DOKEZO Responded Mfumo wa TBS unasumbua kutoa gari Bandarini, gharama zinakuwa kubwa na zinaangukia kwa mteja

DOKEZO Responded Mfumo wa TBS unasumbua kutoa gari Bandarini, gharama zinakuwa kubwa na zinaangukia kwa mteja

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
676
Reaction score
1,634
Mimi ni mmoja wa wateja niliyeagiza gari kutoka nje ya nchi. Gari langu limefika bandarini tangu wiki iliyopita, lakini hadi sasa halijatolewa kutokana na changamoto kubwa ya mifumo, hususan mfumo wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Kwa kweli hali hii inakatisha tamaa sana. Tangu mfumo huo uanze kutumika hivi karibuni, umekuwa kikwazo kikubwa kwa sisi wateja. Sipo peke yangu—tupo wengi tumekwama bandarini tukikosa huduma kwa wakati.

Ukifika bandarini, hasa katika ofisi za TBS, utakutana na msongamano mkubwa wa watu waliokwama kama mimi. Hakuna mwendelezo mzuri wa huduma, na majibu yanayotolewa hayana uwazi wala uhakika.

Kinachouma zaidi ni kwamba muda wa bure wa kuhifadhi gari bandarini unaendelea kuisha, na gharama za ziada (storage) zinaendelea kuongezeka kila siku—mzigo wote huo unaangukia kwa mteja.

Tunaomba sana mamlaka husika, hususan TBS, wachukue hatua za haraka kuboresha mfumo huu na kuhakikisha unafanya kazi kwa ufanisi. Hali ya sasa siyo rafiki kwa wafanyabiashara wala wananchi wa kawaida.

Swali letu ni moja tu—hali hii itaendelea hadi lini?”

Ufafanuzi ~ TBS: Mawakala wa Forodha na Waagizaji wa Bidhaa nchini wafuate Taratibu wakati wa kuomba kibali kupitia TANeSW
 
Mifumo mipya ya single window yote matatizo matupu TMDA madudu yaleyale.

Serikali itoe tamko, kama delays zitatokana na mifumo yao basi gharama za storage zisimhusu mteja.

SWISSPORT wanaweka storage tu hawaelewi kwamba mifumo haifanyi kazi. TMDA mfumo mpya umeshawashinda hata IT hawajui matatizo mengine wanasolve vipi.

Haya mambo ya kubadili system kila mwaka tena bila extensive training ya angalau miezi 6 kabla ya kupush mfumo kwenda kufanya kazi kunadhulumu watu wengi
 
TBS wanataka Tsh 350,000 kwa kila gari na mfumo wao usipolipia hautoweza kupata release ya TRA pana vitu vingi sana kwenye magari harafu Anatolia mtu mwingine anasema gari kuingia mjini inatakiwa lilipiwe Tozo tena hata sijui hizo kodi na Tozo zote ni za kupita wapi...
 
We acha tu mkuu tunateseka sana maagent kazi zinakuwa zina presha kinoma atleast wewe umeelewa kinachoendelea lakini wenzako wanawasha moto ukimueleza scenario anaona kama unafanya mchezo just imagine hapo tbs agent anaweza kukaa zaidi ya siku kadhaa na hajafanikiwa ukizingatia Malipo anayopata na ugumu wa kazi uliosababishwa na mifumo mibovu haviendani
 
Japan si wana ma-agent wa TBS kule kule?
 
We acha tu mkuu tunateseka sana maagent kazi zinakuwa zina presha kinoma atleast wewe umeelewa kinachoendelea lakini wenzako wanawasha moto ukimueleza scenario anaona kama unafanya mchezo just imagine hapo tbs agent anaweza kukaa zaidi ya siku kadhaa na hajafanikiwa ukizingatia Malipo anayopata na ugumu wa kazi uliosababishwa na mifumo mibovu haviendani
Aisee hiyo mifumo Watz tunavamia Tu, au ni madili ya watu
 
Wanafanya maksudi,ili wawaingize watu kwenye
Storage tu wawatoe hela
Hamna lolote

Ova
 
Why wanaingiza mifumo bila kufanya testing kama imekaa sawa? Hii changamoto ipo maeneo mengi sana, ukipata mzigo wako kwa wakati nenda kasali na kushukuru 😃
 
We acha tu mkuu tunateseka sana maagent kazi zinakuwa zina presha kinoma atleast wewe umeelewa kinachoendelea lakini wenzako wanawasha moto ukimueleza scenario anaona kama unafanya mchezo just imagine hapo tbs agent anaweza kukaa zaidi ya siku kadhaa na hajafanikiwa ukizingatia Malipo anayopata na ugumu wa kazi uliosababishwa na mifumo mibovu haviendani
Na kinacho udhi majibu yao mepesi sana unashindwa hata kuelewa sasa tumshtakie nani maana kila mmoja hana jibu wala suluhisho ya tatizo lililopo mbele yetu. Hii mifumo iko kama ilishakwisha muda wake ndio tumekuja tupiwa sisi huku tuteseke tu wenyewe wamesha isimika wamejiendea huko.
 
Why wanaingiza mifumo bila kufanya testing kama imekaa sawa? Hii changamoto ipo maeneo mengi sana, ukipata mzigo wako kwa wakati nenda kasali na kushukuru 😃
Kabisa mkuu ni zaidi ya mateso na gharama zisizo za lazima.
 
Ukiagiza gari mpaka liwe mkononi mwako kuna mateso bila chuki...
 
Back
Top Bottom