Uingereza Yaipa Zanzibar Mkopo wa Sh.Tilioni 1 Kujenga Uwanja wa Ndege Pemba

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,128
49,850
Wadanganyika mnaitwa huku 🤪🤪
---
Serikali ya Zanzibar na Uingereza zimesaini makubaliano ya mkopo wa bei nafuu wa Euro 400 milioni sawa na Sh1.04 trilioni kwa ajili ya ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Pemba na zaidi ya kilometa 103 Unguja na Pemba.

Fedha hizo ambazo ni mkopo nafuu kutoka Uingereza, unapitia benki za Deutsche na Citibank kiasi ambacho kinatajwa kuwa kikubwa kuwahi kupokewa kwa Serikali hiyo tangu Mapinduzi.

Hafla ya kutia saini hiyo imefanyika leo Juni 20, 2023 katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Zanzibar kati ya Balozi wa Uingereza nchini Tanzania David Concar na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji wa saini hiyo, Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Zena Said amesema ni tukio kubwa la kihistoria kwa Zanzibar kugharamia miundombinu muhimu ya kimkakati kwa kiasi kikubwa cha fedha za namna hiyo.

“Hii itanufaisha uchumi wetu watu kutoka maeneo mbalimbali watakuja na kukuza utalii wetu,” amesema
Waziri wa Fedha na Mipango Dk Saada Mkuya amesema kwa mara ya kwanza Zanzibar kupata kiasi hicho kikubwa cha fedha za mkopo kwa mkupuo.

“Hii ni historia tunakwenda kuifungua Zanzibar katika miundombinu ya kuchumi kwa kujenga barabara za hapa Unguja na Uwanja wa ndege wa Pemba ambao utakuwa wa kimataifa,” alisema Dk Saada.

Naye Waziri wa Ujenzi, Mawasilianio na Uchukuzi, Dk Khalid Salum alisema safari hiyo imeanza muda mrefu tangu awamu zilizotangulia na mawaziri tofauti wa Awamu ya Nane hivyo kufikia hatua hiyo ni jambo la kupongeza.

“Zaidi ya kilomita 800 zinakwenda kujengwa hapa Unguja na Pemba hii haijawahi kutokea mara nyingi zinajengwa barabara zenye urefu wa kilometa 200, lakini mara hii tunajenga kilometa hizo tena kwa wakati mmoja,” alisema Dk Khalid.

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, David Concar alisema katika utekeleji wa mradi huo utafungua fursa za kiuchumi na kijamii kwa taifa na wananchi wa Zanzibar.

Alisema Serikali ya Uingereza itaendelea kushirikiana na Serikali za Tanzania na Zanzibar kuendelea kuitekeleza miradi mingine mikubwa ya kimkakati.

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom