Mkutano unaotarajiwa kufanyika kati ya marais wa China na Marekani unasubiriwa kwa hamu duniani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,035
Rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kufanya ziara nchini Marekani kati ya Novemba 14-17 ambalo atakuwa na mkutano na mwenzake wa Marekani na pia kuhudhuria mkutano wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi la Asia-Pasific (APEC). Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Rais Xi kufanya ziara nchini Marekani tangu April 2017 wakati wa utawala wa Rais Donald Trump, na itakuwa ni mara ya pili kwa Rais Xi na Rais Biden kukutana tangu walipokutana kwenye mkutano wa kundi la G20 uliofanyika mwaka jana huko Bali, Indonesia.

Mkutano utakaofanyika kati ya Rais Xi Jinping na Rais Joe Biden unafuatiliwa kote duniani, kwani China na Marekani ni nchi zenye nguvu kubwa zaidi kiuchumi duniani, na kitakachojadiliwa sio tu kinahusu nchi hizo mbili, bali pia kitaathiri dunia nzima. Kama mkutano huo ukienda vizuri na kuwa na matokeo mazuri, ina maana ni jambo la manufaa kwa dunia.

Ikumbukwe kuwa Marekani imekuwa ikifanya vitendo mbalimbali za kuyumbisha ushirikiano kati yake na China. Tangu Rais Donald Trump aanze kuilenga China kibiashara kwa kuongeza kodi yenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 370 kwenye bidhaa zinazoagizwa toka China, kodi ambayo hadi leo ipo, hadi ziara iliyofanywa kisiwani Taiwan na aliyekuwa spika wa bunge la Marekani Bibi Nancy Pelosi kinyume na utaratibu wa sheria za kimataifa, na China pia imechukua hatua zinazofaa kujibu vitendo hivyo vibaya vya Marekani.

Hata hivyo, katika miezi ya hivi karibuni kumekuwa na mwelekeo mzuri kwenye uhusiano kati ya China na Marekani. Marekani imeonyesha kutafakari na kurekebisha mwenendo wake katika utekelezaji wa sera yake ya kidiplomasia, baada ya kukubaliana na ukweli kwamba licha ya tofauti zilizopo, bila kushirikiana na China kwenye mambo yanayohusu maslahi ya dunia nzima, Marekani haiwezi kufanikiwa. Na kama ikiendelea kuvutana na China, si kama tu Marekani yenyewe hainufaiki, bali hata nchi nyingine duniani zinaathirika.
 
Biden ajiandae vizuri asije kuanguka kwenye ngazi, pia apewe dawa za kumweka sawa kiakili maana huwa anasahau anachohutubia na kusahau mlango wa kutokea akimaliza hotuba.

Ni raisi pekee wa Marekani ambaye anajibiwa maswali karibu ypte ya press na wasaidizi wake.
 
Back
Top Bottom