Burkinabe
JF-Expert Member
- Feb 12, 2023
- 1,892
- 3,196
Wakati Rais Hussein Mwinyi anaingia madaralani, uchumi wa Zanzibar ulikuwa kunakuwa kwa asilimia zisizozidi 5. Lakini ndani ya kipindi cha miaka 3 tu uchumi wa Zanzibar leo unakua kwa asilimia 6.8 huku wa bara ulikuwa unakua kwa asilimia 7 kabla ya kifo cha Rais Hayati JPM tena katikati ya janga la dunia Covid 19, lakini mwaka mmoja tu baadaye (baada ya kifo cha JPM), uchumi wetu ukadorora hadi kufikia asilimia 4!
Leo hii Zanzibar miradi imekuwa inaanzishwa na kukamilika tena kwa wakati na ubora wa hali ya juu tena kwa Gharama zile zile zilizowekwa. Lakini kwa upande wa bara tumekuwa tunapigwa tu kalenda (mfano SGR, JNHPP, JPM Bridge n.k)!
Mfumko wa bei kwa Zanzibar ni karibu asilimia 0, lakini kwa huku bara toka aondoke Rais aliyepewa dhamana na wengi, leo mfumko wa bei kila mmoja ni shuhuda! Na bahati nzuri wengi wetu (ukiondoa mafisadi na familia zao) tunapigika ipasavyo. Mfano nauli za daladala toka 300 hadi 600, nauli za mabasi ya mikoani kama vile Mwanza hadi Dsm kutoka elfu 60 hadi zaidi ya elfu 80, sukari toka 1,600 hadi 5,000 kwa kilo, mche wa sabuni toka 1,500 hadi 3,500! N.k.
Kwa hayo machache, naona kama Mtanzania mzalendo, ninayeipenda nchi yangu na raslimali zake zote ikiwemo watu, Rais Hussein Mwinyi atatufaa zaidi akija huku Bara. Mama tunampenda sawa, lakini amalizie tu hii miaka yake ya urithi aende zake akalee wajukuu zake huko Kizimkazi.