Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Uzuri wenyewe bado yuko hai na afya tele nenda kamuulize ili upate ithibati ya maneno yangu!!

Nitajaribu kuipata clip ya maneno yake juu ya ushirikina wa wapemba nikienda hapa.

Munajivunia mambo yasiyokuwepo na wala hayatakuwepo kamwe! Jivunieni kugundua tekinolojia ya kuongeza uzalishaji Wa kilimo cha Tende na Alua.Jivunieni tekinolojia ya kuongeza thamani ya Karafuu ili mpate soko kubwa hata mkaweze kuuza nje ya nchi. Sasa ninyi munajivunia kufuga "popo"! Hao "popo" wamewasaidia vipi katika maendeleo ya mtu mmoja mmoja au kama Taifa? Hao popo wamewasaidia vipi kutafiti na hatimaye kuchimba mafuta tunayosikia kuwa munayo hapo Visiwani?
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu


Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Zanzíbar hakuna harufu ya udini, ni Taifa la dini ya kiislam.
Halafu hakuna anayekatazwa kula bali kula hadharani na kuendesha biashara za vyakula barabarani.
Kuhusu kwaresma hata wakristo wenyewe hawajui hallmark ya kwaresma ni nini? Wengine wanatafsiri kutokula kabisa, wengine just taking portion wengine vitu tu usivyovipenda. Ila kwa ya le yaliyokuwa determined na imani yenu tunayafuata mfano ijumaa kuu, pasaka tunaheshimu kwa kadri mlivyoelekeza
 
In fact ni ratiba ya msosi imebadilishwa.badala ya mchana vitu vinamegwa usiku kwa kiwango kilichozidi ile desturi ya mchana!!
Ni sawa kabisa
Ramadhani lengo lake wala si kushinda na njaa, hiyo ni just a symbol tu, ni kama wewe ukiheshimu msalaba au kanisa unadhani hivyo vitu huwa na tofauti na majengo au furnitures nyingine?
Kuna tofauti gani katika mbao ya kiti cha bar na mbao ya msalaba? Au tofali zilizojenga dangulo na zile zilizojenga kanisa?
We elewa tu kukaa na njaa mchana is just a symbol, hivyo hatushindani kukaa njaa, tunahimizwa kufanya ibada zaidi
 
Kiufupi mifungo ya namna hii ni kwa ajili ya shows tu.Ni kwa ajili ya kujitangaza tu kama uonavyo watu wakifanya pale viwanja vya DabaSaba.Ingekuwa mfungo ni kwa ajili ya kuwasiliana na Mungu basi ungeweza kufanyika hata usiku.Lakini hawataki kufunga usiku kwa sababu nyakati hizo watu wanakuwa wamelala na hivi hakutakuwa na mtu Wa kuwaona.
We nawe boya!

Kwa same line of thinking unawaonaje wanaoenda kanisani ni sababu ya show off, hivi wasingeweza kusalia majumbani? Mungu hasikii sala za majumbani?
Fikiri kabla ya kuropoka....
 
We nawe boya!

Kwa same line of thinking unawaonaje wanaoenda kanisani ni sababu ya show off, hivi wasingeweza kusalia majumbani? Mungu hasikii sala za majumbani?
Fikiri kabla ya kuropoka....

Sawa mkuu Mimi boya.Uboya wangu unatokana na hiyo hoja yangu au kitu kingine? Hoja yangu ni kwa nini mfungo uwe mchana tu na sio usiku pia? Kwani kutokula kukifanyika usiku Mungu hawezi kugawa sunah? Au na yeye anakuwa amelala?
 
Duuu kusema kwel wakristo hawatendewi haki mi nishawahi kushuhudia maeneo ya magomeni kuna mtoto kama ana miaka 15 kwa kukisia alikuwa anakula ubuyu kipigo alichopigwa nahisi hatorudia kula hadharani
 
poleni wakristu mlio zenji ila kama wangetoa tamko na hapa bara weeee pangechimbika.
 
Hawa ndugu zetu wa kiislamu wamekaa kishari shari sana yani sijui wapoje yani nisile kisa we umefunga. Hivi hii imani yenu inawafundishaga nini mbona mnapenda roho mbaya mbaya.
 
Hawa ndugu zetu wa kiislamu wamekaa kishari shari sana yani sijui wapoje yani nisile kisa we umefunga. Hivi hii imani yenu inawafundishaga nini mbona mnapenda roho mbaya mbaya.
Hujalazimishwa kukaa nchi ya watu, rudi kwenu,mnajipendekeza tu. Haaaah, rekebisheni katiba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom