Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Hata bungeni mjadala huu ulikuwa mgumu sana na kwa hakika haukupatiwa majibu mpaka leo tunatumia dhana tu ili hili jambo lipite, lakini kama unafahamu nature ya Zanzibar ilivyo bado wengi wape itaendelea tu mkuu! Huwa sifahamu viongozi wa serikali wanapata wapi nguvu kutangaza hali hii!
Nadhani hii ni made in Zanzibar only.

Vv
 
Upande wa pili upi? Dini zote si zimeletwa either na waarabu au wazungu, hata history inasema. Ndiyo maana tunautofauti mfano ukienda nchi za South east asia ambapo wamishionari walichelewa kupenetrate unakuta wengi ni buddhist na si wakristo wala waislamu. Missionaries au arabs wangewahi kule hizi nchi nazo zingekua zimejaa wakristo, au waislamu. Bado mtu anataka proof kua dini imesambazwa toka na kikundi flani cha watu wachache. Dini zote ovyo tu, story zilizotungwa na wanadamu.
Ahaaa,kwa hiyo nani aliwaumba wanadamu?????.
 
Kwani mukila mpaka mujionyeshe acheni uchokozi kama kweli muna dini
Mwenye imani thabiti ya dini hawezi kutenda dhambi ati kwa sababu amemwona jirani yake akitenda dhambi. Watu wa dini mjitahidi kukua kiroho na kuwa imara kiimani.

Vv
 
Upande wa pili namaanisha imani zengine.
Unajua kujibu suala hili,linataka ukusanyaji wa imani zote,halafu zitiwe katika mchujo wa fact of atleast of how it imagined/root,halafu unakuja kwenye ideology,fainali utapata mbili za mwisho,na hapo ndipo yatakapokuja maamuzi thabiti,lakini itumike mizani ya fact/uhalisia sio ushabiki,naamini haitokuwa taabu kwa mwenye kuutafuta ukweli.
 
Kumbuka kuna miungu zaidi ya 3000. Unataka story ya mungu yupi nikwambie kaanzia wapi?
Ni kama siku hizi tu story zinaanza polepole za mtu zinaanza kukuzwa, chukulia mfano Elon Musk, na mambo yake ya kutaka kupeleka watu Mars, kuweka renewable energy sources kwenye kila nyumba, its science leo tunaelewa hivyo, ila kuna kikundi cha watu wachache wanamuona jamaa kama mwokozi vile, story zinasambaa polepole, zinakuzwa, inafika muda watu wanaanza kuzikisia zimekuzwa kweli utadhani jamaa kageuka mungu anataka kukomboa wanadamu, sasa kwa leo unaweza ona upuuzi maana tumeendelea, ila miaka elfu kadhaa nyuma, hata kipaji cha kawaida tu mtu unaonekana very extraordinary, people were ignorant ukilinganisha na leo. Soma biblia na quran uone vifungu vinavyopingana mule, anayesema vinaongelea amani namshangaa sana, maana vimejaa utumwa, ukandamizaji wa wanawake, mauaji, tena in plain direct text.

Ungezaliwa alafu usijazwe dini kichwani ukaachwa hadi ufike umri wa mtu mzima tuseme miaka 20, alafu ukaanza kuambiwa kuna mungu, mtu aliyetenganisha bahari kwa fimbo, ungeamini kweli? hehehe
Wewe umeona Mars ni moja ya kitu kikubwa katika maumbaji Kwa ujumla??.wewe una falsafa/ideology ya kwamba vitu vimejiumba wenyewe???.kuna uwezekano mkubwa,ya kwamba umekosa kujua mambo muhimu,na kujifahamu,mawazo Yako mbalisana kutoka kwenye uhalisia,nakupa ushauri ukilichunguza jambo hili usiwe na pupa,wala Ustashi wa kiimani tafuta haki na ukweli.
 
Hapo ndiyo mjue kuwa siyo wote wanaoabudu wanamwabudu Mungu wa mbinguni. Wengine wanaabudu sheria zilizowekwa na wanadamu ili kuwakandamiza wanadamu wengine. We ukifika zenj kandamiza msosi kwani kufunga watu walazimishana. Mtu akikutisha paza sauti wanasheria tutakutetea.
Waislamu wa zanzibar ni wabaguzi sana we fikiri wanambagua hata muislam kutoka tz bara eti wanasema hawaijui dini ya Kiislam vizuri sasa ambaye si muislam atasalimika
 
Waislamu wa zanzibar ni wabaguzi sana we fikiri wanambagua hata muislam kutoka tz bara eti wanasema hawaijui dini ya Kiislam vizuri sasa ambaye si muislam atasalimika
Hayo mimi siyajui,na wala sijasikia hilo,ingekuwa vizuri ukawapelekea waisilamu wa Zanzibari.
 
Unaowaita wahamiaji ni Watanzania, mtavimba mpasuke wale watabaki kuwa kwao Zanzibar, hata hivyo wazanzibari waliozaliwa Bara ni chini ya 50,000 ila sote tunajua kuwa Watanzania waliozaliwa Zanzibar ni 800,000 Dar peke yake nusu. Hata hivyo WAKRISTO ZANZIBAR NI 30% upasuke ila ndio ukweli. Ukiweka hao unaowaita wageni wa Bara, Wakenya, Wazungu na Wawekezaji wa nje. Pia watalii 300,000 ambao 99% ni Wakristo.
By the way, watalii watakula wapi kama migahawa yote inafungwa? huu ni uhujumu uchumi ukizingatia taifa linategemea sana tourism
 
By the way, watalii watakula wapi kama migahawa yote inafungwa? huu ni uhujumu uchumi ukizingatia taifa linategemea sana tourism
Huwezi kuwapangia na kuwalazimisha wafate imani yako,ukumbuke uislamu ulifika kule Zanzibar Miaka 1400 iliyipita,si kwamba wanafanya Kwa kubahatisha,watalii ni kitu kipya na hakina ulazima kwa wazanzibari,na kitu ambacho,piga kufa hakina thamani kubwa mbele ya imani zao,lazima ufahamu vile vile,lazima ufahamu visiwa vya Zanzibar ni baba wa ustaarabu Kwa Afrika mashariki na Afrika Kwa ujumla,nakushauri utakapokwenda zanzibari,inaonesha umekosa kitu fulani,nenda Zanzibari kwa kusoma ustaarabu.
 
Nawatakia mfungo mwema ndugu zangu Waislamu. Msiache kunialika kufutulu huo ndio undugu.
 
Munajivunia mambo yasiyokuwepo na wala hayatakuwepo kamwe! Jivunieni kugundua tekinolojia ya kuongeza uzalishaji Wa kilimo cha Tende na Alua.Jivunieni tekinolojia ya kuongeza thamani ya Karafuu ili mpate soko kubwa hata mkaweze kuuza nje ya nchi. Sasa ninyi munajivunia kufuga "popo"! Hao "popo" wamewasaidia vipi katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja au kama Taifa? Hao popo wamewasaidia vipi kutafiti na hatimaye kuchimba mafuta tunayosikia kuwa munayo hapo Visiwani?

Kuhusu technology ya "POPOBAWA" haitusaidii lolote directly katika uchumi au uzalishaji wa tende na halua.

Hili nataka ufahamu kuwa tende sio zao linalokuzwa Zanzibar isipokuwa wananchi wake ni watumiaji wakubwa wa tunda hilo, material makubwa ya halua ni UWANGA ambao alhamdulillah inazalishwa vyakutosha Zanzibar.

Kuhusu thamani ya zao la karafuu alhamdulillah iko njema sema tu serikali ya kidhalim ya Zanzibar inawapa bei ndogo wakulima na ndio maana inasafirishwa kimagendo kuelekea Mombasa Kenya ambako bei ya huko iko poa kiasi, na alhamdulillah kwa baraka ya zao hili ndio maana wapemba kwa kiasi flani linawabadilisha maisha yao kuwa nafuu kulinganisha na Unguja.

POPOBAWA linatusaidia indirect na ndio maana mtu akileta ujeuri Pemba huyu ndio huwa kiboko yake! Tokea 1995 uchaguzi wa vyama vingi urudi tena Zanzibar CCM haijawahipo kupata hata kiti cha udiwani Pemba hii ni kwasababu wapiga Kura wako strong huwezi kuwanyang'anya chaguo lao kirahisi lakini pia hii silaha inawatisha wagombea wa CCM.
 
Mkuu umeeleza tu asili ya Mfungo au Ramadhani lakini hujaeleza maudhui ya mtu mwingine asiye muislamu kukatazwa kula hadharani.Kama ulivyoeleza vizuri kuwa maudhui ya ninyi kujifutarisha hadharani katika makundi ni njia mojawapo ya promotion ya Uislamu ndivyo naomba pia utueleze maudhui ya watu wengine wasiohusika na mfungo kukatazwa kula hadharani.

Kwa mujibu wa dini yetu ya kiislamu hakuna mtu hahusiki na mfungo wa Ramadhan labda kwa wale ambao Quran imebainisha wenye dharua mbali mbali kama wagonjwa, watoto, wasiojiweza nk. na hawa wanaruhusiwa kula kadri wawezavyo kula lakin si hadharani. Lakini kama wewe si muislamu na unataka kula hadharani ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mpaka utakapoleta hoja (references) ya hiyo Imani yako kupindua hoja niliyoiweka ili tuone kama una uhalali (ruhusa) kula hadharani mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Lakini katika hali ya kawaida kwa nchi ya Kiislam kama Zanzibar marufuku ya kula hadharani Mwezi Mtufuku wa Ramadhan ndio mahali pake.
 
Ukiona mambo ya Mungu yanalazimishwa kwa mtutu wa bunduki jua hapo kuna unafiki mkubwa. Kuna watu wengi sana watashinda njaa wala si kufunga.
Mambo ya imani yanatakiwa yawe ya hiari na ndio Mungu anakubali hilo jambo. Wao wakazane kuelimisha jamii yao umuhimu wa kufunga Ramadhani na thawabu zake, halafu wawa ache wale watu wafanye uamuzi, maana ukiweka sheria ya kudhibiti atakayeonekana hajafunga, bado hujamsaidia mtu yule ambaye alitaka kula lakini ukamtisha au ukafunga hoteli. Hiyo ni logic amabayo wala haitaji ubishi.
 
Unafiki huu, wakija boko haram, na IS kkutaka sheria za kiislam zitumike nchini mwao huko watawafurusha kwa vifaru na kuwaita magaidi, ujinga ujinga tu.. mtu unatakiwa uikana nafsi sio uifiche isione..msweeee.
 
Msimu wa mauzo madogo ya ike nyama umewadia...
Biashara itarudi tena kuanzia tarehe 27/6/2017
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom