Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Zanzibar: Watakaokula mchana hadharani Ramadhani kukiona

Status
Not open for further replies.
Wewe umefunga.... Mwenzio anakula inakuuma nini...?? Hivi hawa ndugu zetu kama wana wakristo wanaishi nao watawaruhusu kula kweli? Au ndio ukiajiliwa au kuishi na muislam lazima ufate matakwa yake ya kidini...
Unakosea unaposema matakwa ya kiislam. Je matakwa ya kiislam ni kufunga tu? Je wametakiwa kwenda msikitini kwenda Makkah n.k?
 
Hivi wewe ukiwa umefunga nami nakula chakula changu hadharani inakuuma nini....!!?? Hivi ina maana wakristo huwa hatufungi?? Mbona tunaishi na nyie vizuri...
Hata kama mfanyakazi wako wa ndani kama siyo muislam mpe uhuru ale kwa muda wake... Wewe uliyefunga uko na Mungu wako... Kumnyima uhuru mwenzio kisa umefunga hain maana... Na mfungo wako ni batiri...
Umeambiwa kula hadharani sio mfanyakazi wa ndani asile kwanini unakuza jambo?
 
Kwani wamelazimishwa kufunga au wameombwa au kutakiwa kutokula hadharani? Kumbuka kutokula hadharani wakati wa mchana haimzuii mtu kula nyumbani kwake au mahotel yatakayokuwa wazi.
Mbona wakati wa kufungua futari zenu mnakula hadharani hatuwabughudhi.Huko ni kupungukiwa imani.Unapokuwa umefunga vishawishi ni vingi hata warembo ukutanao nao nishida.Tatizo mnaangalia upande mmoja ila ipo siku mtaujua ukweli nao utawaweka huru na mtakuwa huru kweli kweli.
Yesu alipelekewa chakula kujaribiwa akiwa amefunga hakumuuzi mtu bali alijibu kwa hekima kuwa mtuhataishi kwa mkate tu bali kwa neno litokalo kwa Mungu.
Jifunzeni kutokuwakwaza wengine.
 
Huu ni ubaguzi wa wazi wazi
Over!
Of course ni ubaguzi lkn unavumilika kutokana na mazingira kwa mfano kuna nchi ambazo zina wakristo wengi zaidi kuliko waislam maofisi ya serikali hayaitambui IDD lkn yanaitambua Xmas ukiwa muislam kuomba kupumzika siku ya IDD ni kwa barua kwa sab sio Holiday ya kitaifa. Wazungu wanalazimika kuvaa hijab nchi za kiarab japo sio sheria. Tuvumiliane tu.
 
Karibu yaheee sie twasubiri futar tu na eid.mambo mengine utajua mwenyewee
Yaheee nakuja huko....haya mambo ya kushinda njaa na pesa ninayo mfukoni siwezi mie amii....naja huko...mambo yenyewe ya kupigana NJUKUTI SIWEZI MIE...NAJA ami
 
Mbona wakati wa kufungua futari zenu mnakula hadharani hatuwabughudhi.Huko ni kupungukiwa imani.Unapokuwa umefunga vishawishi ni vingi hata warembo ukutanao nao nishida.Tatizo mnaangalia upande mmoja ila ipo siku mtaujua ukweli nao utawaweka huru na mtakuwa huru kweli kweli.
Yesu alipelekewa chakula kujaribiwa akiwa amefunga hakumuuzi mtu bali alijibu kwa hekima kuwa mtuhataishi kwa mkate tu bali kwa neno litokalo kwa Mungu.
Jifunzeni kutokuwakwaza wengine.
Kwani unapata tatizo gani ukilia ndani mchana kwa mwezi mmoja kwa mwaka? Mbona tunavumiliana mengi tu kwa mfano kutokupiga kelele makanisani au misikitini wakati waumini wako ndani wanaabudu kupisha misafara au maandamano ya kidini ikiwemo ya mazishi n.k.
 
Zanzibar ni kisiwa hatari Sana, siipendi ccm ila Kwa kuibana Zanzibar na kuikalia Kwa mabavu ipo sawa kabisa.
Leo hii Zanzibar ikiachwa kuwa taifa huru pasipo muungano na Tanganyika,Zanzibar haitakalika itakuwa Kituo cha magaidi.
Lakini Zanzibar inalipiza kimya kimya kwa kuihujumu Bara ikiwepo kuwanyanyasa Wabara walioko Zanzibar. Yaani kila watu wanasamehe jasho lao na kurudi Bara
 
Kilichoniacha hoi kwenye hilo tangazo ni kile kitendo cha kulazimisha waisilamu wote wafunge. Kama mtu anataka kufunga atafunga kwa hiari yake na sio kwa kulazimishwa. Inaonekana huko kufunga walio wengi hawatilii maanani ila ni mpaka itumike nguvu ya serekali kuhakikisha watu wanafunga. Sasa najiuliza ukikuta mtu anakula hadharani akipelekwa mahakamani anafungwa kwa sheria ipi, ya dini ama ya nchi?
 
Kwani unapata tatizo gani ukilia ndani mchana kwa mwezi mmoja kwa mwaka? Mbona tunavumiliana mengi tu kwa mfano kutokupiga kelele makanisani au misikitini wakati waumini wako ndani wanaabudu kupisha misafara au maandamano ya kidini ikiwemo ya mazishi n.k.
Mbona wakati wa kufuturu tunawaona mnatandika mikeka nje mnakula hadharani hamjifungii ndani harafu mnataka wengine wajifungie wanapokula mnapokuwa hamjafungua nyie.Mnajuaje kuwa mnapofungua na wao wanakuwa wamefunga.In short kwa wakristo kufunga hakuna muda maalumu mtu aweza kufunga muda na wakati wowote kutegemea na hitaji lake kwa Mungu.Sijaona hoja hapo.
 
Jamani walichokataza ni kula hadharani ,lakini ukiwa ndani ni ruksa,pale Maisara ukumbi wa CCM na ukumbi wa Magereza na hata hotel kubwa bado hutoa huduma za vyakula na hii sio kitu kipya kwa Zanzibar kipo tokea enzi za Karume tena siku hizi ni nafuu zaidi kuliko miaka ya nyuma,tutake au tusitake Zanzibar ni kama nchi ya Kiislamu ,90.9% ni waisalamu.
Hata kwa Raju utakuta watu wanpombeka mchana kweupeee, ilausitoke na chupa lako nje hapo unatafuta ugomvi. Lazima kuheshimu mila na tamaduni za jamii husika. Kumbuka hawakatazi dini nyingine kula ila kuna maeneo maalum kama mahoteli ya kitalii na majumbani mwenu. Ila kama mkristo umepanga nyumba ya ustaadh itabidi ushindie soda na biskuti maana ukikarangiza vitanukia mchana na ni kosa.
 
Mbona wakati wa kufuturu tunawaona mnatandika mikeka nje mnakula hadharani hamjifungii ndani harafu mnataka wengine wajifungie wanapokula mnapokuwa hamjafungua nyie.Mnajuaje kuwa mnapofungua na wao wanakuwa wamefunga.In short kwa wakristo kufunga hakuna muda maalumu mtu aweza kufunga muda na wakati wowote kutegemea na hitaji lake kwa Mungu.Sijaona hoja hapo.
Kuwa mvumilivu tu. Unadhani kila mtu anafurahishwa na kelele za adhana kutoka misikitini? Au kelele za kengele kutoka makanisani? Wengine ni wagonjwa hawapendi kelele lkn wanavumilia. Hii ndio demokrasia.
 
Kilichoniacha hoi kwenye hilo tangazo ni kile kitendo cha kulazimisha waisilamu wote wafunge. Kama mtu anataka kufunga atafunga kwa hiari yake na sio kwa kulazimishwa. Inaonekana huko kufunga walio wengi hawatilii maanani ila ni mpaka itumike nguvu ya serekali kuhakikisha watu wanafunga. Sasa najiuliza ukikuta mtu anakula hadharani akipelekwa mahakamani anafungwa kwa sheria ipi, ya dini ama ya nchi?
Kumbe nikifanya biashara ya Bar One inaelekea Italica sana Zanzibar.
 
Kuwa mstaarbu heshimu imani za watu . Kama wewe umeona waislam tu mimi niko mkoa fulani hapa nilikataliwa kupanga nyumba eti sababu tu ya imani yangu tena chaajabu mmiliki wa nyumba ni kiongozi wa wanakondoo.
Wewe hukatazwi kula ulichoambiwa usile hadharani muda wa mchana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom