ZANZIBAR: Hatimaye House of Wonder Imepata mkandarasi, kutoka Oman

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,773
21,270
TZA Wonders-1.jpg

Hili jengo (pichani) Nyumba ya Maajabu (House of Wonder) ni sehemu ya urithi wa visiwa hivi vya Zanzibar, toka mkoloni alipong'olewa kuja mpaka miaka ya hivi karibuni jengo hilo limeingizia Zanzibar mapato mengi yatokanayo na utalii.

Miaka ya hivi karibuni jengo hilo lilibomoka na kuanguka hali iliyopelekea watu wengi kupata mshtuko kuwa, uenda ndiyo mwisho wa enzi ya uwepo kwake visiwani humo.

beit-pic-data.jpg


Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilijitahidi kutafuta mkandarasi wa kuliboresha na kulirejeshea uhai na hatimaye, kampuni kutoka uarabuni imefanikiwa kupata tenda ya kulirejesha.

Zabuni ya kazi ya marejesho ilitolewa mbele ya mheshimiwa Salem bin Muhammad Al Mahrouqi, waziri wa utalii zanzibar na mbele ya balozi mdogo wa Oman Zanzibar pia alikuwepo balozi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania nchini Oman na Katibu wa tume ya taifa ya elimu, Utamaduni na Sayansi.

Screenshot_2023_0215_084313.jpg


Mkataba huo ulitiwa saini na H.E. Eng Ibrahim bin Saeed Al Kharusi, katibu mdogo wa wizara ya turathi na utalii, na Mh. Simai Saeed, Waziri wa Utalii na mali kale Zanzibar.
 
Kazi hizo wanaziwezeaga wajerumani ,lakini kama jengo hilo walilijenga waarabu basi hao watalitendea haki

Ova
 
Jibu hoja ndugu, hii ni Tanzania, au hii tender ilikua ni non union matter?

haikupata contractor kutoka Tz?
Ukute mwarabu ana thamani zaidi zenjberi kuliko chogo wa bara.........kwa mwenye uelewa, hivi waarabu wana chogo au hawana?
 
Back
Top Bottom