Zimbabwe Election: Progress & Results

Tatizo si ukoloni wala ukibaraka, tatizo ni Je? aliyenda ni nani Zimbabwe, kwa maana halisi ya Demokrasia Morgan ndiye mshindi unless tune itangaze matokeo zaidi ya siku 10 sasa, hiyo pekee inampa credit Tsvangirai kuwa ndiye aliyeshinda hoja za ukibaraka wa wazungu zinge sound sana kama matekeo yangetoka halafu akashindwa akalazimisha ushindi( Morgan)
 

hivi 2000 Bush alitangazwa mshindi baada ya muda gani?

Gordon Brown alichaguliwa na nani kuwa PM wa UK?

MT kushinda au kushindwa tutajua baada ya tume kutangaza mshindi

 

NAkuunga mkono kwa 200%! Nina wasiwasi na utimamu wa akili za Mugabe! Mugabe pamoja na wenzake kina Museveni wamepata urais miaka ya 1980's bhati mbaya au nzuri kwao ndio miaka ambayo vuguvugu la kupevuka kwa demokrasia na utawala wa vyma vingi ndio ulikuwa umefikia kwenye peak! Ile miaka ya kuwa na Rais wa maisha ndio ilikuwa imefikia ukingoni. Cha ajabu hizi figures zimekuwa na vichwa vigumu sana. bado wanafikiri kuwa waliumbwa wawe ma Rais na si mtu mwingine yoyote.

Hatima ya nchi yoyote inatakiwa iwe mikononi mwa wananchi. Kumpa mtu mmoja nguvu kwa sababu tu anaweza kuwahonga askari na majeshi ni kulisaliti TAifa. Mugabe ni mmoja wa viongozi wasio na jipya katika nchi zao. Yeye ni mpigania uhuru na si kiongozi wa nchi, ni kama Museveni. kazi zao zilikwisha baada ya nchi zao kupata uhuru.

Mugabe hapati karaha hata kidogo kwa taabu wanazopata watu wa Zimbabwe, kitu cha muhimu kwake ni kuendelea kuwa na Power na kutanua na mkewe.
 
..Zimbabwe pana kazi ngumu kwelikweli. wenye silaha hawamtaki Tsivangarai.

..tatizo la huyu Tsivangarai ni kwamba hana liberation war "credentials."

..kwa rika lake, Tsivangarai alipaswa kuwa amepigana vita ya ukombozi. lakini wenzake wanadai he was MIA.

..Makamanda wa Jeshi la Zimbabwe, time and again, wameeleza kwamba hawataki kusikia habari ya amiri jeshi mkuu asiyekuwa na liberation "credentials."

..kuwashawishi makamanda wa ZDF wamkumbali Tsivangarai ni kazi ngumu kama kushawishi Wamaasai wamteue Laigwaanan ambaye hajatahiriwa wala kupitia jando.

..wengine hapa tulieleza kwamba badala ya kum-demonize Mugabe, "wakubwa" wangemtafutia an exit-strategy.

..wakubwa burned their bridges with Mugabe, sasa hawawezi hata kumuuma sikio kama walivyofanya kwa Mzee Mwai Kibaki ambaye alikuwa na matatizo ktk kura kama haya ya
Mugabe.


NB:

..asilimia kubwa ya makamanda wa ZDF wamepitia mafunzo yao ya awali ya kijeshi hapa Tanzania.
 
Mwambie nasisi tuna tatizo kama lake huko Visiwani kwa hiyo asiwe na shaka atapigwa kalenda tu.
 
.......sumu ya nyerere hiyo, mtu akitaka demokrasia ya kweli na ku-reason na wazungu basi anakuwa labelled "kibaraka"!! kaazi ipo, yaani waya wooote huo Zimbabwe, wewe huoni??

Kama wewe ulivyoniita mimi Uncle Tom kwa sababu nina-attend The Limbaugh Institute of Advanced Conservatism....kwikwikwiiiii....na usiseme niko predictable kwa sababu ukisema hivyo na mimi nitasema hivyo hivyo kuhusu wewe...LOL
 

 
umechemsha kaka, kila kitu na mahala pake.....wrong place, wrong time!!!......labda kama unataka kuharibu mtiririko wa thread, siwezi kuwa patna wako ktk hilo! SORRY.

Nilijua tu utasema nimechemsha.....so who's predictable now?
 
Kuna mtu anaweza kunieleza why Morgan anaitwa Kibaraka na CCM washindwe kuitwa majina yote machafu kwa wizi wa wazi wa pesa zeti , kura zetu na hata kukataa mpango wa amani na maendeleo ya Tanzania kwa kuukataa Mwafaka ?
 


