Ze Comedy aka Orijino Comedy: Mwendelezo

kadaMpinzani,Kakindo,Mwakasege,JokofuKiwete,InterestedObserver,



Mimi nadhani hawa ZeComedy wamefungua uwanja kwa Comedians wengine kuwajadili na kuwachambua wanasiasa. Mimi nadhani hiyo inaongeza ushiriki wa jamii ktk siasa. Hilo ni jambo zuri kwangu.
Safi sana kwa kuwa na mtazamo huo, katika siasa na utawala endelevu, nafasi ya wananchi wa kawaida katika kuamua mambo yao ni kubwa na ndio msingi wa uendelevu.
 
Naona Kada Mpinzani, Jokofu Kiwete na wachache wengine, mnakataa kuona hoja ya msingi. Hiyo hoja imesisitizwa tena hapa, kwa umakini kabisa, na Interested Observer. Tuirudie tena kwa namna mbalimbali:

Huwezi ukasema wewe sio mwizi eti kwa sababu aliyegundua wizi wako naye kuna siku alishaiba.

Huwezi ukasema wewe sio mgonjwa eti kwa sababu anayesema wewe ni mgonjwa kuna kipindi alishaugua.

Tukiacha hayo, niongezee yafuatayo: Nielewavyo, Mtunza Hazina wa Vilema Tanzania ni mmojawapo wa Vilema wenyewe. Kwani Slaa alishawahi kuwa kilema? Kama alipewa fedha za vilema na akazila, basi tuambiwe kiasi na wakati. Hata hivyo, hilo haliwasafishi wale walio kwenye listi ya ufisadi. Kiongozi aliyeiba bilioni 500 za Watanzania au aliyesaini mikataba ya kuuza nchi kwa kuhongwa ni fisadi, na anabaki kuwa fisadi hata kama Slaa alikula shilingi elfu 10 za vilema.

At the risk of digressing, naomba nitumie fursa hii kusahihisha baadhi ya makosa yaliyofanywa na wenzetu kwenye posti zao hapa:

Lunyungu kasema Slaa katoka kundini. Kundi lipi? Nielewavyo, Slaa bado ni Mkatoliki, tena Mkatoliki mzuri. Lunyungu ameongezea kwamba Slaa kaacha Daraja la Upadri. Haiwezekani, kwani Daraja la Upadri haliachiki. Lunyungu kasema vile vile kuna watu wameshakuwa wadhambi na bado wakawa Askofu. Si hoja, kwani hata Petro aliwahi kumkana Yesu na bado akaambiwa "Chunga kondoo wangu" (akawa Papa). Mwishowe, nimtaarifu Lunyungu kwamba kama Padre Karugendo aligombana na Askofu wake, basi hilo ni kosa kubwa mno. Pardi anaweka nadhiri ya kumtii Askofu wake.
 
haya basi naona hapa pia tumepishana lugha katika kuwasilisha ujumbe uliodhamiliwa, basi acha nikubali mnavyoona nyie katika maandishi tu hapa lakini moyoni i have a different view !

Najua na naheshimu aliyosema dr. Slaa kwamba he was doing it for the country, but is he clean too himself or does he have those dark secrets ? pengine naye anaficha tu makucha yake, mengi yamesemwa juu yake lakini naona watu wanafunga masikio utadhani hawana la kusema, lakini kama ingekuwa JK hapo kala pesa za vilema, sijui kavunja ndoa za watu, mara kaanza kujenga nyumba alivyokuwa padre/sheikh nakwambia hizi zingezagaa hadi kwenye radio za vijijini, JF hapa ndio ingekuwa kama daily news, asubuhi mchana jioni lakini kwa kuwa kafanya huyu jamaa basi watu wameamua kulala fofofo !
Kuhusu Slaa kuwa mweka hazina sina uhakika nao, lakini kwa kuwa alikuwa padre pengine alipewa jukumu la kuhakikisha msaada fulani ufikie walengwa ( vilema ) na hatimaye ukafikia mikononi mwake, n.k kama ilivyosemwa na nadhani madai hayo ze comedy wangemwaga details zaidi !

