Fidel80
JF-Expert Member
- May 3, 2008
- 21,947
- 4,445
Hahahaha!
Naona huji ngoja nikapumnzike nyumba ya wageni.
Hahahaha!
Kongosho nafasi ya upande wa pili hatujaisikia hapa JF tu ila sio kama mitaani hawaongei.Wengine hata kufurahia wanafurahia kuweza kupata vitu kwa kutumia miili yao.cha kujiuliza, wote tumeng'aka sasa wanaofanya ni akina nani?
Ningependa kusikia ushahidi toka kwa victim angau mmoja
tunawahukumu bila kuwapa nafasi ya kusikia upande wao
1. Kuna wanawake wanaojali sana miili yao kuiheshimu na wanautu, hawa wanatabia ya kuwa na misimamo na hawababaishwi na lolote mbele yao ili mradi anaujuzi na taaluma yake kichwani hawa hawadanganyiki.
2.Kuna wanawake wengine wanajiheshimu kwa kiwango cha uvuguvugu.hii inamaana kwenye tabia nzuri,kuheshimu miili yao na kuwa na msimamo wapo kiaia,na kwenye kutoiheshimu miili yao,kutokuwa na msimamo na kuwa na tabia mbaya napo wapo kiaina.hawa ni wa uvuguvugu.hawa huweza kurudi katika pointi namba moja endapo watapata ushauri mzuri na endapo wakipata ushauri wa hovyo wataangukia katika kundi namba tatu hapa chini.
3.Kuna wengine hao wanaitwa "i dont care",hawa hawana cha kupoteza,wao wana open their nanii na kutoa kuanzia atakaye mkutanisha na mabosi,bosi mwenyewe.yani wanasemaga niangushage a.k.a ma mama huruma walichopewa na mungu kumnyima mwanaume dhambi,na asipompa itapata kutu.
Kwa makundi hayo matatu hapo juu wenye kufall katika namba 1 ndo wanaunafuu wakutoa gift ,but group la 2 wanaweza change kutokana na mshauri atakaye mpata.
Wanawake mkazanie hapo kwenye namba 1.
Hapo ndipo salama yenu ilipo.
EMT tuko pamoja, ila swala la kulaumu wapokeaji pekee mimi nakubaliana nalo pale inapotokea anaelazimika kutoa hiyo rushwa anapokua hajitambui kutokana na umri. Zaidi ya hapo, wanaendekeza wenyewe.Kama ambavyo mwalimu halazimiki kupokea ,ndivyo ambavyo mwanafunzi nae halazimiki kutoa .Utayari wao ndio unaopaswa kulaumiwa.
Kuhusu walimu waliojiunga na ualimu ili tu wapate ajira nakubaliana na wewe kwa 105%. Nakumbuka mara ya mwisho kwenda kutembelea shule yangu ya sekondari nilikuta walimu wengi kweli vijana, baadhi nilisikia wana mahusiano na wasichana wa pale shuleni, tena tofauti tofauti. Na mmoja nilihakikisha mwenyewe, sadly alikua anatembea na binti ambae ni ndugu yangu na alikua na miaka 14 tu at the time. Pamoja na kwamba inawezekana binti alijirahisi mwenyewe ila ni dhahiri kwamba mwalimu ndie mwenye makosa zaidi maana yeye ndie aliyetakiwa kuwa mlinzi badala ya mtumiaji.Inasikitisha sana!!
Niiiiice.
Alafu namba tatu sio kina "i don't care". . . .ni wajasirimiili. Wao mawazoni hawaoni kwanini wakose kitu wakati uwezo wa kukipata upo ndani yao.
Mimi hapa nitazungumzia hili la mwisho tu. Ni kitu cha ajabu lakini ndio ukweli kuwa wazazi matata na wenye tabia mbaya ndio wanaokuwa wakali kwa kutaka watoto wao wasiwe na tabia njema.3.Mtu kama huyu akija kuwa mzazi atakuwaje?Ataweza kumfundisha mtoto wake kuwa tofauti na alivyo yeye?
Baada ya majadiliano na rafiki yangu kuhusiana na rushwa (zawadi) ya ngono mashuleni, vyuoni na maofisini nimejikuta najiuliza maswali mengi ambayo ningependa tusaidiane kuyajibu kwasababu kwa namna moja ama nyingine matokeo yake yanaathiri hata mahusiano, ndoa na malezi.
Kwanza ni wazi kabisa kwamba mtu akishaanza ni ngumu kuacha kutokana na ukweli kwamba anakua amejipa ulema wa aina fulani.Kwamba kama alifaulishwa sekondari kuna nafasi kubwa atahitaji kufaulishwa chuoni, na akifaulishwa chuoni kuna nafasi kubwa atahitaji kubebwa pale atakapokua kwenye mchakato wa kupata kazi na baadae kwenye kujiendeleza (kupandishwa cheo, kupata nafasi za masomo, kushirikishwa kwenye semina zinazolipa n.k).
Sasa je. . .
1. Mtu anapoanza kuhonga mwili wake ili afanyiwe kazi yake (kusoma, kuwa na CV kali, good work ethics, experience n.k) kwanini anafanya hivyo?Ni kutojiamini (mwenyewe siwezi) au ni kuzungukwa na watu wasio na imani nae (wazazi, ndugu na jamaa wasioisha kumwambia hatofika popote)???
2.Je kuna hatari gani mtu kutegemea mwili wake badala ya akili na uwezo unaohitajika kupata kazi,kufaulu n.k?
3.Mtu kama huyu akija kuwa mzazi atakuwaje?Ataweza kumfundisha mtoto wake kuwa tofauti na alivyo yeye?
4.Malezi yanachangia vipi kuwafanya ndugu zetu wawe hivyo?
Najua kwa kiasi kikubwa hata system yetu (kupeana kazi kwa kujuana bila kujali sana uwezo wa kazi ) inachangia kwa kiasi kikubwa, maana isingekua inaruhusu ingekua ngumu kutoa na kupokea rushwa ya aina hii ila napenda kuangalia kile kinachowasukuma wahusika zaidi.
LIZZY,
HONGERA KWA MADA NZURI SANA, KWANI HILI NI TATIZO KUBWA SANA KTK JAMII YETU. MIMI KITU NILICHOGUNDUA NI KWAMBA PAMOJA NA KWAMBA KUNA WANAUME WENYE TABIA CHAFU LKN KUNA WAKINA DADA AMBAO WAKIWA MASHULENI/VYUONI BADALA YA KUTUMIA MUDA WAO KUSOMA SERIOUSLY ILI WAWEZE KUFANIKIWA LKN WAO WANAKUWA NA STAREHE NYINGI SANA NA MWISHO WAKE WANASHINDWA KUFANIKIWA KTK UPANDE WA CAREER ZAO. NA INAPOFIKIA ANAKARIBIA MITIHANI NDIYO ANAKUMBUKA VINGI AMBAVYO HAKUVIFANYA NA HIVYO WAO WENYEWE WKT MWINGINE KUANDAA MAZINGIRA YA KUTOA NGONO ILI WAFANIKIWE. EBU CHUKULIA, MWANAFUNZI ANAKUPIGIA SIMU NA KUKUULIZA KAMA UPO OFISINI ANA SHIDA NAWE (MWALIMU), NDIPO ANAKUJA OFISINI HUKU AMEVAA KIMTEGO NA HUKU ANAHITAJI FAVOR. NA CHA AJABU, BINTI ANAFIKIA HATUA YA KUKUAMBIA YAANI MIMI NIKO TAYARI KWA LOLOTE ILI UNISAIDIE TU. WKT MWINGINE, HUYO MWL NAYE UZALENDO UNAMSHINDA. NA KUMBUKA KWAMBA - WENGI WA MABINTI WANAOPENDA STAREHE NI WAREMBO, NA HIVYO WAMEFIKIA HATUA YA KUFANYA MIILI YAO KAMA MITAJI YA KUFANIKIWA.
Lizzy, hali ni mbaya sana hata Ma-ofisini, hasa kwa masekretari ambao wengi wao wana kipato kidogo. Na hata kwenye hizi semina watu wanafanya sana ngono. Kwa kweli ni hali ya hatari sana.
Mimi naamini kwamba tatizo kuu ni Kutojiamini na Tamaa za baadhi ya madada zetu.
@ EMT. . .
Kuhusu kutokuaminika, come on now.Kwenye dunia hii ya teknolojia hata nikitaka tu kuhakikisha kwamba kijana wa jirani alinitongoza naweza, sembuse ushahidi wa kwamba mkuu wa shule/kazi anataka tubadilishane favours?Labda kama mtu hajaamua tu ila sio kwamba haiwezekani.
EMT mbona ni rahisi hata kupata rafiki wa kuunga mkono hoja.Sema tatizo kubwa zaidi ni kutokua na uwajibishwaji. . . unaweza hata ukawa na ushahidi wa video nao ukayeyushwa tu.Lizzy inategemea dunia ya teknolojia unayoizungumzia ni ipi. Kwenye shule zetu za msingi hata zile za sekondari kuna teknologia gani? Kama inakuwa ngumu ku-prove kuwa mwanamke amekuwa raped, unafikiri itakuwa rahisi ku-prove kuwa ametongozwa? Pia kumbuka hapa tuongelea wasichana wadogo kama wa primary na sekondari ambao hawana hata ujuzi wa kukusanya ushahidi.
Mimi nafikiri suala hapa wala sio teknologia. Imbalance relationship iliyoko kati ya mwalimu na mwanafunzi ndio inayommweka mwanafunzi katika mazingira magumu ya ku-prove. Kutongozwa na kijana wa jirani ni tofauti na kutongozwa na mwalimu wako. Kwa huyo kijana wa jirani ni rahisi kuamua lakini kwa mwalimu wako inaweza kuwa ngumu kwa wengine as it could go either way.
@ EMT. . .
@MAMMAMIA hivi ni rahisi kweli kumwambia mtu mwingine asiibe na kumaanisha wakati wewe mwenyewe umetoka kuiba muda sio mrefu?Ni ngumu kufundisha na kukazania maadili ambayo wewe mwenyewe huna.
EMT mbona ni rahisi hata kupata rafiki wa kuunga mkono hoja.Sema tatizo kubwa zaidi ni kutokua na uwajibishwaji. . . unaweza hata ukawa na ushahidi wa video nao ukayeyushwa tu.
Boss hii ya pili wengine huwa wanatamba kabisa kuwa amepata kazi baada ya kutembea na fulani na wao wanaona fahari kabisa kuwatambia wanawake wenzao..mmezungumza mengi lakini kuna vitu viwili hatujataja
1.tamaduni za kiafrika..
fikiria mahari kwa mfano ni nini????
kwa nini waafrika mwanamke anatazamwa kama kifaa cha kununuliwa na kutumika?????
je tamaduni hizo hazichangii 'mawazo' ya 'kupata mwili wa mwanamke' kwa mbinu na hila kuwa ni jambo la kijanja na la maana???
2.ni utamaduni wa 'kurushana roho' wa wanawake hasa kitanzania.....
mtu atatembea na boss wake ili tu wenzie 'awarushe roho' wanawake wenzie ofisini hata kama
hakuna malipo ya kupandishwa cheo au nini.....
mmezungumza mengi lakini kuna vitu viwili hatujataja
1.tamaduni za kiafrika..
fikiria mahari kwa mfano ni nini???
kwa nini waafrika mwanamke anatazamwa kama kifaa cha kununuliwa na kutumika?????
je tamaduni hizo hazichangii 'mawazo' ya 'kupata mwili wa mwanamke' kwa mbinu na hila kuwa ni jambo la kijanja na la maana???
2.ni utamaduni wa 'kurushana roho' wa wanawake hasa kitanzania.....
mtu atatembea na boss wake ili tu wenzie 'awarushe roho' wanawake wenzie ofisini hata kama
hakuna malipo ya kupandishwa cheo au nini.....
nataka jamhuri imchukulie hatua stahiki huyu..unataka ukaokoe jahazi?