Jifunze visa na mbinu za kukabiliana na wezi wa majumbani

MeinKempf

JF-Expert Member
Jun 11, 2013
11,094
7,218
Napenda tujifunze mbinu mbali mbali za ku deal na wezi na vibaka majumbani na maofisini kwetu.

Miongoni mwa mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya binadamu ni ishu nzima ya kuibiwa na wezi kama vibaka, majambazi na hata ndugu au jamaa zetu wa karibu tunao waamini.

Kumbuka nyakati hizi Vijana wengi na watu wazima wamekuwa wakijinyima sana na kujitahid kujenga walau ka sehemu ka kujisitiri (NB: Hakuna baba /mama mwenye gari bali kuna baba /mama mwenye nyumba), sasa wengi wakihamia kwenye miji yao baada ya muda mfupi au baadae sana wanakuja kuwa wahanga wa wizi.

Hapa uzi huu hata wale waliopanga kwenye hizi nyumba za watu unawahusu.

Baadhi ya mbinu ni kama zifatazo:

1- Kusali /kuswali na kuomba kwa Mungu /Allah kabla ya kulala.

Jitahidi kuwa na ratiba ya kusali na kuomba kwa imani yako na wanafamilia yako, na sio kulala kama wapagani. Mungu ana nguvu sana ya kuweka invisible security kwa mji wako. Usipuuze, kama ni mkristo au muislamu naamini wajua nguvu ya sala / swala kabla na baada ya kulala. Utaleta mrejesho wake hapa .

2- Uimara na ubora wa madirisha na milango ya nyumba husika .

Hapa Hakikisha madirisha (hasa ya jikoni, stoo, chooni na kwa watoto yako imara sana) ,epuka kujenga kwa kutumia flat bars pekee hasa hizi za mm4 au 4.5, 6 mimi nakushauri jenga dirisha lako kwa kutumia nondo nzito kabisa halafu hizo nondo waweza weka urembo wako unaotaka.

Hizo flat bar zinakunjika kama aluminium tu wezi wakija ila nondo watakuwa na kazi ya ziada kuikata, kuipinda hata kuiyeyusha kwa gesi. Waweza shituka mapema ukawadhibiti. Pia zege la kutosha na zito kwa madirisha na milango (hapa kwenye ujenzi wengi tuna puuza nguvu ya cement nzito na sio ya kuchakachua wakati wa kubandika madirisha na milango (wengi tunataka tu kuona madirisha na milango inebandikwa bila kujali uimara wake- be attentive enough.

Pia Milango ya mninga au mpingo (Iron tree and Ebony tree) ni mostly recomended. Epuka milango ya bei chee na isio imara.

3- Weka master switch itayokuwa pembeni ya kitanda cha kulala.

Hii mbinu ni nzuri sana na wengi mwaweza kuwa hamuijui, unapoweka wiring na switch za nyumba yako, weka na hiyo main switch ya kuweza kuwasha na kuzima taa zote za nje ya nyumba na hata ndani fasta fasta , ukisikia kitu hakiko sawa kwa nyumba yako, usipuuze mara nyingi huwa kweli , hivyo waweza Nyoosha tu mkono wako kitandani bila hata kuamka kitandani na kuzima kwa muda na kuwasha taa zote ...washa zima lazima wezi wanashituka na kujua kuwa huyu yuko macho , ukizima taa zote unawapoteza kabisa. Maana kuna ile uko usingizin unahisi kama kuna watu au kitu kwa nyumba yako hakiko sawa, basi wewe zima taa zote kisha washa na kuzima...nakwambia watabaki wanajiuliza kama hilo tendo ni bahati mbaya au uko macho.

Kumbuka Usipende kulala taa za vyumbani zinawaka.
NB: weka main switch vyumba vyote vya watoto, master na chooni kwa master yako. Waelimishe matumizi yake na usiri wake in case of emergence.

4- Weka alarm kwa vitasa na makufuli ya milango na madirishani. Bila kusahau kuwa na filimbi yenye mlio wa maana.

Inakuwa ni automatic alarm , yaani mlango hata uwe mzuri vipi na vitasa vyake, weweza ongeza na kufuli za alarm (hapa wenye maduka makubwa na magari wanafahamu ) wanaelewa umuhimu wake. Yaani akigusa tu mlango au dirisha na kutumia nguvu kuingia basi alarm au king'ora kinapiga hatari kiasi kwamba mtaa mzima wanashituka. Hayo makufuli yapo na alarm zake zipo hapa mjini, tena usiku mnene sauti yake inasambaa sana. Hata wakikupiga dawa ya usingizi alarm inatibua dili lao haraka sana.
Ila pia filimbi ni muhimu iwe karibu na kitanda ila eneo la siri. Inasaidia sana kutibua mipango ya wezi.

5- Jitahidi kuwa Na baruti au kingo'ra ndani ya nyumba yako.

Waweza kuwa unashangaa, ika nakwambia baruti (gunpowder) inasaidia sana, ukihisi kitu kisicho cha kawaida ukiipiga aisee lazima watafutane kwanza hao wezi (wanaweza hisi kuwa una miliki manati ya mzungu kumbe ni baruti tu). Inakuwa pembeni ya unapolala baba na mkeo. Kumbuka, ukiwa nayo inakuwa siri ya wewe na mkeo tu, tena ikibidi kainunue hata mkoani mbali kabisa. Na king'ora cha kuwatibulia ishu yao,na kinakuwa kinaamsha polo sio ya nchi hii mpaka majirani pia watashituka.

6- Weka shoti ya kurusha au kutetemesha kwa milango na madirisha. Na fence ya live kuzunguka nyumba yako.

Dirisha zako na milango unaziwekea mfumo wa kupiga shoti hasa kuanzia saa nne usiku mpaka saa kumi na moja alfajili. Isiwe shoti ya kuua, hapa nazungumzia ule umeme unaoshitua tu, tahadhari, hapa usiwekewe na vishoka watu wa umeme mnanielewa, fata taratibu za nchi na mamlaka zake. Waelemishe pia wanafamilia wako kuacha kugusa madirisha na milango usiku mnene. Najua hii ni ngumu sana , ila nzuri ukiweza masharti yake.

7- Toa elimu ya kujilinda kwa wanafamilia yako wote nyumbani.

Hapa kosa kubwa huwa ni pale baba anapojipa jukumu la ulinzi na usalama wa nyumba yake yeye mwenyewe peke yake kumbuka kidole kimoja hakiui chawa katu, kuwa una wapa elimu mke , watoto na hata beki tatu namna ya kuishi kwa tahadhari hasa nyakat za usiku, ikitokea hatari wafanyeje na pia saini au viashiria vya kuwasiliana na wana familia yako na majirani pia, hii husaidia sana wakat wa majanga ya wizi. Maana kuna muda wanaweza kukuwahi mshua, ila Dogo janja au beki Tatu akaenda kuminya alarm ya king'ora chumbani kwake, hapo wez lazima wajue wamebugi.,na watakimbia mbaya.

8- Ishi na majirani na wanafamilia yako vizuri.

Ushirikiano na wenzako unao ishi nao kila siku ni muhimu sana , hata kama una pesa zako au una hali ngumu, dont under estimate the power of neighborhood . Dharau na majivuno hayafai, wanaweza ona kitu kibaya kinaendelea kwako hasa wizi wakapiga jiiii (wakakaa )kimya kutokana na tabia zako.

9-Usilale kama pono samaki usiku.

Jitahidi kulala kisungura usiku, na jiwekee utaratibu wa kutokulala kimoja amka hata mara moja na ku survey nyumba yako , kumbuka ushakua mtu.mzima mambo ya kulala kama mtoto alalavyo uache (tabia mbaya kulala level seat na udenda juu). Kumbukeni wazee wetu wa zamani walivyokuwa makini na kulala hata kama kafanya kazi ngumu mchana kutwa.

10-Punguzeni ulevi kupindukia.

Watu wengi wanalalamika kuibiwa wakati wao wanashinda baa tena wakinywa mapombe makali makali tu, akirudi nyumbani analala kama furushi la viazi vya njombe..wezi lazima tu wakuchoree raketi maana wanajua unarudi saa sita hivyo mida ya saa nane unakuwa ulimwengu mwingine kabisa, wanazama wanafanya yao. Asubuhi ukiamka unajikuta uko wewe na mbupu zako tu.

11-weka ulinzi wa mbwa na hata security guard kama kamera CCTV na bloototh kwa vifaa vyako.

Pale inapokuwa hali yako ya kiuchumi yaruhusu. Fuga mbwa wakali wa kisasa (sio jibwa koko) hasa ndo walengwa pitbull, germanshepherd, na

pia weka mlinzi ako trained kwa ulinzi na sio babu (wa miaka 70+) kwajili ya cheap labor...cheap always cost a lot. Pia kamera za siri chumbani ,sebureni au jikoni ni.muhimu sana kuwepo na ziwe on 24/7hrs.

12-Kuwa na silaha ndogo ndogo ndani mwako.

Hasa karibu ya kitanda , vitu kama panga usiweke panga jipya, hapa nazungumzia panga lenye kutu kutu kali na lenye makali ya ncha mbele (faida zake ni 2 in 1yaani linakata na kumuachia tetenasi Hugo mwizi), pia
jambia lenye makali ya kung'aa(sharp sword),

visu vya kubonyeza Kisha kinafumuka kisu kirefu chenye makali upande na upande kama msumeno.,
Spray za pili pili kali au zile za kuwasha , na hata ikibidi tindi kali ya kupulizia kama dawa ya rungu uwe nayo pia ndani , lakini bila kusahau mkuki wenye sumu ya nyongo ya mamba au simba kiasi kwamba ukiona anapiga chabo we unamtumbua u jjicho au utumbo afu catalist yake inakuwa inakuwa nyongo ya mamba (huo mkuki umasaini au jamii za wawindaji unapatikana sana) faida zake ni nzuri.

, ili kwamba Ukihisi kuna wezi basi uweze jihami kwa silaha hizo. Hakika hata wakiwa kumi na kufanikiwa kuchoropoka na remote ya tv ila wataenda kusimuliana huko mbele ya safari juu ya shoo waliyokabiliana nayo huku wakitoa shukrani za kunusulika kuungana na Israel mtoa roho.

13-Kuweka gadget za security kwa vifaa vyetu muhimu nyumbani.

Hapa vitu kama falt screen t.v ,computer, radio, simu, na vinginevyo vyaweza wekewa tracing gadget kiasi kwamba vikiibwa waweza trace na kufanikiwa kuvidaka kisha ukapata mwizi wako. Hapa yakupasa kuwa una andika baadhi ya fitures muhimu za vity vyako (kwa waliopitia kamali wanajua kitu yaitwa macho kwa karata) kwa diary yako ina case ukimkamata unaanza kutaja alama na baadhi ya taarifa muhimu kwa kitu chako. Sio una nunua kitu cha thamani aafu vikiwekwa hapi 2 vinavyofanana unashindwa tofautisha , utakuwa uzembe na uzururaji.

14-Kuwa mtu wa mazoezi na sio kuwa mzembe mzembe ka Dan mtoto wa mama.

Hasa madingi na vijana wa siku hizi wazembe sana kazi kufuga vitambi tu...fanyeni mazoezi uwe fiti kiakili na kimwili (be fit psychologically as well as physically), use na uwezo wa kusimamia shoo ya varangati au tifu kwa dakika kumi bila ya kukata pumzi. Na sio kuwa nyoro nyoro kama mchicha mwiba.

15-Kuleni chakula cha usiku mida ya usiku wa manane na kwa ratiba maalumu.

Simaanishi kuka ugali maharage saa nane usiku, lahasha ,hapa ina wahusu wana ndoa, acheni tabia Ya kubanjuka SAA mbili kila baada ya kumaliza kula, pumzikeni kwanza kisha muamshe popo kuanzia saa sita, saba au nane usiku. Hakika wezi wakija watawakuta mko macho , hapo ndo watapokuwa wanasonya na kuondoka wenyewe kwa jazba. Na pia sio kukamuana kwa fujo kila siku, mnachosha sana miili kiasi kwamba mkilala ni kama dead body..kulaneni kwa ratiba maana hiyo kitu si mchezo.
Mkimaliza mtalala kama gunia la mbaazi toka manyara.

16-usipende karibisha kila mgeni ndani mwako.

Fatilieni wenye nyumba zao za maana
wanavyokuwaga na tu viti nje kama ka kijibanda ka makuti au ka ibaraza ka nje basi kanawekwa viti viwili vitatu na meza , hapo mnaweza kula na kunywa na kupiga soga lenu na hata kunywa hapo hapo nje bila ya kuingia ndani kwako mpaka majogoo. Hapo unadhibiti wachora ramani kwa kupiga chabo kwani wakipata upenyo wa kukaribishwa ndani tu wamenasa Raman nzima (na wengi tunalizwa hapa pasipo kujua), wema usipitilize na kama ikibidi basi kutana na marafiki na jamaa viwanja vya mbali kama baa au beach au hotel hata ikibidi beba familia yako mkamalizane mbali mbali. Pls trust no body.

17-kuwa makini na madalali wa nyumba, mafundi (ntawataja), wenye nyumba na wale wanaobeba mizigo yetu siku ya kuhama.

Tulio panga tuna dhani tumemaliza kazi kwa kumuamini sana dalali anayejua in and out ya nyumba au chumba chako, pls kuwa makini
Watu hawa maana waweza uza ramani ya nyumba yako.kwa wazee wa kazi. Angalieni sana mitandaoni watu wanaiacha nyumba in and out.wakati wa kusaka wateja ..sasa wewe ukiingia ndani wajiona.umemaliza
Unapigwa tukio unashindwa unganisha dots...

Mafundi ujenzi wa nyumba zetu, mafundi milango na madirisha, mafundi umeme, boda boda na watu wengine wote ...tuwape kazi zetu ila tukae nao kiintelijensia , usimwamini sana kama mkeo au mumeo, wengi wameumiza watu, mpe kazi ikiwezekana under close or regular supervision.
Wenye nyumba nao mmmmh...wengine ukakasi wanakuchora tu.unavyoingiza mavitu ya thamani, mwisho wa siku wana kuchomesha kwa.wana wanafanya yao na wao kugawana mgao.

18-Mwizi ukimdaka mpe kichapo na adhabu heavy mpaka iwe historia kwake maisha yake yote.(kill him not, let him go)

Endapo utafanikiwa kumkamata mwizi wako wakati akitenda uhalifu wake..mtandike au hata kumuachia alama atazoeda kuwasimulia wenzake, wake zake ,watoto zake na pia kubaki nazo maisha yake yote , ila usiue pls. Ila adhabu zao zipo nyingi tu ..dont kill him/her pls. Ili akawe balozi mzuri huko aendako.

19-Tuweni makini na mademu au ma boyfriend .

Hii ni kwa wote KE na ME , mnakuwa kwenye mahusiano na mwenzio tena ya muda mrefu huku mki share in and out za maisha yenu ya kila siku, afu mkimwagana kuna uwezekano mmoja wenu akamchoresha kwa wana zilipendwa wake hata kama ni baada ya miez 6 au mwaka.
Chamsingi kama umepanga basi hama na eneo mlilokuaa mkiishi na zilipendwa wako na.kama nyumba inavyumba vingi waweza haa.vyumba akihama mpangaji ili tu kuwapoteza maboyaa au ukishindwa kabisa kata nae mazoea kabisa. Na kama umejenga jitahid kuanza kuishi kwa umakini sana kuanzia hapo . Wengi hulizwa na wandani wake kama tu njia ya kumkomoa.

20-Kuwa una lala usiku kwa kuweka miziki yenye tungo tata kwa sauti ya chini.

Sio kuweka.miziki laini laini kama ya blues...mwanaume wa kweli unaweka miziki migumu Usiku (yakupasa kuwa na kaflash kako au cd maalumu )yenye compilation ya nyimbo zenye tungo tatanishi kwa wezi mfano mimi nina flash yenye nyimbo kama:

(a)sijalala mwanangu Utauwawa bureeee....,
(b) Parapanda italia parandaaaa...nao wengine watakuwa wamekwisha kuondokaaaa kwenda....
(c)itakuwahuzuni kwa ndugu na masela safari yako itavyofika ya kwenda ahela..kamanda wa daz nundaz
(d)kama noma na iwe noma sikubali leo narivenji mimi...
(e) mikono juu mwendo wa mateka mikono juu...
(f)Pale kati patamu ....mwizi anajua nikidakwa wimbo huu utamuhusu.
(g) mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe...
(h) maisha ni mapambano...
(i) Mikononi mwa polisi....by sugu / Mr. II

Yaani hiyo hata wakinyemelea dirishani kwako wakikuta nyimbo hizo zinapigwa watakuwa na mawazo sana nini lengo la kuwekewa nyimbo ngumu kama hizo badala ya byimo laini za kusindikiza usingizi. Kumbe ni mbinu zako tu za kujihami

21. Fanya vetting ya beki 3 au mtu mwingine unayetaka kuishi nae.

Hapa zama hizi kulingana na ugumu wa malezi au kujifanya tuko bize na maisha basi tunachukua beki Tatu yeyote bila hata ya kumfanyia uchunguzi wa kina, mwisho wa siku wengine ni washirika wa wezi. Ila pia ishi nae vizuri, stigmatization is strictly prohibited, usimnyanyapae kumbuka yeye ndio anaachiwa nyumba yako au chumba chako wakati wewe haupo.

22. Jiunge na klabu za mazoezi hasa za karate au mapigano.

Wewe huendi kuwa bondia mkamiaji, hapana we unakuwa unapiga tizi na kupata skills mbili Tatu za kujihami, sio mdingi mzima unakuja kuzabwa vibao na makonzi na tutoto twa miaka 20 (maana wezi wengi ni kati ya 18-35) tena mbele ya mkeo na watoto wako. Ila ukiwa na mbinu za mapigano walau utaonesha utofauti, hata kichura, push ups na kuruka kamba kunasaidia sana.

23. Kuwa unakaa kijiweni kitaa hata nusu SAA Mara moja moja ukipata nafasi.

Hii husaidia kuwa social na wana, unawanunulia "mambo yao" hata buku 3 tu wao inawatosha huku mnapiga mastori ya uongo na ukweli, hapa vibaka na wezi mtaani unakuwa une wa neutralize maana wanakupa data mbali mbali nawe unakuwa msela wao, hata usiku wanapita mbali kwani wanakuwa wanaona soo kukufanyia umafia

24. Peruzi social media kama JF usiku mnene.

Hapa unakuwa una soma nyuzi mbali mbali usiku mnene(mshana junior time...ahaaa just mocking) kiasi kwamba wakija kuzunguka nyumba yako, wewe unakuja fungua Uzi huu na kuchukua mbinu mojawapo haraka haraka kwàajili ya kukabiliana na tishio husika. Watasonya na kusepa

25. Epuka kulala huku feni inakupepea na pia kulala sehemu moja siku 365 za mwaka.
Feni hasa wale wa sehemu za joto kama Dar, kulala nayo karibu huku inakubembeleza siopoa, hapo unakuwa kama panga anavyokung'ata huku anakupulizia, utakuja kuibwa hata wewe mwenyewe.

Pia badili style na angle za kitanda chako mshua Mara kwa Mara hata kila baada ya miezI sita, na ikibidi siku nyingine unalala sebureni (hapa usilale kwaajili ya masherti ya mganga), hapa unawapoteza maboya...wakiingilia sebureni wanakodhan hakuna MTU, wakipiga chabo tu wanakukuta maana umetulia sebureni tuliii na booonge la rungu kama la kuulia noa (mdudu).

26. Usilalae huku unakoroma kama ng'ombe anayechinjwa.

Hakuna kosa kubwa kama mdingi mzima au maza house kulala unakoroma kama unakata roho (matukunyema na mabonge nyanya inawahusu) hii wakisikilizia tu mlio wao wanazama ndani maana kukoroma bindamu unakuwa hauna fahamu za kibinadamu. Usikorome kama kikongwe.

NB: Mimi ni raia tu niliyeamua ku share nanyi baadhi ya mbinu hizi na maarifa. Naruhusu kukosolewa hasa kwa kujenga (constructive cristism) ,kwani sijakamilika na ndio maana nimekaa chini nikaumiza kichwa hivyo na kuja na mambo hayo tajwa, pls mkisambaza kwa magroup yenu basi mfanye acknowledgement kwa JF Platform.

Pia mtanisamehe kwa TYPO za hapa na pale maana kuandika kuwa kutumia simu si mchezo.

Asanteni na karibuni sana kwa mawazo mbadala.
 
Hapo kwenye adhabu umenikumbusha niliwahi kumfungia mwizi choo cha wageni wiki nzima. Nilikuwa nampa maji glass moja asubui, slace tatu za mkate mkavu mchana na kijiugali au kisosi cha wali usiku. Aliwataja wenzie polisi wakawadaka. Toka siku iyo mtaani naitwa mjeda
 
Back
Top Bottom