Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Hii Nchi haiongozwi na Dini yoyote. Hakuna sheria yoyote ya Nchi inayomzuia mtu kula mchana wala usiku.
 
Karibu twende,nilipoenda zanzibar nilijua hakuna kitimoto!Inapatikana tena kuna mafundi wa kuandaa hataeii
Zanzibar haijasalimika na makafiri wako kule na ndio maana wanatahadharishwa kuwa na staha mwezi wa Ramadhani
 
unaona au uhalisia huo😵😵😵
more than 90% ni Muslims
Sio 90% ndo waislam sema 99% ni waislam hizo amri zipo kabla ya Muungano lamsingi hao wenye itikadi nyingine wanatakiwa kutii tu.ni masiku machache lakini yana kheri nyingi sana na ndani yake kuna makumi matatu.
 
BanKutum 21225488 said:
unazungumzia kula hadharani jioni wakati wa kufungua, wakati zuio ni la mchana wakati watu wamefunga !

Kula sana kupita kiasi kumekatazwa kwa sababu utasababisha mfumo wa umeng'enyaji chakula mwilini utashindwa kufanya kazi sawasawa.Matumizi zaidi ya kipato yako discouraged kwa sababu mbeleni utashindwa kukidhi mahitaji.Sasa tueleze kula hadharani kumekatazwa kwa sababu gani?
 
Asante kwa kuchangia.Sasa hebu tueleze mantiki ya kidini ya kukataza waislamu kutokula hadharani mchana wakati Wa Ramadhani? Mtume alipokataza watu wasijilie hadharani alitaka kufundisha nini hasa? Kuna picha humu zinawaonyesha waislamu wakifuturu nje jioni.Je, Mtume alitaka kufundisha nini kuruhusu watu wale hadharani jioni?

Well., Unajuwa Ramadhan ina mafunzo na mantiki nyingi sana lakini labda kwa uchache:-

1. Kwanza ni Kutekeleza sheria ya Ibada funga kama tulivyoamrishwa katika Quran kitabu kitukufu. ""Fungeni mwezi mtukufu wa ramadhan kama walivyolazimishwa kufunga walikuwa kabla yenu ili mupate kumcha M/Mungu"' (kwa ajili ya andiko hili ndio mana tumekatazika waislamu kula mchana mwenzi Mtukufu wa Ramadhani) Na Mtume alipokataza tusijile mchana mwezi wa Ramadhami pia sababu ni hiyo hiyo apo juu tu ambayo Quran tukufu imetutaka.

2. Iyo kufuturu nje na kwa magroup jioni ni kuonyesha umoja katika uislamu lakini pia kunyesha mapemzi baina ya waislamu kwamba wamekusanyika wenye nacho wasionacho lakini hawakujali nafasi zao wala utajiri wao wamechanganyika ili kuleta usawa. Lakini pia ambao hawajabahatika kuwa waislamu wakiwaona waislamu katika hali ile ya umoja wakitekeleza Ibada inaweza kuwa ni sababu na wao kuwa waislamu na kujumuika katika hii Ibada ya funga ili na wao waweze kuepukana na adhabu ya moto siku malipo wafutiwe madhambi yao na waweze kuingizwa peponi na Allah Subhana Wataala Mola wa viumbe vyote.

Zipo nyingi fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lakini nitakuwa nakupa kadri utakavyokuwa na hamu kujuwa.
 
Kula sana kupita kiasi kumekatazwa kwa sababu utasababisha mfumo wa umeng'enyaji chakula mwilini utashindwa kufanya kazi sawasawa.Matumizi zaidi ya kipato yako discouraged kwa sababu mbeleni utashindwa kukidhi mahitaji.Sasa tueleze kula hadharani kumekatazwa kwa sababu gani?
Wewe unahitaji kula ukidhi njaa yako au unata kula hadharani !? ...ni wazi unataka kufanya karaha tu kwa wafungaji !
 
Zanzibar haijasalimika na makafiri wako kule na ndio maana wanatahadharishwa kuwa na staha mwezi wa Ramadhani
Kwamba wafunge biashara zao ama?Halafu Rais wa viunga vyote ni kafiri kwa mujibu wenu!
 
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar(SMZ) imetoa onyo kwa wananchi watakaokula hadharani katika kipindi cha mchana wakati wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma, Khamis Juma Maalim wakati akijibu swali la mwakilishi wa jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub aliyetaka kujua serikali inatoa tahadhari gani kwa watu watakaobainika kula mchana wakati wa Mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema utamaduni wa wananchi wa Zanzibar ni kuheshimu kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa makundi yote ikiwemo wa dini tofauti. Alifahamisha kwamba utamaduni huo upo hata kabla ya Mapinduzi ya Januari 12 mwaka 1964 wa dini tofauti kuheshimu dini za watu wengine.

Alisema kazi ya kutoa elimu kuhusu ujio wa mwezi mtukufu wa Ramadhani imeanza kutolewa na Ofisi ya mufti ambayo ndiyo yenye jukumu la kushughulikia masuala ya mambo ya dini ya Kiislamu.

Alisema kazi kama hiyo imeanza kutolewa na maimamu wakuu wa misikiti mbalimbali Unguja na Pemba ikiwemo katika sala za Ijumaa ambazo hukusanya idadi kubwa ya Waislamu kwa wakati mmoja.

Alikiri kuwepo vijana wengi wanaoacha kufunga katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kula hovyo pamoja na kuvuta sigara. Maalim alisema zipo taarifa kwamba hoteli nyingi hufanya kazi wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ambapo wateja wake wakubwa ni vijana wa Kiislamu. Waislamu nchini wanatazamiwa kuanza mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wiki ijayo ambapo ibada ya funga ni moja ya nguzo tano za dini ya Kiislamu

Chanzo: Habari Leo
=====================================
Nataka kujua kipindi kwa kwaresma mbona hawakutoa tamko hili.

Kwaio wakristo wawe wanajificha wakati wa chakula cha mchana.

Hapana naona kuna harufu ya udini kuanza Zanzibar.
Kwa hiyo asilimia 2 hawana haki ya kulindwa na sheria hiyo? Na wakati wa kwaresma wanaokula mchana wanachukuliwa hatua gani? Pia muhimu kujua kama Zanzibar ni nchi ya kiislamu?
 
mlaaniwe mnaopinga tangazo la serikali
imeshatangazwa ni marufuku kula hadharani wewe una hoji nn sheria zipo na zitafanyakazi kwa wazembe watakaozivunja
 
Kwamba wafunge biashara zao ama?Halafu Rais wa viunga vyote ni kafiri kwa mujibu wenu!
Kupanga ni kuchagua ! wakafanye biashara kwengine.Rais wa viunga vyote sio Imamu wetu hivyo ukafiri wake hautuhusu
 
Sasa why uende kumuomba ''Abdallah'' akuchinjie kuku wakati Abdallah mwenyewe mlevi, mzinzi na anagonga mkuu wa meza kama kawa?
Si ndio hapo,mimi nilishasema mtu akinitembelea asiulize kachinja nani!
 
Zanzibar iko miaka nenda rudi.Hukatazwi kula kama ni mkristu Bali tunaambiwa usile hadharani.

Kwanza wanaweka onyo kwenye kila ofisi za serikali,public areas.Jamani hiyo IPO Zanzibar, tena ukishuka na ndege au boti hujavaa kitambaa wana kuomba ujifunge kitambaa kichwani.

Ninachokiona ni mila tu wala siyo issue ya udini nakumbuka waislamu ni 95%
Kwani mila inatambuliwa na sheria hadi kufikia kuminya uhuru wa jamii ingine usiokubaliana na mila hiyo kwenye taifa huru?
 
Kupanga ni kuchagua ! wakafanye biashara kwengine.Rais sio Imamu hivyo ukafiri wake hautuhusu
Hahahahaaaaa,nina mpango wa kufungua bucha ya kitimoto zanzibar maana nasikia biashara hiyo inalipa sana huko!Yaani mzigo haukai!
 
Well., Unajuwa Ramadhan ina mafunzo na mantiki nyingi sana lakini labda kwa uchache:-

1. Kwanza ni Kutekeleza sheria ya Ibada funga kama tulivyoamrishwa katika Quran kitabu kitukufu. ""Fungeni mwezi mtukufu wa ramadhan kama walivyolazimishwa kufunga walikuwa kabla yenu ili mupate kumcha M/Mungu"' (kwa ajili ya andiko hili ndio mana tumekatazika waislamu kula mchana mwenzi Mtukufu wa Ramadhani) Na Mtume alipokataza tusijile mchana mwezi wa Ramadhami pia sababu ni hiyo hiyo apo juu tu ambayo Quran tukufu imetutaka.

2. Iyo kufuturu nje na kwa magroup jioni ni kuonyesha umoja katika uislamu lakini pia kunyesha mapemzi baina ya waislamu kwamba wamekusanyika wenye nacho wasionacho lakini hawakujali nafasi zao wala utajiri wao wamechanganyika ili kuleta usawa. Lakini pia ambao hawajabahatika kuwa waislamu wakiwaona waislamu katika hali ile ya umoja wakitekeleza Ibada inaweza kuwa ni sababu na wao kuwa waislamu na kujumuika katika hii Ibada ya funga ili na wao waweze kuepukana na adhabu ya moto siku malipo wafutiwe madhambi yao na waweze kuingizwa peponi na Allah Subhana Wataala Mola wa viumbe vyote.

Zipo nyingi fadhila za Mwezi Mtukufu wa Ramadhan lakini nitakuwa nakupa kadri utakavyokuwa na hamu kujuwa.

Mkuu umeeleza tu asili ya Mfungo au Ramadhani lakini hujaeleza maudhui ya mtu mwingine asiye muislamu kukatazwa kula hadharani.Kama ulivyoeleza vizuri kuwa maudhui ya ninyi kujifutarisha hadharani katika makundi ni njia mojawapo ya promotion ya Uislamu ndivyo naomba pia utueleze maudhui ya watu wengine wasiohusika na mfungo kukatazwa kula hadharani.
 
Sasa why uende kumuomba ''Abdallah'' akuchinjie kuku wakati Abdallah mwenyewe mlevi, mzinzi na anagonga mkuu wa meza kama kawa?
Huyo ni kafiri mwenzio japo hilo ni jina tukufu, yaani Mtumishi wa Mungu, Usishangae hilo jina ukamkuta Mmakonde kampa mbwa !
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom