Zawadi Pekee kwa Rais Samia ni Wanawake Kuingia Nafasi za Maamuzi Wenyeviti Serikali za Mitaa katika Mitaa 564 Dar es Salaam

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
942
WhatsApp Image 2024-03-08 at 09.12.45.jpeg

Ahimiza Wanawake Dar es salaam wenye sifa na uthubutu kujitokeza kwa wingi kuingia katika nafasi ya uwenyekiti Serikali za mitaa 2024.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake (UWT) Mkoa wa Dar es salaam Ndugu. Mwajabu Mbwambo, ameshiriki katika mkutano wa waandishi wa habari uliondaliwa na katibu mkuu Uwt Taifa Ndugu Joketi Mwegelo. Ukiwa na lengo la kuwahabarisha wanawake katika kuelekea siku ya wanawake duniani kuendelea kumuunga mkono Rais Dr Samia Suluhu Hassan 07/03/2024 Ofisi Ndogo ya Uwt Taifa Lumumba Dar es salaam.

Katika hotuba yake, Cde. Mwajabu ametanguliza shukrani kwa mwenyezi mungu na pongezi kwa mahudhurio mazuri ya kina mama kushiriki katika mkutano huo wa waandishi wa habari.

WhatsApp Image 2024-03-08 at 09.12.21(2).jpeg

Cde. Mwajabu ametoa wito kwa Wanawake wote kuhakikisha wanaunga juhudi za Rais Dr Samia kama kauli mbiu ya Siku ya wanawake WEKEZA KWA MWANAWAKE KUHARAKISHA MAENDELEO YA TAIFA NA USTAWI WA JAMII DR samia amewekeza kwa upatikanaji wa mikopo nafuu, kutoa elimu na mafunzo za wajasiriamali kupiti kila halmashauri nchi nzima, fursa za masoko na mambo mengine mengi muhimu.

WhatsApp Image 2024-03-08 at 09.12.21.jpeg

"Zawadi pekee tunayowe kumpa Raisi wetu Ni kuhakikisha tunaingia katika nafasi za kufanya maamuzi kuwa wenye viti wa serikali za mitaa katika uchaguzi utakao kuja hapo baada mwaka huu 2024. Mitaa 564 angalau mitaa 282 Ndani ta Dar es salaam waingie wanawake vijana na umri tofauti wenye sifa kugombea nafasi hizo kama dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama yetu mpendwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya 50/50"

WhatsApp Image 2024-03-08 at 09.12.21(1).jpeg

Ndugu. Mwajabu Mbwambo
Mweyekiti wa UWT Mkoa wa Dar es salaam.

📍Uwt Dar es salaam-Lumumba
🗓️ 7 Machi, 2024

#Kuelekea kilele cha siku ya mwanamke Dunian
#Dar es salaam
# UwtImara Jeshi la Mama Kazi iendelee
 
Back
Top Bottom