Dada/Mama
WomanOfSubstance afadhali umeiweka habari hii kwa mtindo huu, Kuna mwanachama mmoja (mwanamama) aliiweka hapa wiki iliyopita, Lakini ilikaa kwa mtindo ambao haukuwa mzuri kuichangia, nami ndio nilipata muda wa kupita huko kuangalia kilichoandikwa/bandikwa. Kwa ukweli niliogopa na kushindwa kuamini kwanini tumefika hapo. Nimeona baadhi ya picha/ majina ya watu ninaowafahamu na ambao najua wazi kuwa hawana tabia hizo za ujinga.
Kwa vyovyote itakavyokuwa,hata kama mtu anafanya umalaya na ujinga, lakini si ustaarabu kumbandika kwenye blog bila idhini yake,kwa mtazamo wangu,nafikiri hatufundishani kwa Mtindo huu, Jamii ya wastaarabu ina namna ya kutatua matatizo yake kwa njia za ustaarabu zaidi kuliko hizi tunazoziona sasa.
****Kumbukeni hawa tunaowaumbua humu ni ndugu na Dada zetu.... Kwa taarifa tu wanaoendesha blog hizi wanatafutwa na mwenye blog mojawapo amekwishafahamika,na wanaohusika wanafanya naye mawasiliano,ni wazi kuwa baada ya muda mfupi Blog hizo hazitokuwa hewani.
Lakini kwa namna yoyote itakavyokuwa Watanzania wenzangu tujaribu kujenga Jamii yenye Heshima na Ustaarabu...Hata kama una matatizo na mtu tafuta njia muafaka ya kutatua matatizo yenu bila kuyaweka wazi kwa watu yasiyowahusu..Naamini wengine waliotukanwa kule ni wanachama hapa....Jaribuni kuangalia upya mienendo yenu,kwa sababu maneno yaliyosemwa huko si mazuri,na kwa mtazamo wangu hamuwezi kuyakanusha yote.
Tujirekebishe na tujaribu kuheshimiana na kuheshimu privacy za watu.Hakuna mtu aliye mkamilifu,kila mtu ana mapungufu yake. Tukubali ushauri na kuomba misamaha pale tunapowakwaza wenzetu.Hiyo tu ndiyo itakayotufanya tuishi kwa amani na furaha. Nimesikitishwa mno na Blogs hizo, nami pia kama mwana-adam inabidi nijifunze kumjua bin-adam yupi ni ni rafiki wa kweli na yupi ni hasidi....
Hapa Forum kama Familia moja, Tujiunge kwa pamoja kukemea Tabia hizi mbovu...Naomba kutoa hoja.