeleeni kumpigania awe mwenyekiti jamani. mbona mnaanza kushabikia afukuzwe wakati lengo letu pale Lumumba ilikuwa awe mwenyekiti? msikate tamaa jamani, endeleeni kuchochea mpaka aukwae uwenyekiti.
 
sichukii waislam,nachukia wadini kama wewe.unayemtetea mtu au kumpinga kwa misingi za dini.wajomba na mama wadogo zangu wote waislam.ni wapenzi wangu.huna sababu ya kumtetea ZZK isipokuwa uislam.kwa taarifa yako yule ni muislam fake

Ulikua una haja gan ya kumwita zitto shekhe kisha ukamusisha na mada iliyopo??sasa nani hapo kaingiza chuki za udini baina yangu na wewe??

Ukinichukia mimi sababu ya udini ambao hauspecify uko vip unajipotezea time yako bure tuh,mimi siwez kuukana uislam eti kwa kuogopa kuchukiwa na wewe au yyte yule hata siku moja,uislam ni mfumo wangu wa maisha,as long as ninamfurahisha mola wangu nina haja gani ya kuogopa chuki zako mwanadamu??ili hali wewe na mimi sote kaburin tutaingia??i dont care,never ever...!!!
 
WAKATI Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikiendelea na kikao chake jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, amekacha.

Zitto ambaye katika siku za hivi karibuni aliibua mjadala kwenye vyombo vya habari, hasa alipoingia kwenye malumbano na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amekacha kikao hicho na badala yake ametoa taarifa ya kusafiri nje ya nchi.

Kwa mujibu wa habari hizo, taarifa iliyotolewa kwa wajumbe wa mkutano huo na Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, Freeman Mbowe, ilisema kuwa Zitto yuko safarini nchini Sudan, lakini anatarajia kuhudhuria mkutano huo wakati wowote.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kinachofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, jijini Dar es Salaam zilieleza kuwa baadhi ya wajumbe wameonyesha dhahiri kukerwa na hatua ya naibu katibu mkuu huyo kutoshiriki.

Waliolalamikia hatua hiyo walisema kuwa limekuwa jambo la kawaida kwa Zitto kutohudhuria vikao muhimu vya chama huku akijua fika kwamba yeye ndiye msaidizi mkuu wa katibu mkuu wa chama taifa.

Mmoja wa wajumbe wa kikao hicho aliliambia gazeti hili kuwa moja ya ajenda zilizowasilishwa jana na Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi ni kuhusu mapato na matumizi ya chama ambayo alidai ingefaa Zitto awepo kuisikiliza.

Mjumbe huyo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, alisema ajenda hiyo ilikuwa muhimu kwa Zitto kuwepo kwani akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC), amekuwa akidai kwamba CHADEMA na vyama vingine hawana hesabu za mapato na matumizi ya fedha za ruzuku wanazopata kila mwezi.

Mkutano huo unaendelea leo.

Nchi kwanza chama baadae. Huyu kaenda kushughulikia maswala ya nchi na sio maswala yake binafsi. Wajumbe wapunguze gjazba na walielewe hilo.

Pili, hivi Tanzania nzima gazeti ni moja tu "TANZANIA DAIMA" kwani kila kukicha hapa jf nukuu ni TANZANIA DAIMA TU hasa ikiwa habari zinahusu CHADEMA. Mmmmmm Wenzangu nyinyi mmenichosha. Kwa siku za mbele mkinukuu TANZANIA DAIMA nitafanya mgomo wa kusoma na kujibu.
 
Nchi kwanza chama baadae. Huyu kaenda kushughulikia maswala ya nchi na sio maswala yake binafsi. Wajumbe wapunguze gjazba na walielewe hilo.

Pili, hivi Tanzania nzima gazeti ni moja tu "TANZANIA DAIMA" kwani kila kukicha hapa jf nukuu ni TANZANIA DAIMA TU hasa ikiwa habari zinahusu CHADEMA. Mmmmmm Wenzangu nyinyi mmenichosha. Kwa siku za mbele mkinukuu TANZANIA DAIMA nitafanya mgomo wa kusoma na kujibu.

Pumba ++
 
Kamanda! Mbona kina Mwigamba, Chagulani, wale madiwani Arusha, kina Mwampamba, Juliana, Mchange hawa wote mbona mliwafukuza, kwa nini Zitto kawashinda mnamuogopa.
...hafukuzwi kwa sababu anaandaliwa kuwa Mwenyekiti-vipi hamtaki tena awe mwenyekiti wa CHADEMA?
 
