Good qn, ingawa hujajibu swali langu.
Kwanza kabisa, nataka nikupe utofauti mdoogo na maana ya kufunga kikristo.
Sisi hatuna msimu/kipindi rasmi cha kufunga ingawa ninyi mnaifahamu "Kwaresma"
Pia hatukuwekewa Time limit kuwa mfungo ni wa masaa flan mpaka flan, kwa maana hiyo mtu anayeanza kufunga atafunga kwa masaa 12 (umezoeleka hivyo) na wakati huo huo akitubu na kuomba ama kuombea kitu flani cha muhimu sana, hata kesho ntaweza kujipanga na kufunga tena bila kutangaza ama kuonesha kunyong'onyea.
Kuna anayeweza kufunga kwa masaa zaidi ya hayo...
Musa alifunga siku 40, Yesu Kristo alifunga siku 40 nafikiri na Eliya ama Elisha pia.
Wakati wa mfungo huo hakuna kuamka usiku na kula chakula kwakuwa ni kulegeza swaum.