Maadhimisho ya Diplomasia ya Ping-Pong ni ukumbusho kwa Marekani kuchukua hatua kuondoa mvutano katika uhusiano na China

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111325141351.jpg


Ubalozi wa China nchini Marekani umefanya hafla ya kumbukumbu ya miaka 52 ya Diplomasia ya Ping-Pong, ambapo Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng, alitoa wito kwa pande hizo mbili kutumia busara na msukumo wa tukio hilo la miongo kadhaa.

Wataalamu wa China wanaamini kuwa, tukio hilo sio tu linalenga kuamsha kumbukumbu za Marekani kuhusu historia hii ya urafiki, bali pia ni kuikumbusha Marekani kuonesha busara ya kisiasa na kuchukua hatua kusaidia uhusiano wa pande mbili hizo kuondokana na mvutano uliopo sasa.

Mpaka sasa Marekani bado haijachukua hatua halisi za kuboresha uhusiano wa pande mbili katu yake na China ambao uko katika hali tete tangu marais wa nchi hizo mbili waliokutana na kufanya mazungumzo mwezi uliopita huko San Francisco. Wakati huohuo, Marekani bado inafuata njia ya zamani ya kuingilia suala la Taiwan, na hivyo kuleta kutokuelewana kati ya China na nchi jirani zake.

Wataalamu wa China wana wasiwasi kuwa, mara dirisha la fursa iliyopatikana kwa viongozi wa nchi hizo mbili kukutana litakapofungwa, uhusiano kati ya Marekani na China utaharibika tena wakati Marekani itakapoingia kwenye kipindi cha uchaguzi wa rais mwaka ujao.

Akizungumza katika hafla ya kumbukumbu ya miaka 52 ya Diplomasia ya Ping-Pong, Balozi Xie alisema inapaswa kuondoa mvutano kati ya nchi hizo mbili, na kuongeza kuwa, kwa kuwa nchi hizo mbili zimefanikiwa kusuluhisha mvutano uliodumu kwa miaka 22 miaka 52 iliyopita, zinapaswa kuwa na imani leo ya kuondokana na mawazo ya Vita Baridi, kushinda kile kinachoitwa ‘usahihi wa kisiasa,’ na kuvuka mtego wa mvutano wa nchi kubwa.

Balozi Xie amezitaka pande hizo mbili kufufua upya mabadilishano kati ya watu wa pande hizo, na kuanza safari mpya katika uhusiano kati ya China na Marekani. Ameongeza kuwa, mkutano wa San Fransisco sio mstari wa mwisho, bali ni mwanzo mpya wa uhusiano wa pande mbili kati ya China na Marekani.

Timu ya mpira wa meza ya Chuo Kikuu cha Peking ilialikwa kushiriki katika maadhimisho ya Diplomasia ya Ping-Pong katika miji ya Washington na San Francisco. Timu hiyo pia imejiandaa kushiriki katika Mashindano ya Wazi ya Mpira wa Meza ya USATT mwaka huu yatakayofanyika katika Kituo cha Ontario huko California. Mchezaji maarufu wa mpira wa meza wa nchini China, Ding Ning, ambaye pia ni mhadhiri katika Idara ya Utafiti na Elimu ya Kimwili katika Chuo Kikuu cha Peking anasema, Diplomasia ya Ping-Pong iliyoanza mwaka 1971 ilifungua historia ya mabadilishano ya kirafiki kati ya China na Marekani kupitia mpira mdogo wa ping-pong, na kuimarisha maelewano kati ya watu wa pande hizo mbili. Anasema anaamini kuwa, michezo ni sehemu nzuri ya kuanzia, kwa kuwa watu wako tayari kuwasiliana na kuelewana kupitia michezo wanayopenda.

Ding Ning anasema, mchango wa Diplomasia ya Ping-Pong katika historia bado unawashawishi vijana wa leo, na anatumai kuwa, kizazi cha sasa kitaendelea kurithi udhati na uzuri wa kumbukumbu za Diplomasia ya Ping-Pong na kuandika ukurasa mpya wa mabadilishano ya kirafiki kati ya China na Marekani.

Lakini tofauti na ishara ya kirafiki ya China, Balozi wa Marekani nchini China Nicholas Burns alizungumza katika maadhimisho hayo na kusema, hana matarajio mazuri kuhusu hatma ya uhusiano kati ya China na Marekani, na kwamba inapaswa kutulia na kuangalia jinsi mambo yatakavyokuwa. Pia Balozi Burns ameonya kuwa, hana matumaini kuwa uhusiano kati ya pande hizo mbili utaboreka katika siku za karibuni.

Wataalamu wameonya kuwa, wakati uchaguzi unapokaribia nchini Marekani, dirisha la fursa lililofunguliwa kufuatia mkutano kati ya marais wa China na Marekani linazidi kuwa dogo, na hii inatokana na siasa chafu za ndani za Marekani ambazo zimekuwa za chuki dhidi ya China, kwa kuwa wagombea urais wa Marekani wamekuwa na desturi ya kucheza ‘karata ya China’ ili kuvutia wapiga kura.
 
Back
Top Bottom