Yaani kati ya wajumbe 32 ni wajumbe 23 tu ndio wamehudhuria,ina maana wajumbe 9 hawakuhudhuria lakini gazeti la udaku Tanzania daima limemuona ZZK!!! Duh kweli vifaranga na kuku wana kazi
 
Nyie watu wa ajabu sana tafri yenu mtu akiwa muislam ndiyo anakuwa mdini, labda nisaidie unaweza kunitajia mkirsto mdini? Au amna.

Watu kama hao mimi huwa nawatamani sana Ritz,

Ni sampuli ya kina Matola hiyo,huwa sina papara nao kabisa,naenda nao taratibu,mazezeta haya...
 
Nyie watu wa ajabu sana tafri yenu mtu akiwa muislam ndiyo anakuwa mdini, labda nisaidie unaweza kunitajia mkirsto mdini? Au amna.

We are actually watching all the moves ............Wewe unaelewa vizuri sana namaanisha nini...Jamii yetu ya Kitanzania imejengwa katika misingi ya kutoulizana wewe ni dini gani na wewe ni dini gani...matokeo yake mnaleta chokochoko za kwamba sisi waislam wale wakristo...so what? kuleta hizo fikra katika jamii kwanza ni kosa kubwa ambalo nakuhaikishia as a nation hatuwezi kukubali kwa interest za maslahi yenu yawayo yote mtugawe........Watanzania wazalendo hata katika forum hii wanaona.. Ritz wewe ni moja kati ya watu mnaopenda kupandikiza migogoro katika jamii...kwa kuigawa kwa misingi ya kikabila na dini.....Kama unayafanya hayo kwa interest yako na familia yako...be careful...Wengine bado tunaipenda Tanzania..............
 
Last edited by a moderator:
ndio mi kauzu,na nakuchukia sana na magaidi wenzio,na wanajulikana.mnachukia sana kuona cdm ina wapiganaji wa dini zote,propaganda zenu zinakosa mashiko.Zitto anashikwa adabu na uislam wake fake,kama walivyoshikishwa madiwani wa Arusha wakiwmo christian
Ndiyo maana nakuambia nyie wafuasi wa Chadema mnachuki na Waislam sana, unaona unatuita sisi magaidi kutokana na Uislam wetu wewe siyo wa kwanza, ujumbe wangu kwenu pambanane na CCM msipambane na Waislam.
 
Umejiuliza kwa nini Mwananchi wameandika ;Hofu yatanda??

Mimi huwa ninasoma maudhui ya habari. Huwa sisomi magazeti kwa kutumia kigezo cha headline ambacho mara nyingi ni catchline.
Kuhusu Tanzania daima Kuandika Zitto kukacha ...mimi siwezi kuitetea Tanzania daima ....
Magazeti yote mawil yanaangalia business interest...yanaangalia yaandike vipi habari ndio yatauza copy nyingi.....
Sasa kama yote yanangalia business interest, kwa nini unakataa pale ninaposema nguzo ya Tanzania Daima ni CHADEMA. Inaonekana huelewi hata maana ya neno nguzo katika msingi wa andiko langu. Tanzania Daima is embedded in CHADEMA.
Ni akili fupi kudhania kinachoandikwa na Tanzania daima ndio kauli ya CHADEMA.....
Ndio maana umeambiwa Tanzania daima sio gazeti la CHADEMA.......
Ni kweli mtu mwenye akili fupi atadhania Tanzania Daima ni CHADEMA lakini mtu mwenye fikra na mawazo pevu atatambua kuwa Tanzania Daima imesimama kwenye nguzo za CHADEMA kutokana na maudhui yake pamoja na kwamba halikuanzishwa na CHADEMA.
Alafu...Huku jukwaani tunafahamiana na mitazamo yetu ya kisiasa...sasa wewe unataka kutuletea unafki hapa kwamba sio mtu wa CCM...Hatutaki unafki...mimi naipenda CHADEMA kama taasisi na nitaitetea misingi ya taasisi.........
Huo unafiki unao uona niwa kwako na hii inatokana na mtazamo wako unaobainishwa na uwezo wako kifikra. Wewe endelea kufikiria hivyo kwa sababu huo ndiyo ukomo wako kifikra. Mimi niko huru kusema lolote na kwa wakati wowote. Sijafungwa na vyama vya siasa nadharia.

Kama unaipenda CHADEMA, endelea kuipenda kwa sababu hiyo ni haki yako kama ilivyo haki yangu ya kutokuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania.

By the way, Mtu wa CCM anaonekana vipi na Mtu wa CHADEMA mwonekano wake ukoje na kikubwa zaidi, kwani kuwa mwanaCCM au CHADEMA ni kosa kisheria au dhambi kiimani?.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom