Umuhimu wa ushirikiano kati ya China na Marekani wazidi kuonekana kwenye mkutano kati ya Rais Xi nchini Marekani

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111378067918.jpg

Rais Xi Jinping wa China na mwenyeji wake Joe Biden wamekutana na kufanya mazungumzo ya ana kwa ana yaliyokuwa yanasubiriwa kwa muda mrefu na wadau wengi wa mambo ya uchumi na siasa. Kwenye mkutano huo Rais Xi amemwambia Rais Biden kuwa dunia ni kubwa na ina nafasi ya kutosha kwa nchi hizo mbili kuwepo kwa pamoja, na kwamba ushirikiano kati ya pande hizo mbili unatakiwa kutazamwa kwa muktadha mpana unaozingatia mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani.

Rais Xi amesema kutokana na mabadiliko yanayoendelea kutokea sasa duniani, China na Marekani zinatakiwa kuimarisha mshikamano na ushirikiano na kuungana mkono ili kukabiliana na changamoto za kimataifa na kukuza usalama na ustawi wa kimataifa, na sio kuwa na mtizamo wa kunufaisha upande mmoja na kuweka hatari ya kuzusha migogoro.

Rais Xi amekumbusha kuwa China haina mpango wa kuipita au kuiondoa Marekani kwenye nafasi yake duniani, lakini pia amesema Marekani haipaswi kupanga njama ya kukandamiza na kuidhibiti China. Amesema njia ya maendeleo ya China haitakuwa sawa na njia ya zamani ya ukoloni na uporaji, au njia mbaya ya kutafuta umwamba kutokana na kukua kwake, na wala haipeleki nje itikadi yake, au kujihusisha na makabiliano ya kiitikadi na nchi yoyote.

Pengine jambo moja ambalo amesema waziwazi kuikosoa Marekani, ni kuhusu hatua kadhaa za kuilenga China zilizochukuliwa na serikali ya Marekani. Rais Xi Jinping amesema kudhibiti mauzo ya nje ya China, uwekezaji na vikwazo vya upande mmoja unaathiri maslahi ya China. Pia amesema majaribio ya Marekani kukwamisha maendeleo ya kiteknolojia ya China ni hatua ya kudhibiti maendeleo ya hali ya juu ya China na kuwanyima watu wa China haki yao ya maendeleo. Amemkumbusha rais Biden kuwa ukuaji wa China unaotokana na juhudi za ndani hautaweza kukwamishwa na nguvu yoyote ya nje.

Wadau mbalimbali wa mambo ya uchumi na siasa wameanza kuchanganua yaliyoongewa na viongozi hao kwenye mkutano wa San Francisco, lakini katika hatua ya mwanzo wachambuzi wametaja kuwa kimsingi pande mbili zinaona kuwa ni muhimu kushirikiana kwenye mambo ya maslahi ya dunia.
 
Xi kaitwa Washington. Hakuwa na namna nyingine zaidi ya kutii. Now akawa-brief Putin na Ayatollah kilichojiri including mwelekeo wa uchumi na siasa za dunia.
 
Habari mbaya sana hii kwa wale wafuasi wa mudy na tegemeze wa china.
 
Back
Top Bottom