Same platitudes. Hii ndio legacy ya udikteta inayotutesa waafrika. Kila mtu anayepingana na watawala na kupata support ya wazungu ni kibaraka. Ajabu, wazungu hao wakiwa-support hao the so called liberation parties hatuwasemi. Sasa hivi wazungu wana mwaga misaada kibao kwa JK, ngoja siku upinzani upate nguvu, utaambiwa vibaraka wa wazungu.

Sasa huyu mwingine ni nani ambaye atapingana na Mugabe halafu mseme sio kibaraka wa wazungu? Inawzekana kweli kuna mpinzani ambaye Mugabe atamfurahia ili aonekana ana liberation credentials?
 

What does those liberation credintials means while majority in Zimb are suffering and dying of hunger and diseases in the names of Mugabe an African hero ?
 
JokaKuu: Sijui angefanyeje Morgan maana alikuwa mwanachama wa ZANU PF na hata chama cha wafanyakazi ambacho yeye alikuja kuwa kiongozi wake kilikuwa affiliate wa ZANU PF kama ilivyo COSATU na ANC.

Tusitafute sababu za kuhalalisha ujinga na uroho wa madaraka wa Mugabe. Kinachotokea Zimbabwe ndicho hicho walicho nacho viongozi wa hivi vyama vilivyokuwepo wakati wa uhuru-wanadhani wana umiliki wa kuongoza nchi zao. Tena hata ANC watakuja kuwa hivyihivyo, sasa hivi wanaonekana exceptional kwa sababu bado upinzani hauja-take off huko SA kwa kuwa bado wanapewa kura kwa sababu ya legacy ya kumaliza apartheid. In the next 10 years, ANC hawataweza kuwashawishi wapiga kura kwa sababu ya kumaliza ubaguzi wa rangi. Hiki ndicho kilichomkuta Mugabe; siku zote aliweza kuungwa mkono na wananchi kwa sababu ya liberation, lakini imefika mahala watu wanaangalia future. Sasa ndio hapa akina Morgan wanapoingia.

Hawa viongozi wanaongoza vyama vilivyokuwepo wakati wa uhuru wana taabu na mambo ya demokrasia. In fact, wangekuwa na uwezo mambo ya vyama vingi wangefutilia mbali.

 
Hivi kwa nini kila baada ya chaguzi nyingi Afrika lakini kuwe na mazingaombwe ya namna fulani? Hawa majamaa wamepiga kura sijui wiki mbili zilizopita na kwa nini hawatangazi matokeo? Sisi Waafrika tuna matatizo sana na tunakatabia kakukwepa uwajibikaji na kukataa ukweli. Mpaka sasa sijasikia maelezo yoyote yale ya kuridhisha ni kwa nini matokeo hayajatangazwa. Hata kama hakuna aliyepata asilimia imayohitajika kuitwa mshindi si wangetangaza ili watu wajue. Hii kwa kweli inakera.
 
Kitila,

..hili suala la Tsivangarai kuwa hana liberation war credentials siyo la jana au juzi. hata uchaguzi wa 2002 Mkuu wa Majeshi, wakati huo Gen.Tshivanashe, alitoa tamko kama hili lililotolewa majuzi.

..Zimbabwe ina utitiri wa matatizo yakiwemo inflation, njaa, ardhi, ukabila, siasa chafu [both zanu and mdc],foreign interference etc etc.

..kwanini watu wanashtuka leo hii kwamba Mugabe amekataa matokeo as if Tsivangarai angekubali matokeo kama angeshindwa? mazingira yaliyoko Zimbabwe sasa hivi sidhani kama they are ready for elections.

..personally sijui suluhisho la Zimbabwe ni nini. But I can tell you one thing: I AM FED UP WITH BOTH MUGABE AND TSIVANGARAI.
 


Tatizo mi nafikiri si mda lini wamepiga kura na matokeo yatoke mapema Hapana,mimi nafikiri hata yakichukua mwezi ila matokeo yawe ya haki watu waheshimu ridhaa ya wananchi.

Mimi kweli hii demokrasia inanishangaza wenda sisi waafrika tumeivamia na konskwensi zake do hizo za sisi kuonekana wendawazimu.Swali la kujiuliza kwanini Afrika??

Ukijaribu kuangalia nchi za Asia zilizo na mtindo wa kuchaguana ufalme utaona zimetulia sana kama si akina Bush ku force Demokrasia yao yenye matata siku zote.

Yawezekana kabisa tatizo la Afrika si Mugabe,si JK,si Mseven,Si kibaki bali tumeivamia demokrasia kichwa kichwa sasa Mziki umekua mzito wezetu waliotu force kubeba mzigo tusioujua (wazungu) wanatucheka na kusema Angalia watu wenye IQ ndogo wamebeba na kukumbatia mzigo wasiojua ndani yake kunanini.
 
...dawa kumaliza matatizo ya njaa,ukimbizi,inflation na udikteta ni kumvizia Mugabe na kumtwanga risasi kama walivyomfanya Savimbi na vita ikaisha,assasination kwa viongozi madkiteta wa Africa labda inaweza kufanya kazi
 
Mnaomwita MT ni kibaraka nadhani hamuifahamu vizuri historia ya Zimbabwe. Mugabe hajaanza leo kuwaita wapinzani wake ni puppets alishawaita hivyo akina Abel Muzorewa, Ndabaningi Sithole na hata the hon. Joshua Nkomo. Kwa kifupi siasa za kina mugabe ni za kishamba na za miaka ya 60. Mugabe hali yake ya kisiasa ilianza kuwa mbaya mwaka 98, 99 kumbukeni pia kabla ya hapo kuna yule mbunge independent Magreth Dongo wa Harare South aliwahi kutamka kwamba viongozi wa ZANU PF ni wanafiki, waoga na wanabehave kama wake za mugabe. (Enyways hii ni nukuu ya baadhi ya watu walioanza kumcriticize Mugabe openly). Mwaka 99 chama cha MDC kilizaliwa kutokea ZCTU (juwata ya bongo) na morgan akiwa kiongozi, Kumbukeni kwamba at this time ni wazimbabwe wachache waliokuwa tayari kumcriticize Mugabe openly kipindi hiki.. Umaarufu wa huyu jamaa uliitikisa mno serikali ya Mugabe na mwaka 2000 walishiriki uchaguzi wa wabunge na kuzoa viti 57 kati ya 120 kama sikosei. Hapo ndipo zogo lilpoanza na mibalaa yoote tunayoiona sasa Morgan akaitwa kibaraka, akashtakiwa kwa kesi ya uhaini, akadaiwa kwamba anataka kurudisha wazungu etc. etc. Baada ya hapo uvamizi wa mashamba ya wazungu with the so called war veterans (wengine ambao wana umri sawa na uhuru wa zim)ulianza rasmi it was chaotic and highly barbarian. I am sure hii haiwezi kutokea kwenye nchi yeyote ya kistaarabu. 2002 kulifanyika uchaguzi wa raisi ambao ulikuwa navitimbwi labda kuliko hata ule wa Kenya kwani kuna wapinzani walichomwa moto ndani ya gari na state security urgent sehemu ya Buhera (Huku ndiko anakotokea MT). High court ilitoa order ya kukamatwa kwa hao watu maana wanajulikana lakini mpaka leo wako huru. Uchaguzi huu uliibwa wazi wazi na vyombo karibu vyote vya uangalizi wa kimataifa except SADC vilideclare kwamba ngoma haikuwa free and fair. Hapa officially MT alishindwa kwa kura kama laki nne (400,000).

Hali ya uchumi kazidi kuwa mbaya na mbaya - watu kuikimbia nchi, na mugabe kuanza kufanya yale mambo tuliyoshindwa miaka ya 60. Akataka kuchukua shule zote ziwe za serikali, akaja na sera ya kumilikisha wazimbabwe makampuni kwa asilimia 51 (his cronies enyway), Zimbabwe will never be a colony again na mengine mengi tu. Akaanza kulaumu hali ya uchumi kwamba imesababishwa na ukame lakini baada ya mataifa ya mgharibi kuwafungia yeye na vigogo wenzake kwenda huko magharibi akasema sanctions ndiyo zinasababisha hali mbaya ya uchumi, mambo ni mengi lakini in shart huyu jamaa kwa sasa ni hopeless, hapless na liability kwa Zimbabwe, Africa na civilized world kwa ujumla.

Hivi 28 yrs baada ya uhuru wa tanganyika (1989) kuna mtu alikuwa anaomba ubunge au udiwani kwa credentials za kupoigania uhuru?? Tumeona Kenya juzi mataifa ya magharibi yalivyokuwa yakimsapoti kibaki mwanzo na baadae Raila kuna mtu alizungumza habari ya mmojawapo kuwa kibaraka?

Hata Africa kusini ambako bado vidonda vya apartheid havijapona hatujawahi kumsikia mbeki, Mandela, Ramaphosa wakidai DA ni chama cha vibaraka wanaotaka kurudisha utawala wa wazungu. Sasa huu ukibaraka wa MT unatokea wapi? Simply kwa sababu ya support ya nchi za magharibi. Let us not think that low as Mugabe and his cronies. As youths of the new and globalized world we are not supposed to play, act or live the politics of 1960's.

Mugabe should go and leave Zim and Zimbabweans alone.
 
Time runs out for Mugabe


Patrick Wilmot is based in London. He's a writer and commentator on African affairs for the BBC, Sky News, Al-Jazeera and CNN. He's a visiting professor at Ahmadu Bello and Jos Universities in Nigeria.

Time will tell .... .... ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…