WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,459
- 949
Kwanza kabisa naomba kutoa pongezi kwa wanaJF wote kwa michango yao ya kila aina katika kuibua maswala yanayoigusa jamii ya kitanzania kwa ujumla.Jukwaa hili kwa kiasi kikubwa limekuwa na mshiko ( impact) kuanzia mtu binafsi kwa maana ya kubadili fikra, mitizamo na hata tabia kwa baadhi.
Kijamii, jukwaa limekuwa ni kioo cha kupima muonekanao wa watanzania kwao wenyewe na hata kwa wenzao wasio watanzania.
Baada ya kusema haya machache kama utangulizi, nimeona nije hapa jukwaani na mada yenye kulenga kujitizama kama jamii inayoishi kwenye ulimwengu wenye kiu ya maisha yenye maana na manufaa.Mtashangaa kwamba ninazunguka badala ya kumwaga hoja jamvini izungumzwe na kukatiwa shauri.Mtanisamehe sana kwa hili maana inahitaji busara kuiweka bayana ili ieleweke na isilete maana mbaya na kupelekea kutupiliwa mbali kama kitu kisicho na maana.
Suala ninaloomba mliangalie kwa busara ili kulipatia ufumbuzi ni hili la wanawake kutupiana maneno, shutuma, kejeli na matusi manene maana kusema mazito ni understatement. Blogs zimefunguliwa za kila aina siku hizi zenye kulenga kuchafuana kusiko na tija wala manufaa kwamtu yeyote yule.
Chukulia mifano ya blogs kama theutamu, wakereketwa n.k haya yamekuwa ni majukwaa ya wanawake kutwezana, sisemi kuwa wanaume hawayatembelei na kutoa maoni, la hasha! Wanawake ndo wamezidi kupakazana na hata kuwadhalilisha wanaume ambao ni wapenzi wao au wamewahi kuhusiana kimapenzi.Wanawake hawa wamediriki hata kuwachambua hao wanaume wapenzi wao kwa kuwasasambua vilivyo ikiwa ni pamoja na kuwa describe sehemu zao za siri kwa namna ya kuwatweza. Ni aibu sana kuona wanawake wasomi, warembo na wenye bahati ya pekee kuliko wenzao kutumia fursa hii ya teknolojia kujidhalilisha kwa kutoa matusi bila haya wala soni.
Ukichambua kwa undani zaidi utaona kisa ch akufanya vitendo hivi vya aibu ni wivu, chuki, ujinga kama siyo upumbavu ndio vinawasumbua! Je kweli watanzania tutafika?Kama hawa ndiyo wasomi walioenda kutafuta elimu ughaibuni wanakuwa na mwelekeo kama huu, wakirudi wataweza kuwa na michango ya maana kwa jamii mwanamke ambaye matusi yamemkaa kuliko hata jina lake atakuwa mama au mke wa namna gain? Ataweza kutoa malezi bora? Na je ataweza kuwa kioo /role model wa kuigwa ili alete sifa na manufaa kwa jamii? Mwanamke wa aina hii ni aibu kwa taifa jamani.
Na nyie wakina baba, nawaomba muwasusie wanawake kama hawa, msibabaishwe na urembo wao.Wanawatieni aibu tupu na kuwaweka kwenye mashaka makubwa. Ni aibu kaka/ baba/ uliye na maadili mema kuhusiana na wanawake kama hawa. Watengeni kuanzia leo ili wajirekebishe.Na hili linawezekana maana hao wanawake wanajulikana.Jifikirie wewe mwanaume unayeheshimika ni kwa jinsi gani unajiweka kwenye nafasi ya kudhalilika unapoanikwa na hawa wanawake waziiiiiiii... ni watu wangapi wanasoma blogs hizi? Fikiria ni aibu gani unayompa dadako, mamako, mkeo, mchumba ( ndiyo wake na wachumba zenu wanasoma na wanahuzunika sana!) bintiyo!
Poleni wale wote mliokwisha twezwa na hawa wajinga wasiokuwa na maadili!
Naomba kutoa hoja.