Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Mambo ya nchi nyingine haya kuhusu
Na nyie jipangieni yakwenu huko Tanganyika. We mwehu nini.
 
Wakati mnashangaa na kuona si sawa kwanini watu wanyimwe Uhuru wao wa kula mchana kwa wazi ndani ya mwezi wa ramadhani,basi ndivyo na wazungu wanavyotushangaa waafrika kwa kuwanyima Uhuru watu wenye kufanya mapenzi ya jinsia moja kwa kigezo kuwa ni kinyume na tamaduni zetu.
 
Hebu funga nenda na mkate wako then wakati watu wako kwenye swaum tembea huku unautafuna,utani pm ukimaliza.
Na nyie mnapenda kudeka sana. Kwanini muendekeze kula hivyo....kitendo cha wengine kutokula kisa nyie mmefunga ni kuwafanya msitamani.....sasa kama kweli unamuomba Mungu chakula ni kitu gani kwa masaa kadhaa tu? Tena hapo na daku mnakula wakati wakristo wengine hufunga hata masaa24 bila shida wala kumuingilia mtu uhuru wake. Kwani huko zanzibar hakuna wakristo au wapo chini yenu?
 
imefika hatu hawa watu wasiishi kwa kubebwabebwa na kulelewa kama vitoto vidogo.

haiingii akilini eti kiongozi Wa serikali anasimama kusapoti upuuzi Wa kuwazuia watu wasile hadhari kipindi Cha Ramadhani. huu ni ujinga Wa kiwango cha juu miongoni mwa waumini Wa dini hii na haupaswi kuvumiliwa


Hata mimi sukubaliani nalo, haya mataifa siyo ya kidini naerikali siyo ya kidini, sasa acheni watu wajiamrie watakavyo.
 
imefika hatu hawa watu wasiishi kwa kubebwabebwa na kulelewa kama vitoto vidogo.

haiingii akilini eti kiongozi Wa serikali anasimama kusapoti upuuzi Wa kuwazuia watu wasile hadhari kipindi Cha Ramadhani. huu ni ujinga Wa kiwango cha juu miongoni mwa waumini Wa dini hii na haupaswi kuvumiliwa

Mkuu nakushukuru sana kwa uzi wako huu.Nilichangia kidogo kwenye ile mada ya asubuhi iliyokuwa imeletwa na mdau mmoja.Kutokana na kufanya mambo mengine nilipanga baadaye nilete hoja hii upya hapa.Naona umenirahisishia kazi.

Suala hili sio la kuchekea hata kidogo.Hili suala kama ni la kidini basi swali lake halikupaswa kuulizwa kwenye Baraza la Wawakilishi linaloendeshwa kwa kodi za Waislamu, Wakiristu na Wapagani.Hatujawahi kuona Wakiristu hata siku moja huko Zanzibar nao wakataka kauli ya Serikali juu ya taratibu za Kwaresima au Noel zitakavyozingatiwa. Suala la dini ni suala la Muungano.SMZ isitake kujificha kwenye kisingizio kuwa bara hawahusiki katika jambo hili ili kukwepa nondo wanazovurumishiwa.Tukiongelea Katiba ya Muungano tunaongelea Bara na Zanzibar.Na kwa vile Katiba ya Muungano imetamka wazi wazi kuwa Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini maana yake Suala hilo ni binding hadi Zanzibar na mipaka yake yote.Haiwezekani suala litamkwe Kikatiba katika Jamhuri ya Muungano kisha liwahusu Wabara pekee.

Jambo la pili ni athari za kiuchumi zitokanazo na kukataza watu kula hadharani.Kuna watu wana biashara za kupika chakula kama mama Ntilie.Wapo wanaofanyia shughuli zao ndani na wengine chini ya miti tu. Wanauza chakula mchana na usiku.Unapokataza watu wasile hadharani wapikaji kama hao Wa chini ya miti unataka wakishawauzia wateja wao chakula hao wateja wakakodi sehemu za kwenda kulia chakula? Unapokataza watu wasile hadharani unataka hao mama Ntilie wakakodi "Fremu" za biashara ili wateja wao wawafuate huko ndani wale bila kuonekana? Unapokataza watu wasile hadharani unataka wauza Ice cream, Karanga, Bisi, wauza maji barabarani, wauza maandazi na kadhalika waende wakakodi Fremu? Kwa mtiririko huo huo ni dhahiri vipato vyao vitaathirika sana kipindi chote cha mfungo.Sote tunajua shule za msingi na sekondari zitafunguliwa mwezi Julai na hivi wanafunzi wanaporudi mashuleni wanahitaji kurudi na pesa au kununuliwa mahitaji kadhaa.Je, wazazi Wa wanafunzi wanaojipatia vipato vyao kwa kufanya biashara ndogo ndogo katika mazingira kama niliyoyaeleza hapo juu SMZ inataka hao watu wakose kipato na hivi hao watoto wao wafukuzwe shule au washindwe kurejea masomoni kwa wakati?

Hao wawakilishi na mawaziri Wa SMZ wanaosisitiza ban ya watu kutokula hadharani wengi wao wamewekeza huku bara.Wana hoteli na migahawa kibao huku.Waunguja na Wapemba wengi wana Maduka huku Bara.Wanauza Biskuti, maandazi.Wana Bakery huku.Kwa ufupi vitega uchumi vyao kibao viko huku.Kwa hiyo wanapopiga ban ya watu kujilia hadharani wakati Wa mfungo wao bado wana uhakika huku Bara mchana biashara zao zitakuwa zinaendelea vizuri.Wana uhakika wakiristu na wapagani Wa Bara wakati Wa mchana watanunua bidhaa zao hadharani bila kujificha kujificha.

Jambo la mwisho ni utetezi unaotolewa juu ya hili katazo.Eti ni utamaduni Wa Kizanzibari Wa muda mrefu.Utamaduni gani gani huo unaokuwa juu ya Katiba ya nchi? Eti ni suala la kiimani. Ni Mungu gani huyo anahalalisha wewe ukisali wengine wateseke? Mungu gani anakubali wewe ukisali wengine wajikunyate kunyate? Kwani hiyo imekuwa Bendera ya Taifa kwamba ikishushwa au kupandishwa sharti kila mtu asimame? Imani hiyo ni Wimbo Wa Taifa kwamba ukiimbwa basi kila mtu atulie tulii? Mungu gani asubuhi anakataza watu hadi saa kumi na mbili jioni wasile hadharani ila baada ya hapo watu wale tu kwa kadri wapendavyo nje ya Nyumba, vibarazani, barabarani na sehemu zinginezo? Waislamu hatuwasemi vibaya ila munahitaji kuipa uhuisho (review/reformation/rebirth) baadhi ya mafundisho yenu.Dunia inawaacha ikiwa mutaendelea na tradition za namna hii.
 
kule haki yao kusema hivyo, nyumbu wengi eti hapa dar jua kali hili weekend niache kula jibapa na kitu ya kuchoma mchana kisa imani ya mtu mwingine 🙂, huko ni kuto jiamini inaonyesha tamaa inazidi imani hadi ukiona mwingine anakula wakati we umefunga unaharibiwa funga yako [HASHTAG]#mtazamo[/HASHTAG]
 
Hata mimi sukubaliani nalo, haya mataifa siyo ya kidini naerikali siyo ya kidini, sasa acheni watu wajiamrie watakavyo.
Mbona hatuoni watu mkiwa tetea mashoga kwa kunyimwa kufanya watavyo? Leo mwanamke na mwanaume wanazini kama kawaida na si kosa ila mashoga wanakamatwa.
 
Kilichoniacha hoi kwenye hilo tangazo ni kile kitendo cha kulazimisha waisilamu wote wafunge. Kama mtu anataka kufunga atafunga kwa hiari yake na sio kwa kulazimishwa. Inaonekana huko kufunga walio wengi hawatilii maanani ila ni mpaka itumike nguvu ya serekali kuhakikisha watu wanafunga. Sasa najiuliza ukikuta mtu anakula hadharani akipelekwa mahakamani anafungwa kwa sheria ipi, ya dini ama ya nchi?
Nenda zanzibar kale ukikamatwa utapata jibu watakapo kuhukumu. Kufunga ni lazima kwa kila muislamu sio hiari labda uwe mngojwa,Au jnasafiri,au mjamzito,au unanyonyesha.Na ikiisha ramadhani utalipiza zile siku usizo funga.
 
Mkuu nakushukuru sana kwa uzi wako huu.Nilichangia kidogo kwenye ile mada ya asubuhi iliyokuwa imeletwa na mdau mmoja.Kutokana na kufanya mambo nilipanga baadaye nilete hoja hii upya hapa.Naona umenirahisishia kazi.

Suala hili sio la kuchekea hata kidogo.Hili suala kama sio la kidini basi swali lake halikupaswa kuulizwa kwenye Baraza la Wawakilishi linaloendeshwa kwa kodi za Waislamu, Wakiristu na Wapagani.Hatujawahi kuona Wakiristu hata siku moja huko Zanzibar nao wakataka kauli ya Serikali juu ya taratibu za Kwaresima au Noel zitakavyokuwa. Suala la dini ni suala la Muungano.SMZ isitake kujificha kwenye kisingizio kuwa bara hawahusiki katika jambo hili ili kukwepa nondo wanazovurumishiwa.Tukiongelea Katiba ya Muungano tunaongelea Bara na Zanzibar.Na kwa vile Katiba ya Muungano imetamka wazi wazi kuwa Tanzania ni nchi isiyokuwa na dini maana yake Suala hilo ni binding hadi Zanzibar na mipaka yake yote.Haiwezekani suala litamkwe Kikatiba katika Jamhuri kisha liwahusu Wabara pekee.

Jambo la pili ni athari za kiuchumi zitokanayo ni kukataza watu kula hadharani.Kuna watu wana biashara za kupika chakula kama mama Ntilie.Wapo wanaofanyia shughuli zao ndani na wengine chini ya miti tu. Wanauza chakula mchana na usiku.Unapokataza watu wasile hadharani wapikaji kama hao Wa chini ya miti unataka wakishawauzia wateja wao chakula hao wateja wakakodi sehemu za kwenda kulia chakula? Unapokataza watu wasile hadharani unataka hao mama Ntilie wakakodi "_Fremu" za biashara ili wateja wao wawafuate huko? Unapokataza watu wasile hadharani unataka wauza Ice cream, Karanga, Bisi, wauza maji barabarani, wauza maandazi na kadhalika waende wakakodi Fremu? Kwa mtiririko huo huo ni dhahiri vipato vyao vitaathirika sana kipindi chote cha mfungo.Sote tunajua shule za msingi na sekondari zitafunguliwa mwezi Julai na hivi wanafunzi wanaporudi mashuleni wanahitaji kurudi na pesa au kununuliwa mahitaji kadhaa.Je, wazazi Wa wanafunzi wanaojipatia vipato vyao kw kufanya biashara ndogo ndogo katika mazingira kama niliyoyaeleza hapo juu SMZ inataka hao watu wakose kipato na hivi hao watoto wao wafukuzwe shule au washindwe kurejea masomoni kwa wakati?

Hao wawakilishi na mawaziri Wa SMZ wanaosisitiza ban ya watu kutokula hadharani wengi wao wamewekeza huku bara.Wana hoteli na migahawa kibao huku.Waunguja na Wapemba wengi wana Maduka huku Bara.Wanauza Biskuti, maandazi.Wana Bakery huku.Kwa ufupi vitega uchumi vyao kibao viko huku.Kwa hiyo wanapopiga ban ya watu kujilia hadharani wakati Wa mfungo wao bado wana uhakika huku mchana biashara zao zitakuwa zinaendelea vizuri.Wana uhakika wakiristu na wapagani Wa Bara wakati Wa mchana watanunua bidhaa zao hadharani bila kujificha kujificha.

Jambo la mwisho ni utetezi unaotolewa juu ya hili katazo.Eti ni utamaduni Wa Kizanzibari Wa muda mrefu.Utamaduni gani gani huo unaokuwa juu ya Katiba ya nchi? Eti ni suala la kiimani. Ni Mungu gani huyo anahalalisha wewe ukisali wengine wateseke? Mungu gani anakubali wewe ukisali wengine wajikunyate kunyate? Kwani hiyo imekuwa Bendera ya Taifa kwamba ikishushwa au kupandishwa sharti kila mtu asimame? Imani hiyo ni Wimbo Wa Taifa kwamba ukiimbwa basi kila mtu atulie? Mungu gani asubuhi anakataza watu asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni watu wasile hadharani ila baada ya hapo watu wale tu kwa kadri wapendavyo nje ya Nyumba, vibarazani, barabarani na sehemu zinginezo? Waislamu hatuwasemi vibaya ila munahitaji kuipa uhuisho baadhi ya mafundisho yenu.Dunia inawaacha.
wakuu mbona swala dogo linawatoa povu sana??????
hamjalielewa tangazo hakuna mtu kakatazwa kula wewe nunua msosi wako tafuta sehemu ya stara kisha kula utakavyo kisichotakiwa ni kula hadharani
 
Ivi tanzania bara na visiwani ni nchi ya dini au watanzania ndio wana dini msipende kubaka sheria za nchi.
 
wanabahati mi sipo huko
yaan ugali nimetafuta mimi, kwa jasho langu bila kusaidiwa na mtu, halafu wanipangie pa kula!!

yaan hilo kitu hakina logic kabsa.
Mkuu yaelekea unapenda san ugali,yaani katika vyakula vyote umetaja ugali tu😀
 
Acha ujinga wazanzibar hawapangiwi cha kufanya
Tofautisha wazanzibar na waisilamu wa Zanzibar. Sio wazanzibar wote ni waisilamu hivyo kutangazia umma kuwa hawawezi kula hadharani huo ni upuuzi
 
Hiyo funga ya kulazimishana naona ni maigizo tu mwisho wa siku kila mtu atasimama na nafsi yake siku ya hukumu
 
Hivi nikiwa nakula zangu kitimoto full futa mikononi, yani nakula hadi shavu limeloa futa futani, watanikamata kweli au wataogopa futa la kitimoto
Hakuna watu ninao wadharau kama watu wanaokula nguruwe

Kama unaweza kumla nguruwe basi hata fisi na kunguru hutoshindwa kuwala

Nguruwe ni scavenger kama kunguru na fisi
 
Watu kibao huwa wanagonga misosi vizuri tu ndani mwao. Hii ya kufunga Hotels mchana ni changa la macho na sanasana kuwatesa waksristu, wageni na waislamu wagonjwa ambao hali yao ya afya haiwaruhusu kufunga
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom