1. Nimerudi lizzy, katika hili swala watoa zawadi ni wanawake ila lawama ziende pande zote mbili pamoja na jamii husika.
2. Case 1: Wakati nipo secondary kuna mdada alikuwa anatakwa na mwalimu kimapenzi. Yule dada alikuwa anakula fimbo kila siku bila sababu za maana na sometimes anatolewa nje wakati wa pindi. Mashtaka yakafika kwa mwalimu wa darasa ila hayakufanyiwa kazi, yakafika kwa mwalimu mkuu, mwalimu mkuu akamwambia avumilie maana anamaliza shule mwaka huo na hiyo shule haikuwa na mwalimu mwingine wa hilo somo kwa hiyo hawawezi kumfukuza. Mwisho wa siku sijui ilikuwaje ila majirani tuliona mwalimu na denti wanacheka pamoja, wanakula pamoja.
3. Case 2: kuna mdada flani wa chuo nae alizembea kufanya mtihani, kumfata professor prof akasema akitaka amsaidie huyo dada nae ajue namna ya kumsaidia. Mdada akaondoka pale, baada ya siku tatu akarudi kwa prof na bahasha yenye hela (anadai aliweka tsh 300,000). Kumkabidhi prof, prof akamrudishia ile bahasha akamwambia hakujua kama ana hela kiasi kile, achukue ile hela akatafute lodge/hotel na akishapata amjulishe. Mwisho wa siku sijui nini kiliendelea.
4. Case3: hii imemtoke rafiki yangu kabisaaa. Alikuwa anatafuta kazi, boss wa kampuni binafsi akamwambia aende bagamoyo siku ya ijumaa apelekee cv then atarudi kwao jumapili. Kampuni ipo dar, rafiki yangu na huyo bosi wote wanaishi dar ila cv ipelekwe bagamoyo. Hili likamshinda.
5. Nimejaribu kuelezea case moja moja katika kila level tupime uzito ingawa nina mifano mingi ya hivyo.
6. Sababu za zawadi ya rushwa:
7. 1.Uzembe. reference ni case 2. Kama mdada asingezembea mtihani ina maana asingekumbana na mauza uza ya prof. wanawake nao hujitakia na ndio maana yanawafika haya.
8. 2. kutokujiamini. Baadhi ya wadada hawajiamini kama wanaweza simama bila kushikwa mkono.
9. 3.kupenda mtelemko kama wengine walivyosema.
10. 4. mazingira kwa ujumla. Mazingira yanachangia kwa kiasi kikubwa na walimu wengi pamoja na maboss maofisini wamekosa maadili ya kazi. Refer case1.
11. Jibu la swali lako la 3: wapo wanaotoa rushwa huku hawapendi na wanajutia wanachofanya ila kwa namna moja au nyingine wanahisi hawawezi kufanikiwa bila kufanya hivo, watu wa hivyo kuna uwezekano wakawa walezi wazuri tu as hawatopenda kuona watoto wao wanapitia waliyoyafanya. Watu waliozoea mteremko sidhani kama watakuwa wazazi bora labda mazingira yawabadilishe tena baada ya kuwa na watoto.