Tusichanganye ramadhan ya zanzibar,uislamu,na utashi wako wa kiimani,Kama muumini wa Roman Catholic,Kwa upande wako umetaja isis,book haram,Yakiwa na chanzo cha kuanzia,haya yanaondela katika wakati huu,lazima ufahamu kuna waislamu 1.5 billion ulimwenguni,takribani imani nyingi za kidini zinapinga mauaji yasiyo na hatia,hapa hatushabihishi kikundi au mtu au taifa fulani,ukichukulia hivyo kila upande utakuja na ushahidi tosha,sitaki niingie huko Kwa sababu hukumu inamhusu yule au wale watenda kosa kukiwa na ushahidi,Kama kwa hatuwezi kuwalaumu wakristo kwa udondoshaji mabomu ya atomic/nuklia kule Nagasaki na hiroshima,au mauaji ya hitler,au lords of resistance cha uganda,joseph konya ambaye anauwa watoto kutokana na itikadi zake.yako mengi yanayohusiana na hayo,na yatachukua muda,lakini naamini hayatoleta Faida Kwa upande wowote,jambo la msingi ni kuhishimiana katika Imani zetu za kidini,na kuvumiliana,nitakupa mfano sikukuu zote za kiislamu,Kama eid el hajj hazina holiday/siku za mapumziko katika nchi za kimaharibi(kikristo)hapo zinafuata democracy na securalism/siasa za kimataifa,na kuna waisilamu wanalalamika kwa hilo,lakini ukitizama nchi hizi zina asimia kubwa ya wakristo,mambo Kama hayo yapo china na kwengineko,ukitizama hata hapa Tanzania hakuna usawa katika siku za wikiendi ambazo tulidhirithi kutoka Kwa wakoloni wa kiingerza,ambazo zinatoa nafasi Kwa wakristo kwenda kanisani jumamosi na jumapili na zinawanyima waislamu kwenda kwenye sala yao kuu ya ijumaa,jambo ambalo ni upendeleo mkubwa ambalo linafaa vile vile kutafutiwa maamuzi.
Ushauri wangu Kama Ni watanzania tuache utashi wetu wa kiimani,kama tunataka amani na maendeleo