Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.

wamisako

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
917
871
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
 
Znz ikifika kipindi cha ramadhani, ukienda dukani kununua vyakula vya fast food hawakuuziiw(mfano soda, mikate, maji)...
Na hata ukishikwa na kiu, ukasema uende kuomba maji kwenye nyumba hawakupi.
Inshort wanabana mianya yote ya watu kula mchana, unakuta vyakula vinauzwa hotels za kitalii tu,
Na hata kama ni mkristo, wakikuona unakula njiani wanaweza kukufanyia vurugu,
 
Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine

Sasa kama kila dini kuheshimu dini nyingine, kwanini waislamu nao wasile kama wakristo ili kuheshimu ukristo, mbona wao wanakula hadharani wakati ya kwaresma? Huyu kiongozi atakua na vyeti feki.
 
Hata kama ikitokea watu kumi tu zanzibar ndiyo wakawa si waislamu bado hawastahili kubanwa kiasi hicho kisa imani ya mtu mwingine.Imani hailazimishwi waislamu jitafakarini sana ktk taarifa hiyo.
Uhuru ni utajiri, kuna watu mnawalazimisha kufunga hawana mpango wa kufunga hivyo mnatenda dhambi kwa kuwakosesha uhuru.
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Jamani walichokataza ni kula hadharani ,lakini ukiwa ndani ni ruksa,pale Maisara ukumbi wa CCM na ukumbi wa Magereza na hata hotel kubwa bado hutoa huduma za vyakula na hii sio kitu kipya kwa Zanzibar kipo tokea enzi za Karume tena siku hizi ni nafuu zaidi kuliko miaka ya nyuma,tutake au tusitake Zanzibar ni kama nchi ya Kiislamu ,90.9% ni waisalamu.
 
Hivi wewe ukiwa umefunga nami nakula chakula changu hadharani inakuuma nini....!!?? Hivi ina maana wakristo huwa hatufungi?? Mbona tunaishi na nyie vizuri...
Hata kama mfanyakazi wako wa ndani kama siyo muislam mpe uhuru ale kwa muda wake... Wewe uliyefunga uko na Mungu wako... Kumnyima uhuru mwenzio kisa umefunga hain maana... Na mfungo wako ni batiri...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom