Ziara za Paulo Makonda Aibu kwa Jeshi la Polisi na Wasimamizi wa Haki na Sheria

katawa

JF-Expert Member
Jan 29, 2010
750
1,667
Uwe unampenda ama humpendi,uwe unafuatilia ama haufuatilii ziara zake.

Kitu kimoja utagundua kuwa Watanzania wengi sana wanakandamizwa na wasimamizi wa haki na sheria.

Mamia kama si maelfu ya wananchi wanakandamizwa na kuonewa toka ngazi ya mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

Wananchi wanakandamizwa na wachache wanafuatilia hadi ngazi za juu lakini bado hawapati haki zao.

Mtendaji mkuu wa Serikali ambaye ni waziri mkuu anatoa maagizo lakini watu wa chini yake wanapuuzia. Rejea ziara ya Makonda kule Shinyanga.

Je, kuna anguko la Utawala wa Sheria?
 
YEYE MWENYEWE MAKONDA ANATIA AIBU KWA DHULMA ALIZOZIFANYA WAKATI WA DIKTETA MAGUFULI

Sent from my SM-A145R using JamiiForums mobile app
 
Uwe unampenda ama humpendi,uwe unafuatilia ama haufuatilii ziara zake.

Kitu kimoja utagundua kuwa Watanzania wengi sana wanakandamizwa na wasimamizi wa haki na sheria.

Mamia kama si maelfu ya wananchi wanakandamizwa na kuonewa toka ngazi ya mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

Wananchi wanakandamizwa na wachache wanafuatilia hadi ngazi za juu lakini bado hawapati haki zao.

Mtendaji mkuu wa Serikali ambaye ni waziri mkuu anatoa maagizo lakini watu wa chini yake wanapuuzia. Rejea ziara ya Makonda kule Shinyanga.

Je, kuna anguko la Utawala wa Sheria?

Cha kuchekesha hao ccm wako madarakani kwa kuwatumia hao hao police. Na ccm hawawezi kukubali hilo jeshi la police au vyombo vya kisheria kufanya kazi zake ipasavyo maana wao ndio watakuwa wahanga namba Moja. Kama jeshi la polisi linafunga barabara Zaidi ya masaa ili mwenezi wa ccm apite, huyo Makonda anaweza kukubali jeshi la police lifanye tofauti na huo upendeleo?
 
Uwe unampenda ama humpendi,uwe unafuatilia ama haufuatilii ziara zake.

Kitu kimoja utagundua kuwa Watanzania wengi sana wanakandamizwa na wasimamizi wa haki na sheria.

Mamia kama si maelfu ya wananchi wanakandamizwa na kuonewa toka ngazi ya mtaa, kata, wilaya, mkoa hadi Taifa.

Wananchi wanakandamizwa na wachache wanafuatilia hadi ngazi za juu lakini bado hawapati haki zao.

Mtendaji mkuu wa Serikali ambaye ni waziri mkuu anatoa maagizo lakini watu wa chini yake wanapuuzia. Rejea ziara ya Makonda kule Shinyanga.

Je, kuna anguko la Utawala wa Sheria?
Lini Makonda mwenyewe alifuata sheria?
 
Makonda wakati wa bunge feki la katiba alikuwa anayakaza mashangingi na mijimama ya hilo bunge lahaula limoja likaukwaa mjengo.
Mkuu
Nadhani tunapaswa kujenga hoja na siyo kufabya vioja.

Simkubaki Makonda lakini neheshimu utu wake kama binadamu
 
Ukiniuliza mimi nitakuambia ni sawa hizo ziara ila wahusika hawafanyi maandalizi stahiki.
1. Nilitegemea kabla ya ziara chama na mbunge vingewaalika wote wenye kero zao wafike ofisi ya diwani au mbunge au ya chama wilaya na malalamiko yake na vielelezo yake.
2. Chama au mbunge kingechambua malalamiko na kuyatafutia majibu kutoka taasisi zinazolalamikiwa.
3. Yale malalamiko yatakayopata ufumbuzi, wahusika wangepewa mrejesho wao. Hoja zinafungwa.
4. Yale yaliyokosa majibu wahusika waambiwe na ndo yangekuwa hoja mbele ya mgeni rasmi. Lakini yasomwe na katibu au mwenyekiti wa wilaya husika ila walalamikaji wawepo kufafanua kwa maelezo na vielelezo.

Utaratibu wa sasa unaonyesha kukosa ushirikiano ndani ya chama na baina ya chama na serikali mahali husika. Hili halina afya.

Hawa watendaji mnaowadhalilisha ndio wanaowalindia kura zenu na wanajua mlivyoshinda. SAWA.

Hawa madiwani na wabunge mkishawachafua mbele ya wapiga kura wao, wanapataje ujasiri wa kurudi kuomba kura?

Nia ni njema kwani SIFA inapaswa iende kwenye CHAMA na sio kwa MTU MMOJA. Sasa ni tofauti kidogo.
 
Back
Top Bottom