Zijue Mbinu kadhaa za Kupambana na Tembo Waharibifu wa Mazao Mashambani

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,030
1. Zungushia Shamba lako na Kamba ya Katani kisha ipakae Pilipili Kali

2. Panga Matofali moja moja Kuzungukia Shamba lako lote

3. Tafuta Spika Ndogo Nne kisha zipange kila Kona ya Shamba lako kisha weka nyimbo zenye midundo ya Ngoma tupu

4. Ukiweza mtafute Mtu mwenye Pikipiki mbovu yenye Sauti Mbaya kisha kila baada ya Masaa Mawili awe anakuja nayo hapo Shambani Kwako na kupiga Misele

5. Kama katika Memory Card ya Simu una Sauti ya Mabomu ya Jeshini Kulia kwa Kulipuka au Mtu Kujamba kwa Sauti ya Mpishano ( kwa interval ) itegeshe Shambani Tembo hawatokuja

6. Tafuta Kinyesi cha Ng'ombe kilichokauka kisha Kichanganye na Pilipili kisha Kizungushie kwa Kukimwaga Shamba zima

7. Panga Magogo Kuzungukia Shamba lako lote Tembo hawatokuja

Haya mtakaotumia hizi Njia tajwa hapa mkivuna Mazao yenu kwa Wingi Msimu huu GENTAMYCINE nahitaji Gunia moja moja tu Mazao yenu sasa Ole wenu msinipe Asante yangu nitawaletea Mafuriko ya Tembo kwani nina Ujuzi wa Kutegua Mitego yote hii na Mazao yenu Kuharibiwa vibaya na mjute. ( I'm just Kidding guys )
 
Tembo alievurugwa kama huyu azuilike kwa hio mitego?
tembo-2(0).jpg
 
Huyu mnyama ni hatare,ukimkasirisha anakukanyaga Ili ufe na kama haitoshi anakuchimbia kaburi anakufukia,na anahakikisha anakaa hapo hapo hata masaa matatu Ili usije kufufuka.
 
Back
Top Bottom