Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Kwani huku kufunga ni imani ya mtu au ndio kulazimishana kutokula mchana? Hizi imani zingine za shuruti hizi...zipewe polisi wasimamie basi
 
Yani Mie Niende huko kwa biashara zangu halafu nilie chakula uvunguni???? Hii haipo! Wao Mbona hawakufanya hivyo na Kwaresma????
Nadhani kuna haja ya kufikiria kwanza ndio utoe tamko
 
Zanzibar nawaaminia, njooni na huku bara mtoe tangazo "WATAKAOKULA RAMBIRAMBI KUKIONA".
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu


Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Zanzibar ni nchi ya kiislamu ile sema watu wa bara ndio tunaibana... 99% muslims
 
Mi nafikiri ukiwa umefunga halafu mwenzio anabutua pilau mbele yako na ukaweza kuvumilia ndo imani hiyo maana umeshinda majaribu! Sasa iweje ufunge halafu hutaki kuona mwenzio anakula, hayo ni mambo ya kulazimishana kufunga, maana itaanza taratibu hivyo kwamba isiwe hadharani baadae watatoa amri kwamba hakuna anayeruhusiwa kupika mchana wakati wa mwezi mtukufu, tujifunze 'tolerance'
 
unaona au uhalisia huo😵😵😵
more than 90% ni Muslims
e2a876d3bad9b5c5df5f6764310cf93a.jpg
 
unaona au uhalisia huo😵😵😵
more than 90% ni Muslims
Sawa. Lakini hao 1% au 10% wana gaki ya ku practise dini yao vyovyote wanavyotaka. Kama wanakula majumbani mwao mabarazani shida iko wapi? That is bigotry! [emoji57] [emoji57] [emoji57] [emoji57]
 
Mi nafikiri ukiwa umefunga halafu mwenzio anabutua pilau mbele yako na ukaweza kuvumilia ndo imani hiyo maana umeshinda majaribu! Sasa iweje ufunge halafu hutaki kuona mwenzio anakula, hayo ni mambo ya kulazimishana kufunga, maana itaanza taratibu hivyo kwamba isiwe hadharani baadae watatoa amri kwamba hakuna anayeruhusiwa kupika mchana wakati wa mwezi mtukufu, tujifunze 'tolerance'
Dini haiendeshwi kwa akili za MTU, kwamba Mimi nafikiri Bali ni sharia IPO katika vitabu vitukufu sisi ni kufuata tu. Hakuna andiko linalosema hivyo unavyofikiri Bali lipo linalosema anapata dhambi anaekula mchana Wa Ramadhani au kulisha bila dharura. Yule anaekula hadharani pia anapata dhambi kwa kumfanyia karaha mfungaji.
 
Imani yako inakomaa kwa kukinzana na nafsi yako kujizuia kufanya mambo mabaya

Kuwazuia watu kufanya yale ambayo ni kipimo cha imani yako kwenye nafsi ni udhaifu wa imani yako kwenye nafsi yako.....

Kama wewe umefunga kutoka kwenye nafsi yako kwa imani yako kwanini uhangaishwe na mtu anayekula na kunywa.....!!??

Sasa unakuwa umefunga kwa imani au umejizuia....!!??

Kipimo cha imani ni kipi hali unazuia majaribu kwenye imani yako...,,!!?

Ni mtazamo tu
 
Waliotakiwa kulalamika ni wakazi wa huko wasio kuwa waislamu lakini cha ajabu wanalalamika wale ambao hawapo.Lazima mufahamu kuwa kila sehemu kuna adabu na tanaduni zake na hata kama mkisema mfuate demokrasia ambayo huangalia matakwa ya majority bado wazanzibari wako sahihi.alafu tabia ya kula barabarani ovyo ni tabia mbaya regardless .Alafu kwa nyie msiofahamu utamaduni huo uko zanzibar enzi na enzi sio leo wala jana na umekuwa ukiheshimiwa na wageni na wenyeji
 
Hizi ndizo dalili za serikali kuwa na dini.
Ni bora ikatangazwa kimataifa ili wageni wasijisumbue kwenda zanzibar !!!
Kila mwaka iko hivyo ni utamaduni wa wazanzibari. Na wageni wala hawashangai naona ni nyie mnaotaka kuanzisha chokochoko.
 
[QUOTE="SIM, pob21209328, member: 5Hutokeyimwa kula. kula kwa kujistiri siyo kula huku unatembea barabarani kama bata.

OVER![/QUOTE]

Kwa mantiki ya kawaida ni kwa nini hutokea mtu akala huku anatembea? Ziko sababu kadhaa za kiuzoefu.Moja ni kwamba mtu anakuwa anataka kuokoa muda.Kwamba badala ya kutumia muda Fulani kukaa kula chakula mtu huyo anaamua kuendelea kula huku wakati huo huo akifanya jambo jingine.Au wakati mwingine ni aina ya chakula chenyewe.Viko aina vya vyakula havimulazimishi mtu kuketi chini kuanza kula chakula.Mfano mahindi, Karanga, Biskuti, Ice cream na vinginevyo.Wauzaji Wa vyakula hivi wengi wao hawana nafasi ya mteja kuweza kukaa ili kula hicho alichojinunulia.Vile njaa huwa haitoa alarm inapomuuma mtu.Hutokea mahali popote na muda wowote ule.Kwa hiyo kumwambia mtu asiye na kizuizi chochote cha kujipatia chakula asile chakula kwa staili itakayomfaa kwa kisingizio kuwa ni utamaduni Wa muda mrefu huko ni kukengeuka kimantiki.Utamaduni hauwezi kuwa juu ya afya za watu.Utamaduni hauwezi kuchukua kipaumbele cha afya ya mtu.Chakula ni nguvu ya binadamu.Nguvu ni pumzi ya mwanadamu.Kama sababu ni utamaduni kuna mambo mangapi tumeyaacha Leo na kutumia mibadala yake? Zanzibar leo wengine hawatumii vyoo vilivyojengwa kwa makuti ya Minazi au nyasi badala yake wanatumia vyoo vilivyo ndani ya nyumba na tena vya kukaa.Hawatumii majani kuchambia badala yake wanatumia tissue.Binadamu sio mtumwa Wa utamaduni Bali yeye ndo hutengeneza utamaduni.Utamaduni wapaswa hutokane na matumizi ya mantiki.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom