Zifahamu hatua halisi za kutoa gari kwenye Meli na bandarini

kayeja jr

Member
Dec 14, 2021
9
36
Katika mfululizo wa makala za bandari, leo tunakuletea utaratibu unaotumika kuhudumia shehena ya magari hatua kwa hatua katika bandari za TPA, kuanzia meli inapoingia bandarini, gari linavyoteremshwa kutoka melini na linavyopokewa bandarini, gari linavyotoka bandarini hadi mteja kukabidhiwa gari lake.

Ukaguzi baada ya meli kuwasili bandarini
Hatua ya kwanza inayofanyika baada ya meli kuwasili bandarini ni ukaguzi unaofanywa na Idara za Serikali za Afya na Uhamiaji kwa meli na mabaharia. Hii inafanyika ili kujiridhisha juu ya afya za mabaharia na hakuna mzigo hatarishi ndani ya meli.

Idara ya uhamiaji ina jukumu la kuhakikisha kuwa taratibu zote za uhamiaji zimezingatiwa na mabaharia. Wakati taratibu za ukaguzi zinafanyika bendera ya Shirika la kimataifa la Bahari duniani (International Maritime Organization – IMO) inakuwa inapepea kwenye meli na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka ndani ya meli. Ukaguzi ukishamalizika bendera ya IMO inateremshwa ili kupandishwa bendera ya Tanzania.

Baada ya ukaguzi kinachofuata ni Wakala wa Meli (Shipping Agent) husika kuingia na genge maalumu ambalo jukumu lake ni kufungua mikanda ya kufungia magari ili yasigongane ndani ya meli na kusababisha uharibifu.

Kukamilika kwa hatua hii kunatoa nafasi kwa madereva wa TPA kuingia ndani ya meli ili kuanza kazi ya kuteremsha magari.

Ukaguzi wa magari baada ya kuteremshwa kutoka melini

Baada ya magari kushushwa kutoka melini, hupelekwa kwenye gati (quay side) Karani wa TPA huyapokea kwa ajili ya ukaguzi. Ukaguzi huo una lengo la kutaka kujua hali ya magari kabla ya kuteremshwa. Ukaguzi ukionyesha kuwa gari lipo salama, halikupata hitilafu yoyote, gari hilo litabandikwa stika ya rangi ya kijani yenye alama ya vema (√).

Endapo gari litabainika kuwa na hitilafu ya kuharibika au kukosekana kwa vifaa kama redio, vifaa vya kupandishia vioo (power windows), vioo (side mirrors) nakadhalika gari hilo litabandakwa stika nyekundu yenye alama ya kosa (X).

Baada ya ukaguzi kukamilika, karani atajaza fomu maalumu inayotambulika kama Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT). Fomu hii huonyesha hali halisi ya gari lilivyoshuka kutoka melini na kupokewa bandarini.

Fomu ya VDITT ikishajazwa kwa gari husika nakala moja huwekwa ndani ya gari kwa uthibitisho, kisha gari hilo hupelekwa eneo/ yadi kwa ajili ya kuhifadhiwa ili kusubiri mteja husika aje kuchukua gari lake.

Baada ya gari hilo kufikishwa yadi, askari wa TPA aliyepo yadi atalikagua tena kwa kutumia fomu ya VDITT na kupewa nafasi (position) kwa kuandikwa juu ya bonnet au ubavuni sehemu ya milango.

Gari likisha hakikiwa kuwa limeshuka kutoka melini, karani ataingia kwenye mfumo wa mizigo wa TPA (Cargo system) na kulipigia tally kulihesabu kuwa limeshuka, kisha ataingia katika mfumo wa TANCIS ili kuonyesha (carry in) kuwa gari husika limeshuka kutoka melini na lipo bandarini.

Majukumu ya Wakala wa Forodha katika kutoa gari bandarini

Wakala wa Forodha aliyechaguliwa na mteja kwa ajili ya kumsaidia kutoa gari lake bandarini atatakiwa kufuata taratibu za kiforodha kwa niaba ya mteja ikiwa ni pamoja na kupata vibali kutoka mamlaka husika hususan Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kulipia TRA na kwa Wakala wa Meli ili kupata nyaraka za kutolea gari (release order na delivery order).

Baada ya kukamilika kwa hatua hizo, Wakala wa Forodha ataingia kwenye mfumo wa kulipia wa TPA (e-payment) na TPA itazifanyia tathimini gharama za huduma ambazo imezitoa kwa gari husika ili kupata tozo za bandari kwa gari la mteja. Taarifa hizi zitamfikia Wakala wa Forodha kwa njia ya electroniki kwa kumpatia namba ya kumbukumbu kwa ajili ya kulipia (payment reference number - PRN).

Baada ya Wakala kupata PRN atatakiwa kwenda kwenda benki mojawapo kati ya TIB, NMB, CRDB na Standard Charted au kwa njia ya simu ili kulipia malipo ya tozo za TPA kwa niaba ya mteja.

Wakala akishakamilisha malipo ya TPA ataingia katika mfumo wa mizigo wa TPA (cargo system) kwa ajili ya kutengeneza kibali (announcement) cha kuonyesha gari analotaka kulitoa kutoka bandarini kwa kujaza taarifa zote zinazohusu gari hilo.

Wakala akishakamilisha hatua hiyo atafika bandarini kwenye ofisi ya TPA geti namba 2 na atapewa kibali cha kuruhusiwa kuchukua gari la mteja wake (gate in ticket). Kibali hicho kitakuwa na maelezo yote aliyoyajaza wakala kwenye announcement. Gate in ticket itaambatishwa na nyaraka nyingine ambazo ni Bill of Lading, Delivery order na Release order.

Wakala kuchukua gari bandarini

Baada ya kukamilisha hatua tajwa hapo juu, hatua inayofuata ni wakala kwenda katika ofisi za Kitengo cha Magari kwenye yadi husika (delivery yard) ambako kuna gari la mteja wake, kisha ataonyesha nyaraka kwa ajili ya kutoa gari husika. Karani na askari wa TPA (Incharge) watakagua nyaraka zote ili kujiridhisha kama hatua zote zimefuatwa.

Endapo itabainika kuna hatua ambazo hazijakamilika, wakala atatakiwa kukamilisha hatua hiyo au kufanya marekebisho mahali alipokosea. Baada ya kujiridhisha kwamba hatua zote zimefuatwa, karani ataingia katika mfumo wa TPA wa mizigo ili kupiga truck tally kwa gari husika na kutoa gate pass A itakayomruhusu wakala kuchukua gari la mteja wake.

Karani atasaini sehemu husika katika gate pass A na wakala wa mteja atasaini kuonyesha amepokea gari hilo baada ya kujiridhisha kwa kulinganisha taarifa iliyopo kwenye nyaraka na namba ya chasis ya gari la mteja.

Pia, karani wa TPA atatakiwa kujaza fomu ya makabidhiano ya gari (Vehicle Hand Over Form) ambayo itaelezea hali halisi ya gari wakati wa kulikabidhi kwa Wakala wa Forodha kwa niaba ya mteja.

Fomu hiyo itasainiwa na msimamizi wa yadi, askari wa yadi na wakala wa mteja, kisha wakala atachukua gari la mteja wake. Karani baada ya kutoa gate pass A ataingia kwenye mfumo wa TANCIS na kufanya carry out kwa gari husika ikiwa ni hatua ya kuonyesha kuwa gari hilo halipo tena bandarini na limeshatoka nje ya bandari.

Wakala atachukua gari la mteja wake pamoja nyaraka na kwenda nazo getini askari atazipokea nyaraka hizo na kuzikagua kisha kukagua gari husika na akishajiridhisha kwamba hakuna tatizo ataingia kwenye mfumo wa mizigo wa TPA na kuonyesha kuwa gari husika limeshatoka nje ya bandari (gate out).

Mteja anapopokea gari lake kutoka kwa wakala wake wa forodha ni lazima ahakikishe anapata nyaraka zote zilizotumika kulipia na kutolea gari lake.

Ni muhimu sana kwa mteja kupata fomu ya ukaguzi wa hali halisi ya gari lilivyopokewa bandarini Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT) na fomu ya makabidhiano ya gari kati TPA na wakala wa Forodha Vehicle Hand Over Form.

Endapo mteja hatapewa fomu hizo na Wakala wake anatakiwa kutoa taarifa TPA kwa kupiga simu au kutuma meseji za bure za TPA kutoa taarifa ili wakala husika achukuliwe hatua zinazostahiki, namba hizo ni 0800110032 au 0800110047.
 
Naongezea, kabla ya Meli ya magari kufika.

Mnunuzi akinunua gari Kwa kupitia ma agent hupewa taarifa za Meli gari iliyopakiwa na Estimated Time of Arrival (ETA) katika Bandari ya Dar es Salaam. Hivyo unaweza ukaanza kuitrack Meli Kwa kupitia Vessel Finder au Marine Traffic.

Shipping Agent wa Meli ya magari hupeleka taarifa TPA kuwa anataraji kuleta Meli, hivyo hutoa taarifa za Meli na mzigo utaoshuka au kupakiwa. Hapo hiyo Meli itaanza kuonekana katika website ya bandari kwenye kipengele Cha TPA Daily Shipping List na hii hutolewa Kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa baada ya kikao Cha ship planning kuhusu Meli za kuingia na kutoka.

Meli ikiishafika Tanzania eneo la nje la bahari (Outer Anchorage Area) Captain wa Meli hutuma email Kwa agent kutoa taarifa ya kufika, ambapo watatoa muda wa kufika (End of sea passage), Kisha kama Meli ipo tayari taarifa ya kuwa tayari kwenda kushusha bandari hutolewa (Notice of Readiness).

Hapo Kwenye Notice of Readiness(NOR) Meli inaweza isitoe muda huo huo endapo Kuna marekebisho au kuweka vitu sawa Ili wakifika bandari waanze kazi Direct.

Baada ya NOR kama agent wa Meli (Shipping Agent) alikamlisha kulipa malipo ya kuingiza Meli (Mfano; Tugging, Pilotage, Wharfage) Captain hupewa taarifa ya kuomba nafasi ya Pilot kuja kuifata Meli(Pilot Booking) Ili waingie bandari.

Pia Meli inaweza ikawa imekamilisha malipo na nafasi ya gari(Berth) hakuna hivyo Meli itashusha nanga (Anchor down) kusubiri nafasi Bandari, vivyo hivyo kama malipo hayajakamilika watashusha nanga.

Meli kuingia bandari huwa baada ya Pilot kuwa Booked muda ukifika pilot hupelekwa nje au eneo Meli ilipo na boti ndogo(Pilot Boat) hii huambatana na taarifa ya kuingia Meli ambayo hutolewa Control Tower na Mooring Gangs (wafunga meli). Kisha hupanda melini Kwa kutumia ngazi maalum iliyopo pembeni ya Meli (Pilot Ladder) Kisha hupokelewa na kukaribishwa kwenda sehemu ya kuongozea Meli (Ship Bridge) ambapo hatakuwa anakuwa na Captain wa meli kuelekeza meli iingie vipi na namna Gani itafunga katika gati la Bandari.

Meli inapoingia Bandari baada ya kuvuka eneo la ferry Tug Boat husogea Kwa ajili ya kuipa Meli msaada wa kufunga kwenye gati. Baada ya Meli kusukumwa mpaka kwenye gati zoezi la kuifunga kamba (Ship Mooring) huanza ambapo Kamba ya kwanza (First line) hufungwa mbele na nyuma, Kisha kamba nyingine na kumalizika kamba ya mwisho(Last line) zoezi hili wastani huchukua Kuanzia robo saa mpaka nusu saa.

Baada ya kumaliza kufunga kamba ngazi ya kupandia melini hushuka (Gang way) ili Pilot ashuke na Maafisa wa Afya waweze kuingia Kwa ajili ya ukaguzi.

Pilot hushuka Kisha Maafisa Afya wa Bandari (Port Health Officers) nao hupanda melini Kwa ajili ya ukaguzi. Kipindi Maafisa Afya wanapanda melini Meli hupeperusha Bendera ya njano kuonyesha kuwa Meli Bado haijakidhi Watu kuingia (No permit granted for anyone to board). Muda ambao Watu wa Afya wapo Melini mlango wa kushusha magari (Lamp) huanza kufunguliwa na mabaharia na kuweka vitu sawa Kwa zoezi za upakuzi.

Baada ya Watu wa Afya kumaliza ukaguzi wa Meli na kukagua magonjwa ya mlipuko, usafi wa Meli na vipimo vya COVID-19 hutoa taarifa kuwa Meli ipo salama Kisha Bendera ya Njano hushuka kitendo hiki Cha Meli kuwa sawa na ruhusa ya wengine kuingia Kwa ajili ya kazi huitwa Free Pratique Granted.

Maafisa Afya wakishuka ndipo Maafisa Uhamiaji, Forodha(TRA), Shipping Agent na TPA officer na madereva hurusiwa kuingia melini Kwa ajili ya taratibu za kushusha magari.

Maafisa uhamiaji huomba list ya mabaharia na passport zao, Mtu wa TRA hukagua store na kuweka seal Ili kuzuia mizigo na vitu vyao vikaingia nchini bila kulipa Kodi, Mtu wa Port Security huomba documents za meli, mabaharia na utaratibu wa meli kuhusu wageni wanapoingia kuhakikisha hakuna wazamiaji wakati wa kutoka au wizi (International Ship and Port Security {ISPS} level 1) ambapo wataweka visitors log book, vitambulisho vya meli na ukaguzi Kwa aingiaye na kutoka. Mtu wa Port Operation huomba documents za kuonyesha mzigo wa kushuka Dar na kupanga utaratibu wa namna Gani madereva watafanya kazi.

Baada ya Hapo magari huanza kutolewa Kwa kushuka Kwa njia ya kuendeshwa, muda wa Kuanza Operation ni pale gari la kwanza linaposhuka na muda wa kumaliza ni pale gari la mwisho linapomalizika.

Utaratibu unaofata kama ndugu mtoa mada alioanza mpaka kumfikia mteja wa gari husika.
 
Katika mfululizo wa makala za bandari, leo tunakuletea utaratibu unaotumika kuhudumia shehena ya magari hatua kwa hatua katika bandari za TPA, kuanzia meli inapoingia bandarini, gari linavyoteremshwa kutoka melini na linavyopokewa bandarini, gari linavyotoka bandarini hadi mteja kukabidhiwa gari lake.

Ukaguzi baada ya meli kuwasili bandarini
Hatua ya kwanza inayofanyika baada ya meli kuwasili bandarini ni ukaguzi unaofanywa na Idara za Serikali za Afya na Uhamiaji kwa meli na mabaharia. Hii inafanyika ili kujiridhisha juu ya afya za mabaharia na hakuna mzigo hatarishi ndani ya meli.

Idara ya uhamiaji ina jukumu la kuhakikisha kuwa taratibu zote za uhamiaji zimezingatiwa na mabaharia. Wakati taratibu za ukaguzi zinafanyika bendera ya Shirika la kimataifa la Bahari duniani (International Maritime

Organization – IMO) inakuwa inapepea kwenye meli na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka ndani ya meli. Ukaguzi ukishamalizika bendera ya IMO inateremshwa ili kupandishwa bendera ya Tanzania.

Baada ya ukaguzi kinachofuata ni Wakala wa Meli (Shipping Agent) husika kuingia na genge maalumu ambalo jukumu lake ni kufungua mikanda ya kufungia magari ili yasigongane ndani ya meli na kusababisha uharibifu.

Kukamilika kwa hatua hii kunatoa nafasi kwa madereva wa TPA kuingia ndani ya meli ili kuanza kazi ya kuteremsha magari.

Ukaguzi wa magari baada ya kuteremshwa kutoka melini
Baada ya magari kushushwa kutoka melini, hupelekwa kwenye gati (quay side) Karani wa TPA huyapokea kwa ajili ya ukaguzi. Ukaguzi huo una lengo la kutaka kujua hali ya magari kabla ya kuteremshwa. Ukaguzi ukionyesha kuwa gari lipo salama, halikupata hitilafu yoyote, gari hilo litabandikwa stika ya rangi ya kijani yenye alama ya vema (√).

Endapo gari litabainika kuwa na hitilafu ya kuharibika au kukosekana kwa vifaa kama redio, vifaa vya kupandishia vioo (power windows), vioo (side mirrors) nakadhalika gari hilo litabandakwa stika nyekundu yenye alama ya kosa (X).

Baada ya ukaguzi kukamilika, karani atajaza fomu maalumu inayotambulika kama Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT). Fomu hii huonyesha hali halisi ya gari lilivyoshuka kutoka melini na kupokewa bandarini.

Fomu ya VDITT ikishajazwa kwa gari husika nakala moja huwekwa ndani ya gari kwa uthibitisho, kisha gari hilo hupelekwa eneo/ yadi kwa ajili ya kuhifadhiwa ili kusubiri mteja husika aje kuchukua gari lake.

Baada ya gari hilo kufikishwa yadi, askari wa TPA aliyepo yadi atalikagua tena kwa kutumia fomu ya VDITT na kupewa nafasi (position) kwa kuandikwa juu ya bonnet au ubavuni sehemu ya milango.

Gari likisha hakikiwa kuwa limeshuka kutoka melini, karani ataingia kwenye mfumo wa mizigo wa TPA (Cargo system) na kulipigia tally kulihesabu kuwa limeshuka, kisha ataingia katika mfumo wa TANCIS ili kuonyesha (carry in) kuwa gari husika limeshuka kutoka melini na lipo bandarini.

Majukumu ya Wakala wa Forodha katika kutoa gari bandarini
Wakala wa Forodha aliyechaguliwa na mteja kwa ajili ya kumsaidia kutoa gari lake bandarini atatakiwa kufuata taratibu za kiforodha kwa niaba ya mteja ikiwa ni pamoja na kupata vibali kutoka mamlaka husika hususan Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kulipia TRA na kwa Wakala wa Meli ili kupata nyaraka za kutolea gari (release order na delivery order).

Baada ya kukamilika kwa hatua hizo, Wakala wa Forodha ataingia kwenye mfumo wa kulipia wa TPA (e-payment) na TPA itazifanyia tathimini gharama za huduma ambazo imezitoa kwa gari husika ili kupata tozo za bandari kwa gari la mteja. Taarifa hizi zitamfikia Wakala wa Forodha kwa njia ya electroniki kwa kumpatia namba ya kumbukumbu kwa ajili ya kulipia (payment reference number - PRN).

Baada ya Wakala kupata PRN atatakiwa kwenda kwenda benki mojawapo kati ya TIB, NMB, CRDB na Standard Charted au kwa njia ya simu ili kulipia malipo ya tozo za TPA kwa niaba ya mteja.

Wakala akishakamilisha malipo ya TPA ataingia katika mfumo wa mizigo wa TPA (cargo system) kwa ajili ya kutengeneza kibali (announcement) cha kuonyesha gari analotaka kulitoa kutoka bandarini kwa kujaza taarifa zote zinazohusu gari hilo.

Wakala akishakamilisha hatua hiyo atafika bandarini kwenye ofisi ya TPA geti namba 2 na atapewa kibali cha kuruhusiwa kuchukua gari la mteja wake (gate in ticket). Kibali hicho kitakuwa na maelezo yote aliyoyajaza wakala kwenye announcement. Gate in ticket itaambatishwa na nyaraka nyingine ambazo ni Bill of Lading, Delivery order na Release order.

Wakala kuchukua gari bandarini
Baada ya kukamilisha hatua tajwa hapo juu, hatua inayofuata ni wakala kwenda katika ofisi za Kitengo cha Magari kwenye yadi husika (delivery yard) ambako kuna gari la mteja wake, kisha ataonyesha nyaraka kwa ajili ya kutoa gari husika. Karani na askari wa TPA (Incharge) watakagua nyaraka zote ili kujiridhisha kama hatua zote zimefuatwa.

Endapo itabainika kuna hatua ambazo hazijakamilika, wakala atatakiwa kukamilisha hatua hiyo au kufanya marekebisho mahali alipokosea. Baada ya kujiridhisha kwamba hatua zote zimefuatwa, karani ataingia katika mfumo wa TPA wa mizigo ili kupiga truck tally kwa gari husika na kutoa gate pass A itakayomruhusu wakala kuchukua gari la mteja wake.

Karani atasaini sehemu husika katika gate pass A na wakala wa mteja atasaini kuonyesha amepokea gari hilo baada ya kujiridhisha kwa kulinganisha taarifa iliyopo kwenye nyaraka na namba ya chasis ya gari la mteja.

Pia, karani wa TPA atatakiwa kujaza fomu ya makabidhiano ya gari (Vehicle Hand Over Form) ambayo itaelezea hali halisi ya gari wakati wa kulikabidhi kwa Wakala wa Forodha kwa niaba ya mteja.

Fomu hiyo itasainiwa na msimamizi wa yadi, askari wa yadi na wakala wa mteja, kisha wakala atachukua gari la mteja wake. Karani baada ya kutoa gate pass A ataingia kwenye mfumo wa TANCIS na kufanya carry out kwa gari husika ikiwa ni hatua ya kuonyesha kuwa gari hilo halipo tena bandarini na limeshatoka nje ya bandari.

Wakala atachukua gari la mteja wake pamoja nyaraka na kwenda nazo getini askari atazipokea nyaraka hizo na kuzikagua kisha kukagua gari husika na akishajiridhisha kwamba hakuna tatizo ataingia kwenye mfumo wa mizigo wa TPA na kuonyesha kuwa gari husika limeshatoka nje ya bandari (gate out).

Mteja anapopokea gari lake kutoka kwa wakala wake wa forodha ni lazima ahakikishe anapata nyaraka zote zilizotumika kulipia na kutolea gari lake.

Ni muhimu sana kwa mteja kupata fomu ya ukaguzi wa hali halisi ya gari lilivyopokewa bandarini Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT) na fomu ya makabidhiano ya gari kati TPA na wakala wa Forodha Vehicle Hand Over Form.

Endapo mteja hatapewa fomu hizo na Wakala wake anatakiwa kutoa taarifa TPA kwa kupiga simu au kutuma meseji za bure za TPA kutoa taarifa ili wakala husika achukuliwe hatua zinazostahiki, namba hizo ni 0800110032 au 0800110047.
Ahsante sana mkuu kwa kutupa elimu kuhusu mlolongo wote wa kutoa gari bandarini
 
Naongezea, kabla ya Meli ya magari kufika.

Mnunuzi akinunua gari Kwa kupitia ma agent hupewa taarifa za Meli gari iliyopakiwa na Estimated Time of Arrival (ETA) katika Bandari ya Dar es Salaam. Hivyo unaweza ukaanza kuitrack Meli Kwa kupitia Vessel Finder au Marine Traffic.

Shipping Agent wa Meli ya magari hupeleka taarifa TPA kuwa anataraji kuleta Meli, hivyo hutoa taarifa za Meli na mzigo utaoshuka au kupakiwa.Hapo hiyo Meli itaanza kuonekana katika website ya bandari kwenye kipengele Cha TPA Daily Shipping List na hii hutolewa Kuanzia Jumatatu mpaka Ijumaa baada ya kikao Cha ship planning kuhusu Meli za kuingia na kutoka.

Meli ikiishafika Tanzania eneo la nje la bahari (Outer Anchorage Area) Captain wa Meli hutuma email Kwa agent kutoa taarifa ya kufika, ambapo watatoa muda wa kufika (End of sea passage), Kisha kama Meli ipo tayari taarifa ya kuwa tayari kwenda kushusha bandari hutolewa (Notice of Readiness).

Hapo Kwenye Notice of Readiness(NOR) Meli inaweza isitoe muda huo huo endapo Kuna marekebisho au kuweka vitu sawa Ili wakifika bandari waanze kazi Direct.

Baada ya NOR kama agent wa Meli (Shipping Agent) alikamlisha kulipa malipo ya kuingiza Meli (Mfano; Tugging,Pilotage,Wharfage) Captain hupewa taarifa ya kuomba nafasi ya Pilot kuja kuifata Meli(Pilot Booking) Ili waingie bandari.

Pia Meli inaweza ikawa imekamilisha malipo na nafasi ya gari(Berth) hakuna hivyo Meli itashusha nanga (Anchor down) kusubiri nafasi Bandari, vivyo hivyo kama malipo hayajakamilika watashusha nanga.

Meli kuingia bandari huwa baada ya Pilot kuwa Booked muda ukifika pilot hupelekwa nje au eneo Meli ilipo na boti ndogo(Pilot Boat) hii uambatana na taarifa ya kuingia Meli ambayo hutolewa Control Tower na Mooring Gangs (wafunga meli).Kisha upanda melini Kwa kutumia ngazi maalum iliyopo pembeni ya Meli (Pilot Ladder) Kisha hupokelewa na kukaribishwa kwenda sehemu ya kuongozea Meli (Ship Bridge) ambapo hatakuwa anakuwa na Captain wa meli kuelekeza meli iingie vipi na namna Gani itafunga katika gati la Bandari.

Meli inapoingia Bandari baada ya kuvuka eneo la ferry Tug Boat husogea Kwa ajili ya kuipa Meli msaada wa kufunga kwenye gati. Baada ya Meli kusukumwa mpaka kwenye gati zoezi la kuifunga kamba (Ship Mooring) huanza ambapo Kamba ya kwanza (First line) ufungwa mbele na nyuma, Kisha kamba nyingine na kumalizika kamba ya mwisho(Last line) zoezi hili wastani huchukua Kuanzia robo saa mpaka nusu saa.

Baada ya kumaliza kufunga kamba ngazi ya kupandia melini hushuka (Gang way) Ili Pilot ashuke na Maafisa wa Afya waweze kuingia Kwa ajili ya ukaguzi.

Pilot hushuka Kisha Maafisa Afya wa Bandari (Port Health Officers) nao hupanda melini Kwa ajili ya ukaguzi. Kipindi Maafisa Afya wanapanda melini Meli hupeperusha Bendera ya njano kuonyesha kuwa Meli Bado haijakidhi Watu kuingia (No permit granted for anyone to board).Muda ambao Watu wa Afya wapo Melini mlango wa kushusha magari (Lamp) huanza kufunguliwa na mabaharia na kuweka vitu sawa Kwa zoezi za upakuzi.

Baada ya Watu wa Afya kumaliza ukaguzi wa Meli na kukagua magonjwa ya mlipuko,usafi wa Meli na vipimo vya COVID-19 hutoa taarifa kuwa Meli ipo salama Kisha Bendera ya Njano hushuka kitendo hiki Cha Meli kuwa sawa na ruhusa ya wengine kuingia Kwa ajili ya kazi huitwa Free Pratique Granted.

Maafisa Afya wakishuka ndipo Maafisa Uhamiaji, Forodha(TRA), Shipping Agent na TPA officer na madereva hurusiwa kuingia melini Kwa ajili ya taratibu za kushusha magari.

Maafisa huamiaji huomba list ya mabaharia na passport zao, Mtu wa TRA hukagua store na kuweka seal Ili kuzuia mizigo na vitu vyao vikaingia nchini bila kulipa Kodi, Mtu wa Port Security huomba documents za meli, mabaharia na utaratibu wa meli kuhusu wageni wanapoingia kuhakikisha hakuna wazamiaji wakati wa kutoka au wizi (International Ship and Port Security {ISPS} level 1) ambapo wataweka visitors log book,vitambulisho vya meli na ukaguzi Kwa aingiaye na kutoka. Mtu wa Port Operation huomba documents za kuonyesha mzigo wa kushuka Dar na kupanga utaratibu wa namna Gani madereva watafanya kazi.

Baada ya Hapo magari huanza kutolewa Kwa kushuka Kwa njia ya kuendeshwa, muda wa Kuanza Operation ni pale gari la kwanza linaposhuka na muda wa kumaliza ni pale gari la mwisho linapomalizika.

Utaratibu unaofata kama ndugu mtoa mada alioanza mpaka kumfikia mteja wa gari husika.
Nilikuwa naomba msaada wa kujua gharama zote za bandarini za kulipia na kiasi chake kwa gari zinazoingizwa hapa nchini mfano ukiagiza gari la cc 2000 gharama zake za bandarini ni kiasi gani? Maana wao hawajaweka wazi Kama TRA walivyofanya.
 
Nilikua naomba msaada wa kujua gharama zote za bandarini za kulipia na kiasi chake kwa gari zinazoingizwa hapa nchini mfano ukiagiza gari la cc 2000 gharama zake za bandarini ni kiasi gani? Maana wao hawajaweka wazi Kama TRA walivyofanya
Baadhi ya gharama za kulipia Bandarini Kuna Wharfage,Cargo handling,Stowage wao nadhani Bei Wana estimate kulingana na ukubwa wa kitu kwa kutumia mita za mraba (CBM-Cubic Metres).

Wadau watakuja kukupa ufafanuzi zaidi.
 
Nilikua naomba msaada wa kujua gharama zote za bandarini za kulipia na kiasi chake kwa gari zinazoingizwa hapa nchini mfano ukiagiza gari la cc 2000 gharama zake za bandarini ni kiasi gani? Maana wao hawajaweka wazi Kama TRA walivyofanya

TBS kiasi gani – TZS 350,000
TPA – USD 7.00 per CBM
Corridor Levy – USD 0.30 per CBM
shipping line fee – up to USD 45.00
CFA – TZS 200,000
Registration inalipiwa pamoja na ushuru, plate ni 28,000 mpaka 35,000
 
Wakuuu mie nipo N'gambo, Niliagiza gari ya Bibi yangu kutokea huku, Nimetrack meli imeshafika Tz Dar es salaam Tangu 1 April (last friday)

Ila Agent ananiambia bado haijashusha kwa anayefahamu Timeframe ya Kushusha-until Gari itoke bandarini, Malipo ya TRA na TBS yameshafanywa last two weeks,

imebaki Port charges za huko na AGent fee tu. SIna shaka na Agent maana amekuwa akitusaidia faster tu, sasa i know watu wanabadilika

Kwa anayeelewa anisaidie
 
Nyuzi zako za mwanzo ni zipi mkuu. Ambatanisha link chini ya kila uzi unaouanzisha.

Ahsante.
 
TBS kiasi gani – TZS 350,000
TPA – USD 7.00 per CBM
Corridor Levy – USD 0.30 per CBM
shipping line fee – up to USD 45.00
CFA – TZS 200,000
Registration inalipiwa pamoja na ushuru, plate ni 28,000 mpaka 35,000
Asante
 
Wakuuu mie nipo N'gambo, Niliagiza gari ya Bibi yangu kutokea huku, Nimetrack meli imeshafika Tz Dar es salaam Tangu 1 April (last friday)
Ila Agent ananiambia bado haijashusha kwa anayefahamu Timeframe ya Kushusha-until Gari itoke bandarini, Malipo ya TRA na TBS yameshafanywa last two weeks,
imebaki Port charges za huko na AGent fee tu. SIna shaka na Agent maana amekuwa akitusaidia faster tu, sasa i know watu wanabadilika

Kwa anayeelewa anisaidie
Bado hamjaipata?
 
Katika mfululizo wa makala za bandari, leo tunakuletea utaratibu unaotumika kuhudumia shehena ya magari hatua kwa hatua katika bandari za TPA, kuanzia meli inapoingia bandarini, gari linavyoteremshwa kutoka melini na linavyopokewa bandarini, gari linavyotoka bandarini hadi mteja kukabidhiwa gari lake.

Ukaguzi baada ya meli kuwasili bandarini
Hatua ya kwanza inayofanyika baada ya meli kuwasili bandarini ni ukaguzi unaofanywa na Idara za Serikali za Afya na Uhamiaji kwa meli na mabaharia. Hii inafanyika ili kujiridhisha juu ya afya za mabaharia na hakuna mzigo hatarishi ndani ya meli.

Idara ya uhamiaji ina jukumu la kuhakikisha kuwa taratibu zote za uhamiaji zimezingatiwa na mabaharia. Wakati taratibu za ukaguzi zinafanyika bendera ya Shirika la kimataifa la Bahari duniani (International Maritime

Organization – IMO) inakuwa inapepea kwenye meli na hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia au kutoka ndani ya meli. Ukaguzi ukishamalizika bendera ya IMO inateremshwa ili kupandishwa bendera ya Tanzania.

Baada ya ukaguzi kinachofuata ni Wakala wa Meli (Shipping Agent) husika kuingia na genge maalumu ambalo jukumu lake ni kufungua mikanda ya kufungia magari ili yasigongane ndani ya meli na kusababisha uharibifu.

Kukamilika kwa hatua hii kunatoa nafasi kwa madereva wa TPA kuingia ndani ya meli ili kuanza kazi ya kuteremsha magari.

Ukaguzi wa magari baada ya kuteremshwa kutoka melini
Baada ya magari kushushwa kutoka melini, hupelekwa kwenye gati (quay side) Karani wa TPA huyapokea kwa ajili ya ukaguzi. Ukaguzi huo una lengo la kutaka kujua hali ya magari kabla ya kuteremshwa. Ukaguzi ukionyesha kuwa gari lipo salama, halikupata hitilafu yoyote, gari hilo litabandikwa stika ya rangi ya kijani yenye alama ya vema (√).

Endapo gari litabainika kuwa na hitilafu ya kuharibika au kukosekana kwa vifaa kama redio, vifaa vya kupandishia vioo (power windows), vioo (side mirrors) nakadhalika gari hilo litabandakwa stika nyekundu yenye alama ya kosa (X).

Baada ya ukaguzi kukamilika, karani atajaza fomu maalumu inayotambulika kama Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT). Fomu hii huonyesha hali halisi ya gari lilivyoshuka kutoka melini na kupokewa bandarini.

Fomu ya VDITT ikishajazwa kwa gari husika nakala moja huwekwa ndani ya gari kwa uthibitisho, kisha gari hilo hupelekwa eneo/ yadi kwa ajili ya kuhifadhiwa ili kusubiri mteja husika aje kuchukua gari lake.

Baada ya gari hilo kufikishwa yadi, askari wa TPA aliyepo yadi atalikagua tena kwa kutumia fomu ya VDITT na kupewa nafasi (position) kwa kuandikwa juu ya bonnet au ubavuni sehemu ya milango.

Gari likisha hakikiwa kuwa limeshuka kutoka melini, karani ataingia kwenye mfumo wa mizigo wa TPA (Cargo system) na kulipigia tally kulihesabu kuwa limeshuka, kisha ataingia katika mfumo wa TANCIS ili kuonyesha (carry in) kuwa gari husika limeshuka kutoka melini na lipo bandarini.

Majukumu ya Wakala wa Forodha katika kutoa gari bandarini
Wakala wa Forodha aliyechaguliwa na mteja kwa ajili ya kumsaidia kutoa gari lake bandarini atatakiwa kufuata taratibu za kiforodha kwa niaba ya mteja ikiwa ni pamoja na kupata vibali kutoka mamlaka husika hususan Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na kulipia TRA na kwa Wakala wa Meli ili kupata nyaraka za kutolea gari (release order na delivery order).

Baada ya kukamilika kwa hatua hizo, Wakala wa Forodha ataingia kwenye mfumo wa kulipia wa TPA (e-payment) na TPA itazifanyia tathimini gharama za huduma ambazo imezitoa kwa gari husika ili kupata tozo za bandari kwa gari la mteja. Taarifa hizi zitamfikia Wakala wa Forodha kwa njia ya electroniki kwa kumpatia namba ya kumbukumbu kwa ajili ya kulipia (payment reference number - PRN).

Baada ya Wakala kupata PRN atatakiwa kwenda kwenda benki mojawapo kati ya TIB, NMB, CRDB na Standard Charted au kwa njia ya simu ili kulipia malipo ya tozo za TPA kwa niaba ya mteja.

Wakala akishakamilisha malipo ya TPA ataingia katika mfumo wa mizigo wa TPA (cargo system) kwa ajili ya kutengeneza kibali (announcement) cha kuonyesha gari analotaka kulitoa kutoka bandarini kwa kujaza taarifa zote zinazohusu gari hilo.

Wakala akishakamilisha hatua hiyo atafika bandarini kwenye ofisi ya TPA geti namba 2 na atapewa kibali cha kuruhusiwa kuchukua gari la mteja wake (gate in ticket). Kibali hicho kitakuwa na maelezo yote aliyoyajaza wakala kwenye announcement. Gate in ticket itaambatishwa na nyaraka nyingine ambazo ni Bill of Lading, Delivery order na Release order.

Wakala kuchukua gari bandarini
Baada ya kukamilisha hatua tajwa hapo juu, hatua inayofuata ni wakala kwenda katika ofisi za Kitengo cha Magari kwenye yadi husika (delivery yard) ambako kuna gari la mteja wake, kisha ataonyesha nyaraka kwa ajili ya kutoa gari husika. Karani na askari wa TPA (Incharge) watakagua nyaraka zote ili kujiridhisha kama hatua zote zimefuatwa.

Endapo itabainika kuna hatua ambazo hazijakamilika, wakala atatakiwa kukamilisha hatua hiyo au kufanya marekebisho mahali alipokosea. Baada ya kujiridhisha kwamba hatua zote zimefuatwa, karani ataingia katika mfumo wa TPA wa mizigo ili kupiga truck tally kwa gari husika na kutoa gate pass A itakayomruhusu wakala kuchukua gari la mteja wake.

Karani atasaini sehemu husika katika gate pass A na wakala wa mteja atasaini kuonyesha amepokea gari hilo baada ya kujiridhisha kwa kulinganisha taarifa iliyopo kwenye nyaraka na namba ya chasis ya gari la mteja.

Pia, karani wa TPA atatakiwa kujaza fomu ya makabidhiano ya gari (Vehicle Hand Over Form) ambayo itaelezea hali halisi ya gari wakati wa kulikabidhi kwa Wakala wa Forodha kwa niaba ya mteja.

Fomu hiyo itasainiwa na msimamizi wa yadi, askari wa yadi na wakala wa mteja, kisha wakala atachukua gari la mteja wake. Karani baada ya kutoa gate pass A ataingia kwenye mfumo wa TANCIS na kufanya carry out kwa gari husika ikiwa ni hatua ya kuonyesha kuwa gari hilo halipo tena bandarini na limeshatoka nje ya bandari.

Wakala atachukua gari la mteja wake pamoja nyaraka na kwenda nazo getini askari atazipokea nyaraka hizo na kuzikagua kisha kukagua gari husika na akishajiridhisha kwamba hakuna tatizo ataingia kwenye mfumo wa mizigo wa TPA na kuonyesha kuwa gari husika limeshatoka nje ya bandari (gate out).

Mteja anapopokea gari lake kutoka kwa wakala wake wa forodha ni lazima ahakikishe anapata nyaraka zote zilizotumika kulipia na kutolea gari lake.

Ni muhimu sana kwa mteja kupata fomu ya ukaguzi wa hali halisi ya gari lilivyopokewa bandarini Vehicle Discharge Inspection Transfer Tally (VDITT) na fomu ya makabidhiano ya gari kati TPA na wakala wa Forodha Vehicle Hand Over Form.

Endapo mteja hatapewa fomu hizo na Wakala wake anatakiwa kutoa taarifa TPA kwa kupiga simu au kutuma meseji za bure za TPA kutoa taarifa ili wakala husika achukuliwe hatua zinazostahiki, namba hizo ni 0800110032 au 0800110047.
Asante sana mkuu hakika umetoa elimu nzuri mnoo
 
Asante kwa madini unatuongezea sisi mawakala wa forodha tulipo border ujuzi …sisi ujuzi wetu ni ku clear mzigo ukifika border na kumpelekea mteja aliepo nchi za nje …mambo ya bandarini wengi hatujui …UMETISHA
 
24 Reactions
Reply
Back
Top Bottom