Nitakwambia kwa mara nyingine, kama slaa alikula pesa za vilema, ( watu wasiojiweza, hali zao ngumu kabisa katika kutafuta kipitisha kinywa ) unasema hiyo haiwasafishi waliomo kwenye list ya ufisadi ( Dr. Slaa akiwa ndani ) basi hapo jua napinga hadi asubuhi, WHY ? BECAUSE wizi hauna scale, uwe wizi mdogo, wizi mkubwa ! Na kama ungeniuliza mie je ningeiba kama wale walikuwepo kwenye list ya mafisadi ( Slaa akiwemo ndani ) au niibie vilema .... haki ya nani nisingeguza pesa za vilema hata chembe ! MBAYA ZAIDI KUMTETEA SLAA KAMA KWELI ALIIBA HIZO PESA ZA VILEMA MBAYA ZAIDI ALIKUWA KATIKA CRITICAL POSITION, **PADRE** NOW YOU CANT TELL ME NOTHING, SASA JE HAPA ALIVYO SASA HIVI, MWANASIASA, SI NDIO ATAIBA HADI NEPI ZA WATOTO ! kama mtapinga sawa pingeni, lakini mie naweka masikio yangu pamba, sitaki kusikia bana !

Lakini mkuu, sawa nimekusikia, mie naishia hapa, nitaamini mnavyoona nyie kwa maandishi tu hapa !
 
Being frank, jamaa walishindwa kuchekesha walipoiga sehemu ya Dr Slaa, nilikuwa sehemu flani na wananchi wa chini kabisa, wengi wala walikuwa hawaelewi jamaa walibaki wanakandamiza macho kwenye TV lakini hawakuambulia kitu.

Nadhani Motive ilikuwa politically zaidi kuliko kuchekesha, Hamana haja ya kuwazomea, watazamaji watawachoka wenyewe wasipojirekebisha. Nadhani wanatakiwa kuigiza mambo yanayochekesha, Mfano, jinsi walivyo wakilisha suala lenyewe, sidhani kama kuna mtu ata confess madhambi yake wazi wazi, kwahiyo halikuchekesha.

Njaa tu inawatatiza!
 
Wanaweza wakawa na njaa au la lakini ni dhahiri watu hawa ni wenye akili timamu na wanaojua wanachokifanya,si haki ya JF kuwapangia wao cha kuhubiri,nikubaliane tu wengine humu;kuwafanyia kampeni ni kuwapa chati isiyostahiki na pia wao wajibu wao mkubwa ni kuburudisha watu wapenzi wao kwa njia ya vichekesho huku wakifikisha ujumbe waliokusudia,they did huko nyuma kuhusu serikali n.k na sasa wamefanya against washindani wa CCM,let's respect kazi yao kwa msingi wa kutoa nafasi ya kusikia yanayosemwa na upande wa pili wa shilingi.JF si chama cha siasa hali kadhalika The Comedy si chama cha siasa.
JF ni wigo wa wenye ukomavu wa hoja na tuamini pia The Comedy ni mfano hai wa ukomavu wa Kisanii kwa Mtanzania
 
Wakumbuke yaliyowakuta wanaume family, waliamua kuwa wanaCCM wakazunguka kumpigia kampeni kikwete, umaarufu wao ukashuka sana na wakasambaratika na hakuna mtu aliyejali, ni upeo mfupi wa wasanii wetu hawajui kwamba hawatakiwi kutake sides kwenye jamii, wajue jamii imegawanyika kiitikadi na jamii inwachukulia wasanii kama watu walio "neutral" hawako CCM wala upinzani, ni TOT pekee yao ndo wanajulikana kwamba wao ni CCM na watu hawana shida nao kwani kipato chao wanakipata toka CCM, nyinyi ze commedy mkianza kujiassociate na CCM mtaanza kukosa hata matangazo halafu mtakufa njaa hapa mjini mkichukilia ni wachunga ng'ombe tu mtaipata fresh, msikubali kutumiwa, ni hayo tu.
 
Nafikiri hao ze comedy wana upeo mdogo, na kumbukeni mwenye upeo mdogo ni rahisi kutumiwa na wazito maana hajui nini maana ya ufisisadi na jinsi wananchi wanavyoishi katika mazingira duni. Sanaa ni kuelimisha na sio kuibomoa jamii. Ni hayo tu.
 
kama upadre ni ihali, basi anao uhuru wa kuuacha. kwa hiyo sio hoja ya msingi.

pili, kama kuuacha ni kosa au dhambi. tuache pengo na papa wakamshtaki na wala sio serikali sababu serikali haina dini, hivyo sio swala lenye uzito bali ni kutapatapa tu pasipo sababu. hata hivyo si serikali yenyewe inatuambia tusichanganye dini na siasa, sasa mbona yenyewe inafanya hivyo.

ila kwa taarifa zaidi kwenye nyumba zote za ibada ufisadi umeisha anza kukemewa bila kujali mtoa mada ni padre mwenzake Dr au askofu.

tatu, katika sheria zote za nchi, hakuna sehemu tunakatazwa kutomshtaki au kumlaum mtu eti sababu na wewe ulishawahi kukutwa na shtaka au umeshtakiwa. yaani umwibia mtu kitu eti sababu hawezi kukupeleka maakamani sababu aliwahi kubaka na kufungwa au aliwahi kushtakiwa na kosa lolote lile. hata peer reasoning does not concur.

sect.55 of the evidence Act inasema 'the fact that the accused is of the bad charecter is irrelevant'

sasa serikali iache kuchanganya dini na siasa, inabidi ijibu tuhuma, au kada mpinzani na Kilitime wake watusaidie.
 
Unajua Seki anaanza kulewa kwa umaarufu wa kikundi cha ze comedy. anatakiwa kujua kuwa wanachi ndio wanaompa umaarufu. pia anatakiwa ili aweze kupata umaarufu asikubali kununuliwa na upande wowote ule. anatakiwa awe makini sana na kuangalia alama za nyakati. swala linalowagusa wananchi asilifanyie mzaha mzaha.. wananchi wana hasira sana na ze comedy wanaona kuwa wamenunuliwa kuuwa nguvu za upinzani kwa sababu wanajua kuwa wananchi wengi wanaangalia ze comedy. kwa nini asionyeshe shule ambazo hazijakamilika? wakina mama wanaokenda kujifungua wakiwa wanalal 2 kwenye kitanda? Mabarabara yetu yalivyo mabovu? aachane na hoja za kina Slaa hizo ni siasa. akiendelea hivyo umaarufu utashuka sasa hivi. kwani hajua watanzania hawachelewi kuwazomea kila wapitapo?
 
hawa jamaa hata kama wanapewa mshiko na CCM,lakini pia huwa wanawakandamiza haohao CCM,juzi tu walimrudi JK kwa safari zake.Ila ninavyoona mimi ni kuwa hawa jamaa inawezekana kweli walipewa kamshiko kidoogo,maana CCM wanajua sasa hivi wakianza wao kukandamiza Slaa hakuna atayesikiliza,hivyo wakawatumia hawa jamaa.Sasa hawa nao wakiwa machizi,njaa zao zitawapeleka pabaya.Kama wataanza hivyo,then watapoteza umaarufu wao sasa hivi
 
Story na Mariam Mndeme (Ijuaa wikienda)

Mbunge wa Mbinga Magharibi (CCM) Kapten John Komba, amelipiga kundi la Ze Cimedy, kuigiza sauti yake kwenye vipindi vyao vya ucheshi ambacho hurushwa hewani kupitia Luninga ya EATV.

Komba ambaye pia ni Mkurugenzi wa kundi la Maonesho la TOT, alisema ameshawasiliana na Ze Comedy na kulitaka kuacha mara moja kuiga sauti yake, lkn ameshagaa kuona bado wanaendelea.

"hii ni sauti yangu ambayo nimepewa na Mungu ili niitumie mimi mwenyewe siyo kwa ajili ya kuigizwa na watu wengine" Kepten Komba aliliambia gazeti hili(Ijumaa) kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mbunge huyu alisema ingawa kundi hilo limekuwa likiigiza sauti za watu mbalimbali, lakini kila mtu anaweza kupokea kulingana na mtazamo wake, hivyo alidai kwamba analichukulia kama dharau juu yake.

Alimtaja msanii wa Ze comedy, Mjuni sylvery 'Mpoki' kuwa ndiye humuiiga mara kwa mara ktk maonesho ya kikundi hicho. Vitendo ambavyo humdhalilisha yeye, familia yake na wananchi anaowaongoza.

Niliwahi kumpigia simu Mpoki nikamuonya, kwanza nilikuwa simjui, nilipoambiwa hiyo tabia yake ya kuiga sauti yangu, nilitafuta namba yake mpaka nikaipata lakini nashangaa yule kijana hataki kuacha.

"Hashangai mimi mbunge mzima kuhangaika kumtafuta mpaka nilivyompatana nikamuonya. Anachofanya ni kiburi ndio maana hataki kuacha. Hivi kwanini asitumie sauti yake ya kawaida kama kweli yeye ni msanii wa kweli? alihoji mh Kapt. Komba.

Alipoelezwa kwamba Ze Comedy huwa hawamuigizi kwa mabaya bali ni kwa lengo la kufikisha ujumbe, Komba alijibu " Kufikisha ujeube siyo lazima watumie sauti yangu, watumie sauti za watu wengine, ya kwangu sitaki kwa sabatu sipendi.

"Nimemkanya hajasikia, kwa hiyo wacha aendelee, lakini kuna siku ataona moto wangu kwa sababu makaidi hafaidi mpaka siku ya idd."
 
Suala la slaa kuoa mke has nothing to do with our normal life, hiyo ni issue yake na familia yake. wewe umetembea na wake wangapi hadi leo?

Hapa issue ni ze comedy kutumiwa, waache ujinga huo wanataka kuharibu kazi yao inayowaweka mjini. Niliona siku ile nikajua kabisa they were fed.

Hata kama ni kweli haimzui kuitaja orodha ya mafisadi na hawa mafisadi ni lazima wajisafishe either kwa kwenda mahakamani au vinginevyo. Slaa atajisafisha kivyake lakini hii haiwapi nafasi mafisadi ku neutralise kisanii sensitive issue kama hii ufisadi.

Mjibu ufisadi wenu, hakuna kusubiri slaa atoe boriti kwenye jicho lake. msilete utani Eboo!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
...i hope 'muashi-miwa' is not serious jamani, heee :eek: ???!!!

...si wan'sema msanii (kama yeye) ndio kioo cha jamii?
 
hapa ndugu mheshimiwa kachemsha, mbona mh. the president anaigizwa na hajawahi kusema chochote. au sauti yake yeye mali sana??
 
Kuna hii hii clip ambayo message yake ni ya kisiasa ingawa inaletwa kwa njia ya vichekesho kutoka kundi la Ze Comedy pale Bongo. Check it out at EastAfricantube.com
 
Huyu Komba naona sasa anazeeka vibaya. Mbona kina Malecela, Makamba, Mengi, hata Mkapa wamewahi kuigwa sauti zao. Na kama ni umaarufu, wa hao waheshimiwa ni mkubwa kuliko wa kwake wa kupiga kwaya na taarabu. Sasa hako kaubunge tu ndio ajione ni mheshimiwa kushinda hata hayati mwalimu Nyerere ambaye amekuwa akiigizwa sauti yake mara nyingi na watu kama kina Steve Nyerere..?? Asituyeyushe na umaarufu wa ukubwani. Sauti inatolewa na Mungu na hakuna mmiliki wa sauti duniani. Kwa hiyo asiingilie sanaa. Kinachokera zaidi, yeye ni msanii, halafu anashindwa kuelewa sanaa..?? Yesu Kristo (kwa wakristo watanielewa) huwa anaigizwa makanisani kwa watu kufundisha jamii yale aliyokuwa akiyatenda. Hata sinema za Yesu zipo. Sasa yeye ni nani..?? Shida za kubahatisha vyeo ndio hz..!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom