Zawadi ya ngono

kuna uzi uliwai kuwekwa hapa jf.na ulikuwa unaelezea ukubwa la tatizo ili la gift ya....
Na ilikuwa inasema 75% kama sikosei ya wanawake walioajiriwa serikalini na sector binafsi walivuliwa sketi.
Nilikua nakazia tu uzi.

Kaazi kweli kweli!!
Sasa shule wanaenda kufanya nini?
 
Huyu ni virus mbaya sana. Kuna watu wanaamini kuwa they can always get what they want by using their bodies. This is too bad. Ndio maana hata mashulkeni, cyuoni, degree za chupi ziko nyingi tu. Na hiyo kama unavyosema, haiishi hapo, hata makazini.

Hii ni tabia mbaya sana kwa kuwa inacreate unjustice kwenye jamii. mtu wa namna hii hata kama hawezi ku deliver, basi atapandishwa vyeo weee, na mwishoni atakwua mwanasiasa, maan ahuko ndio kumekufuru...
hv mtu kama hawezi kudeliver vizuri utampromote vp? maana performance appraisal za siku hzi sio zile za kisirisiri kumbuka. labda wanautumia system ya zamani
 
Hii ni kati ya rushwa ngumu sana japo taarifa na wakati mwingine mazingira huonesha kuwa baadhi ya wanawake wachache na wasiojiamini na kile walichonacho kichwani, huamua kutumia mwili ili kupata favor hizo ulizotaja. Kuna huu wa uchu wa ngono (lust) miongoni mwa waajiri ( waajiri wengi ni wanaume-hasa kwa hapa kwetu), hawa wakati mwingine wanapomuona mwombaji mwanamke huongozwa na uchu badala ya vigezo.

Kutojiamini na kudhani kuwa 'uchi' ni mpango kamili ambao unaweza kuutumia katika majadiliano ya kazi na vitu vingine ni udhaifu unaofanya hata wanawake wengi wanaopata nafasi kwa kutumia akili, busara na hekima zao basi waonekane kama wametumia 'silaha uchi' kupata wanayoshika
Na huo "uchu" unaendekezwa na watoaji ofcourse.
Mwanaume anataka, mwanamke nae anakua tayari kutoa hivyo mzunguko unaendelea tu.
 
mpaka mtu akupe rushwa ya ngono ujue kazoea, ni ngumu sana kumvulia nguo mtu humjui hakujui hakuna mapenzi, na wanaanza kidogo kidogo toka mashuleni mpka wakifika kwenye ajira huona ni kawaida, kuna wanaotoa rushwa/zawadi ya ngono hata kwenye kupandishwa vyeo mtu huyu huwezi kusema kuwa ana shida, unakuta ana kazi nzuri anataka cheo fulani anatembea na boss apandishwe cheo au anatembea na boss ili awe anapata favours fulani fulani ofisini, hapana ni hulka na tabia mbaya ya muhusika

athari? zipo nyingi dada, kwanza ni kutokujiamini kwa mhusika, mfano unaweza mpa kazi(imagine ndo bosi wako) aliyokupa mapaka ipitishwe huchukua muda mrefu maana hajui kama inafaa au la, pili kama ndo anatembea na mkurugenzi na amuweke mkononi tegemea majungu, akiona unamzidi uwezo atahisi unampita, atakufitinisha na bosi mpaka uondoke mwenyewe, vilevile inaathiri utendaji wa sehemu husika maana iwe kitengo/ idara au biashara maana ufanisi utashuka na morality ya kufanya kazi kwa wengine inaweza pungua

mtu huyu akija kuwa mzazi kuna mawili anaweza lea mwanae kwa mazingira sahihi au ndo aina ile ya wazazi ambao huwaambia binti zao "wewe si mwanamke leta hela ya kula...."
 
Futa hiyo kauli ya "wanawake wengi bana"

Nwy ni kweli madhara yake yanaenda mbali sana, imagine huyo anaejua kupata vitu kwa kutoa mwili wake tu. . . unadhani hata akija kuwa mke wa mtu ataacha?Ndio mwanzo wa kuleteana magonjwa majumbani.
lol! most of them waliosaidiwa mm ni shuhuda after tht wakiguswa tu kidogo ,haoooooo kilaiini!
 
lol! most of them waliosaidiwa mm ni shuhuda after tht wakiguswa tu kidogo ,haoooooo kilaiini!

Sasa hao si wanalipa madeni.
Sawa na dukani tu. . . unaweza ukalipa na kuchukua bidhaa hapo hapo, unaweza ukaacha pesa ukafuata bidhaa baadae au ukachukua bidhaa malipo ukaleta baadae. Ndio maana mimi simaind sana favours, mtu anaweza akakunyang'anya kazi hivi hivi ukimkatalia kwasababu yeye ndie aliyesababisha ukapata.
 
Hahahaha. . .

Smiley unasikia.Unapokubali kula vya hao wakaka uwe tayari kuliwa siku na wao wakiwa tayari.
kwani nimekula nikiwa na dhiki gani? hapa tunazungumzia wadada ambao wanaliwa wakiwa na nia ya kufaulu .kupata kazi yaani wanataka kufanikiwa kwa kutumia miili yao.mimi ni tofauti hzi ni zawadi
 
Sasa hao si wanalipa madeni.
Sawa na dukani tu. . . unaweza ukalipa na kuchukua bidhaa hapo hapo, unaweza ukaacha pesa ukafuata bidhaa baadae au ukachukua bidhaa malipo ukaleta baadae. Ndio maana mimi simaind sana favours, mtu anaweza akakunyang'anya kazi hivi hivi ukimkatalia kwasababu yeye ndie aliyesababisha ukapata.
lizzy hapo utakuta siyo kazi tu au shule ...unaweza ukawa upo na nafasi fulani labda dr ukatibu mtu au TRA ukamsaidia mtu kupata lesseni na vitu km hivyo....lkn matokeo yake baada ya hapo mtu hata hakukatalii.
 
kwani nimekula nikiwa na dhiki gani? hapa tunazungumzia wadada ambao wanaliwa wakiwa na nia ya kufaulu .kupata kazi yaani wanataka kufanikiwa kwa kutumia miili yao.mimi ni tofauti hzi ni zawadi
Tofauti wapi?Deni ni deni tu aisee...liwe la pesa au kitu. Siku ukitakiwa kulipa itabidi ulipe vile unavyoweza.
 
lizzy hapo utakuta siyo kazi tu au shule ...unaweza ukawa upo na nafasi fulani labda dr ukatibu mtu au TRA ukamsaidia mtu kupata lesseni na vitu km hivyo....lkn matokeo yake baada ya hapo mtu hata hakukatalii.
Yeahhh yapo mengi kweli yanayopatikana kwa rushwa, hivi iko siku watu wataacha kweli?
 
Haiingii akilini kabisa eti mijanaume kibao ikupe mizawadi halafu iende pasi na fadhila!

Yeah,mwenyewe anaweza akadhani hawataki chochote ila kuna mazingira wanayojiandalia.Hata mimi tu siwezi kumpa mtu zawadi hovyo. . . . achilia mbali mwanaume mzima na tamaa zake.
 
Afu wewe unayepinga vitu mwangani.
Gizani ni mdhaifu sana.
Afu kama huu uzi unaku touch hivi.
Au historia inakuhukumu?
mimi kila mwaka nachukua zawadi ya mfanyakazi bora niko vizuri am professional ujue kuna mahali hapahongeki besides sijasoma elimu zenu uchwara za bongo. niko na confidence na kazi yangu ipo kwenye damu yangu siitaji kuhonga k nipate kazi cause nauzika kila mahali dunia nzima usipime
 
mimi kila mwaka nachukua zawadi ya mfanyakazi bora niko vizuri am professional ujue kuna mahali hapahongeki besides sijasoma elimu zenu uchwara za bongo. niko na confidence na kazi yangu ipo kwenye damu yangu siitaji kuhonga k nipate kazi cause nauzika kila mahali dunia nzima usipime

nimekufuatilia toka mwanzo! naona umeanza kupanic!:laser::llama:
 
hapana mkuu naona huyu mdau badala ya kuchangia mada anadeal na mimi. mimi sio kilaza atii

unajua hii kitu wengi wanaanzia shule kabisa! mtu hawezi kuweka juhudi kwenye masomo mwisho wasiku anaanza kutengeneza mazingira kwawalimu! akitoka hapo akienda mtaani kusaka kazi nakwenye anaendeleza! wanawake baadhi huwa hawajiamini! naasilimia kubwa niwale vilaza! mtu kama unajuhudi kwenye masomo hata walimu hawatapata loop hole yakukuchezea! watakupenda nakukuheshimu!
 
yote hayo n ni matokeo ya roho mbaya za wanaume kupenda kutumia udhaifu wa wanawake kujinufaisha kimwili. tuchukulie swala la ajira,suppose lizzy jinsi soko la ajira lilivogumu leo hii boss wa tbl hrm tena aseme anataka k katika wadada mia wangapi watakataa? maisha na wanaume ndo vinaharibu wadada.ila mimi namshukuru mungu toka la kwanza hadi chuo nilitumia akili yangu ata kazi yangu niliipata kiuhalali kabisa
ingawa watu hawaachi kuchonga ila ndo ukweli,
Kwa ulivyoongea hapa Smile, itakuwa ngumu sana kukuamini kama wewe hukupitia hapo... Haya bana...hata hivyo mradi mkono unaenda kinywani!!
 
Back
Top Bottom