Unahitaji mtaalam wa kilimo wa kukuongoza namna bora ya kuzalisha mazao yako na kuyafanyia certification?

kilimomaarifa.tajiri

JF-Expert Member
Sep 8, 2015
574
409
Salaam ndugu zangu

-Je unahitaji mtaalamu mshauri wa kukuongoza namna bora ya kulima mazao mbali mbali (Mazao ya Horticulture (Parachichi, Nyanya, Hoho, Tikiti Maji, Kabichi, Karoti, Pilipili kali, Vitunguu maji, Viazi mviringo, , Cereals (Nafaka-Mahindi, Mpunga n.k), na Beverage (Hasa Kahawa)?

-Je tayari una mazao shambani lakini unahitaji mtaalamu wa kuku guide/kukuongoza kitu cha kufanya shambani kila siku mpaka siku ya kuvuna na kwenda sokoni ( Kudhibiti wadudu, na magonjwa?

-Je nyinyi ni wakulima (KIKUNDI/Ushirika) mnahitaji mataalamu wa kuwaongoza katika namna bora ya kuzalisha mazao yenu pamoja na kupata soko zuri?

Je nyinyi ni wafanyakazi ambao mpo shirika fulani, na mnafanya Certification standards mbalimbali (Kama UTZ/RFA, GLOBAL GAP, RFA, 4C, ORGANIC, Fair trade n.k), Lakini hamna ujuzi wa kutosha au mpo na Non Conformities lakini hamjui namna ya kuzifunga ili mpate cheti?

KARIBUNI TUWASILIANE


Huduma ninazo zitoa


-Naandaa mipango kazi ya uzalishaji wa mazao mbali mbali (Mpango kazi una beba, mahitaji yanayotakiwa, gharama na kiasi cha malighafi, mtaji unaotakiwa, uanzishaji kitalu, usimamizi /kazi za kila siku shambani, matumizi ya pembejeo zote (madawa na mbolea) na vipimo, kuvuna na hadi sokoni (Kuna wanunuzi ntakuunganisha nao)

-Kuna miongozo (Vitabu), soft copy ambazo zinakuelekeza namna ya kulima zao husika, hatua kwa hatua, hali ya hewa inayotakiwa mahitaji yanayotakiwa, gharama zake, namna ya kudhibiti wadudu, magonjwa

-Kutoa miongozo ya kila siku, kwa mazao ambayo yako shambani ( mfano namna ya kudhibi wadudu na magonjwa, mbolea, utunzaji wa jumla wa mazao n.k)

-Kundesha mafunzo/ kujenga uwezo juu ya kilimo bora cha mazao mbali mbali kwa Wakulima (vikundi au Ushirika au Estate)

-NAOMBA NITOE ELIMU KIDOGO SANA KWA WALE AMBAO NI WAGENI KABISA KWA MAMBO YA CERTIFICATION:

*Maana ya Certification: Huu ni utaratibu/Mfumo wa wa kidunia wa kuzalisha mazao kwa kufuata masharti ya walaji/Wateja.

* Hivyo walaji (Wateja) wameweka masharti mbalimbali (Ya kijamii, kiuchumi na Kimazingira) ya namna bidhaa anayoitaka, namna gani iandaliwe, kwa mfano wapo wanaokwambia usitumie madawa ya viwandani, au pembejeo baadhi za viwandani (Organic Certification), kuna wengine wanaangalia zaidi maswala ya kimazingira na Uchumi (RFA certification, UTZ, Cafe Practices (Mnunuzi mkuu wa bidhaa za standard hiyo anaitwa Starbucks-USA), Global GAP certification), Maswala ya kijamii (Fair trade Na 4c Certification na 4C ).

*Fahamu kwamba bidhaa ya kilimo inayoenda nje ya nchi ikiwa Certified, huwa na bei kubwa sana, Mfano mdogo tu Parachichi moja aina ya Hass ambayo bado haijawa Certified linauzwa mkoani Njombe Tsh 300-Tsh 500, Ukienda nchi kama Uholanzi/Ubeligiji kwenye super market parachichi moja inauzwa dola 1-2 za kimarekani, hapo kabla ya kuwa Certified, lakini ukilikuta liko Certified (Organic/GLOBAL GAP) linauzwa hadi dola 5 za kimarekani

* Faida za kuwa Certified: 1. Unatimiza matakwa ya mteja, 2. Unamfanya ajiamini kuwa anakula bidhaa bora hivyo yuko tayari kulipa pesa yoyote apate kile kilochobora (Kilichothibitishwa kimataifa). 3. Pia kama ni wakulima wakiwa Certified, baada ya mauzo ya bidhaa zao wanunuzi huleta Premium (Shukrani/Nyongeza ya bei) kwa wazalishji, hapo premium inatofautiana kutoka standard moja hadi nyingi (Ziko standard ambazo mnunuzi analeta nyongeza ya Usd 3 kwa kila kilo 50 za mzigo alizonunua, zipo standard wanunuzi wanaleta Usd 5 kwa kila mzigo alionunua, Zipo standard kama Organic au Fair-trade Mnunuzi analeta Usd 22/ kilo 50 za mzigo alizonunua.

*Kila Certification standard ina kanuni na taratibu zake, uhai wa cheti, Pembejeo zinazoruhusiwa kutumika na zisizo ruhusiwa kutumika

*Tangu kuanza maandalizi ya kuwa certified, mpaka kufanyiwa ukaguzi na Certification body kama Ceres, Parner Africa, Afri Cert, Imo/Eco Cert, mpaka kupata cheti, unahitaji si chini ya miezi 6 ya maandalizi

*Ili uweze kufanya Certification, Unahitaji mtaalumu wa kukuongoza katika masuala mbali mbali, mfano Kukusaidia kufanya analysis ya shamba lako (Eneo lako unalotaka kulima mazao), kukuandalia miongozo mbali mbali kama, Dodoso, n.k ICS, Farm management plan, Social, Economic and Environmental Policy, Farm/Farmer List, kuandaa checklist, Crop Monitoring program, Risk analysis n.k.

*Baadhi ya mazao yanayofanyiwa Certifation (For export Purpose) kwa Tanzania hapa ni Mazao ya Horticulture (Parachichi, Nyanya, Maharage mateke-French beans), Viungo (Mdarasini, Iriki, Tangawizi), Beverage (Kahawa, Cocoa), Katani, na Ufuta

Kama unajambo lolote unahitaji utaalamu wangu karibu tuwasiliane

Gharama zangu ni nafuu sana na Mazungumzo yapo
1. Gharama ya kupata miongozo mbalimbali (PDF-Softcopy) ya namna ya kulima kila zao, Kila PDF ni tsh 10,000
2. Gharama ya kuongozwa namna ya kusimamia miche yako shambani, gharama ni tsh 30,000/ siku 30
3. Gharama ya kufundishwa na kuandaliwa documents zote za Certification, hadi kupata cheti cha ubora, (Gharama za hapa ni maelewano kutegemea na aina ya kazi na mahali kazi inapofanyika)
4.Kujibu maswali ya kilimo kwa njia za text/meseji za kawaida au WhatsApp (Kila swali ni Tsh 5000)

KARIBUNI SANA
-Nina uzoefu wa miaka 10 wa kufanya kazi hizi za kilimo (Crop Agronomy +Certifications)
-Simu: 0744302645 (Whats App)
-Email. kilimomaarifa.tajiri@gmail.com/tulime.pamojatz@gmail.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom