Zanzibar ya Rais Mwinyi na tuhuma za ufisadi unaoanzia juu kabisa

Steven Joel Ntamusano

JF-Expert Member
Jun 17, 2023
2,948
1,988
Asubuhi ya leo nikikatiza maeneo ya mbuyuni huku Mbezi Beach wakati naelekea mjini tulipofika maeneo ya Kwa Mwinyi, pale ilipo nyumba yake ya miaka mingi rafiki yangu akanionyesha kiwanja kikubwa chenye heka kadhaa.

Akaniambia ni kwa sababu ya mvua tu lakini kuna michakato ya ujenzi wa Mall kubwa imezuiwa na hii hali ya eneo zima kujaa maji. Nilipomuuliza mmiliki wa eneo hilo nyeti ni nani akaniambia ni Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar.

Nikakumbuka kuna video moja inatembea huko instagram inayomuonyesha mzee mmoja wa kizanzibari akiueleza uongozi wa Rais Mwinyi kwamba Nyerere alisema kiongozi wa juu kabisa ni lazima achague moja kati ya mali na utumishi wa watu anaowaongoza.

Video kama zile mara nyingi zinatolewa hadharani baada ya anayeiandaa kuwa ameshajihakikishia kuhusu hilo analolisema mbele ya watu. Mali na utumishi wa watu siku zote ni vigumu sana kwenda pamoja.

Hiyo Mall japo sijaiona ramani yake naweza kuhisi ukubwa wake utakuwa vipi kwa kutazama tu eneo lote ambalo litatumika kuijenga, namna lilivyoanzia huku barabarani likaenda mpaka kule karibu na barabara ya mzunguko inayotokea karibu na Maringo ikazunguka kule usawa wa Beach ya Kawe.

Ni eneo kubwa ambalo mpaka uwezo wa ujenzi umeweza kupatikana maana yake gharama ya ujenzi sio ndogo. Ndio hapa hizi kelele kwamba Mwinyi ni rais mwenye harufu nzuri ya utafutaji wa mali, zinaanza kuwa na mashiko, kama ni kweli hilo eneo linamilikiwa na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar.

Inawezekana zikawa ni tuhuma tu, zinazotokana na hulka yetu ya kitanzania. Hata Mama Sitti ambaye ni mzazi wa Rais Mwinyi aliwahi kuzushiwa eti analimiki lile jengo linalotizamana na mahakama ya Kisutu pale kwenye kona ya kuelekea posta mpya, ni tuhuma zilizokuwa zikisikika miaka ile mumewe alipokuwa Rais wa Tanzania.

Hizi ni tuhuma tu lakini la maana sana ni kwa serikali anayoiongoza kuweza kutafuta njia ya kuzijibu. Kwani wenye kutuhumu hufanya hivyo wakiongozwa na roho za chuki kwa Mheshimiwa, Njaa zikituzidi tunaanzisha habari za kumnyooshea kidole kiongozi fulani ilimradi tu kujifariji sisi wenyewe.
 
Asubuhi ya leo nikikatiza maeneo ya mbuyuni huku Mbezi Beach wakati naelekea mjini tulipofika maeneo ya Kwa Mwinyi, pale ilipo nyumba yake ya miaka mingi rafiki yangu akanionyesha kiwanja kikubwa chenye heka kadhaa.

Akaniambia ni kwa sababu ya mvua tu lakini kuna michakato ya ujenzi wa Mall kubwa imezuiwa na hii hali ya eneo zima kujaa maji. Nilipomuuliza mmiliki wa eneo hilo nyeti ni nani akaniambia ni Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar.
Kuna ujenzi pia wa kiwanda kikubwa sana kilometres 2 hivi ukitoka Kibada kuelekea Kisarawe B kinatajwa kwamba ni cha kwake pia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Raisi Mwinyi anafanya kazi kubwa na nzuri sana , hakika atakumbukwa kwa hiki anachokifanya , tatizo wale wezi waliokuwa wanaiibia nchi wamebanwa hawapati kile walichokuwa wanapata ndio wanaleta tuhuma zisizo na kichwa wala miguu...

Miaka3 mitatu ya raisi Mwinyi tunajivunia.
 
Asubuhi ya leo nikikatiza maeneo ya mbuyuni huku Mbezi Beach wakati naelekea mjini tulipofika maeneo ya Kwa Mwinyi, pale ilipo nyumba yake ya miaka mingi rafiki yangu akanionyesha kiwanja kikubwa chenye heka kadhaa.
""""Njaa zikituzidi tunaanzisha habari za kumnyooshea kidole kiongozi fulani ilimradi tu kujifariji sisi wenyewe"",
,,

,Penyewe haswaaaa!!!!
 
Asubuhi ya leo nikikatiza maeneo ya mbuyuni huku Mbezi Beach wakati naelekea mjini tulipofika maeneo ya Kwa Mwinyi, pale ilipo nyumba yake ya miaka mingi rafiki yangu akanionyesha kiwanja kikubwa chenye heka kadhaa.
heshimiwa, Njaa zikituzidi tunaanzisha habari za kumnyooshea kidole kiongozi fulani ilimradi tu kujifariji sisi wenyewe.
Mwinyi ana tamaa sana ya kumiliki vitu vikubwa. Nakumbuka wakati baba yake ana umri wa zaidi ya miaka 90!alilazimishwa ajengewe nyumba ya rais mstaafu yenye thamani ya tshs bil 7 miaka kama 8 iliyopita maeneo ya masaki nyuma ya hotel yao ya sea Cliff, huku akijua kuwa mzee mwinyi ana majumba ya kutosha na umri umeenda sana. Lengo lilikuwa aimiliki yeye na aliisimamia
 
Nchi ina viongozi majangili tupu
 
Hapana, pamoja na udikteta wako lakini hakupenda sn familia yake iingie kwenye siasa na wizi wa nchi.
Madikteta hupenda kuwarithisha Watoto wao Madaraka na huyu angefanikiwa kututawala hadi uzeeni na angemuachia Mwanae.

Sio mimi ni Historia ndio inasema hivyo.
hqdefault.jpg

Mobutu alikuwa amemuandaa Kongolo
1974-president-mobutu-sese-seko-r-currently-on-a-visit-to-uganda-for-F3F7B2.jpg

Iddi Amini nae alikuwa anamgroom Mwanae.
 
Back
Top Bottom