BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,769
- 288,332
Bora imekufa maana ilikuwa inaharibu reputation za watu mbali mbali (Watanzania) wanaoishi Tanzania na nchi za nje. Mtu akikuchukia tu basi anatafuta picha yako na kuitundika huko na unaanza kutukanwa matusi ya nguoni na watu mbali. Siku za karibuni kulikuwa na mabadiliko maana Watanzania wengi walikuwa hawakubaliani na tabia hiyo ya kuweka picha za watu na kuanza kuwatukana matusi ya nguoni na waume/wake zao na wakati mwingine hata wazazi wao. Naona Watanzania wengi waliokuwa na wasi wasi kuhusu kupigwa picha katika sherehe mbali mbali au kumbi za starehe sasa watapumua bila wasi wasi.