Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera


[HASHTAG]#ZanzibarPolice[/HASHTAG] #corruption#Zanzibar [HASHTAG]#Tanzania[/HASHTAG] Although Zanzibar was a beautiful place to visit, officials were trying to take bribes from the moment we landed (like the Yellow Fever scammers in Arrivals, then the car hire scammers in the airport car-park). That may explain my frustration at the end of this video.

Although I had a valid ‘Foreigners Driving Permit’, OFFICER ALI here – of the Police Post in Mahonda – stopped us at his roadblock on the second day and demanded a $40 bribe to allow us to drive on. After a long debate, he pockets 60,000 Tanzanian Shillings (about $28) without a receipt – and still tries to shake my hand.

(For those commenting that we should not have paid, the other option was to wait there for TWO DAYS until after Eid, and then pay a court official!) The offence was not carrying my national driving license, even though I had already shown it to get the Zanzibar 'Driving Permit'.

But the money went straight into his pocket.

By Pete Taylor

Kwa mtindo huu wataipinga CUF na kuitafutia migogoro kwa gharama yoyote ile....wazungu sio wajinga bwana...naikumbuka MCC hapa.
 
Mwacheni Mwenzenu, Mna Uhakika alichukua zaidi ya Tsh 5000, Si Mnakumbuka, Mh. Magufuli alishasema Tsh 5000 ya Kupakia Kiatu rangi sio Rushwa?Na hata Kama amechukua Tsh 60,000 Unaweza Ukakuta wako 12, wenzake akaenda Kuwakatia Tsh. 5000 si atakuwa amesevu? Amakwali Hii Ndiyo Tanzania Ninayoitaka, Kwa Spidi Ninayokwenda nayo hii heeee!



Nimejaribu kushindwa kuamini lakini nimeshindwa,
 

Hii ni bahati mbaya tu mtu karecord na tusijifanye kumuona huyu askari kama criminal haya ni mambo yako kila dakika labda mtu anapokea rushwa kama sio askari mfanyakazi somewhere lazima tukubali ni shida kubwa halafu JPM aliongelea kuna siku kama jambo linakubalika tu huyu akienda mahakamani atashinda tu si clip ya JPM ipo kuwa pesa ya kupigia Kiwi tu labda tu kachukua alfu 60 Kiwi mwezi mzima maana alfu was ok. shame
 
Kwa mtindo huu wataipinga CUF na kuitafutia migogoro kwa gharama yoyote ile....wazungu sio wajinga bwana...naikumbuka MCC hapa.
Mhhh mkuu ulichoandika ndicho ulichokusudia? Nashindwa kuunga
 
Da yani bonge la aibuuu tanzania askari wetu amelizalilisha jeshi mnoo lugha hajui na mzungu amechukia yule mwanaume anaeendesha gari anamwambia mimi siwezi kuja tena zanzibar sasa utalii si ndio tunaufukuza jamani daaaa.
 
Da yani bonge la aibuuu tanzania askari wetu amelizalilisha jeshi mnoo lugha hajui na mzungu amechukia yule mwanaume anaeendesha gari anamwambia mimi siwezi kuja tena zanzibar sasa utalii si ndio tunaufukuza jamani daaaa.


Ni kweli kabisa hii ni aibu na reflexion yake kwa viongozi wetu wanapotembelea nchi hizo sijui inakuwaje, kuna baadhi ya vitendo ukifikiria wakati mwingine unaona hata ibilisi anasingiziwa.

Ingekuwa amri yangu watu kama hawa nisingewaruhusu kuja kwenye nyumba za ibada maana hawaji kujutia na kutubu dhambi zao bali kujifariji ili waendelee kufanya uhalifu

Inakuwaje pale tunayemtegemea kuzuia uhalifu anakuwa mhalifu namba moja, binafsi watu waliokula viapo na kuvichezea ningeona wawekwe vizuizini ili viapo vipate heshima yake
 
Huyo askari aliyefanya hapo ni mmoja tu,ingekua kila askari anafanya hivyohivyo Kilio kingekua kikubwa mno,siungi mkono alichofanya ,ila mnyonge mnyongeni lkn haki yake mumupe.

Wewe unaishi Tanzania kweli? Jeshi la Police linahitaji kufanyiwa overhauling. Yaani police wote waliopo waachishwe kazi tuanze upya. Kama Rais wetu anataka kusaidia Watanzania, basi aelekeze pia nguvu kubwa kwa jeshi la police.

Juzi nimesikia story ya jamaa amepigwa na jambazi linaitwa Scorpion huko Buguruni, limemchoma visu hadharani, baada ya jamaa kupoteza fahamu, likamvutia barabarani ili agongwe na magari, kisha likamnyofoa macho. Jamaa alipopata fahamu macho hana. Wakati haya yote yanafanyika, watu wanaona na wanajua ni Scorpion yuko kazini. Hawathubutu kuingilia kwa kuwa wanajua ukiingilia Scorpion atakushughulikia na police hawana msaada wowote. Yaani kila mtu anajua Scorpion anaibia watu, anaua, anatoa watu macho lakini bado yuko free kuendelea na uhalifu. Na police wapo. Police ni majambazi.
 
Ilishatoka amri wapokee ya kung'arisha viatu toka kwenye busara za mkuu. Rushwa ni rushwa na hakika rushwa ni MBAYA SANA na hili ni tatizo la kimfumo. Anayefanya mzaha na suala hili hakika hatutakii mema. Hivi kila mtoa huduma katika nafasi yake achukue rushwa au ukihitajika kutoa ya kubrashi viatu kwa kila askari unayemkuta hii nchi itakalika? Hii ni aibu kubwa kwa taifa, aibu kubwa, kubwa, kubwa. Halitabiri mazuri pia kwa nchi ambayo sehemu kubwa ya mapato yake hutegemea utalii.

Ni majuzi tu hapa tumeona maandamano kwenye ubalozi wa Tz kule USA, raia ya kule wakipinga vitendi vya rushwa vilivyowakumba wenzao wakiwa hapa nchini. Lakini serikali ya matukio inaona ni jambi la kawaida tu na kwamba wanaonajisi uchumi wa taifa wapo bandarini tu!
 
Uonevu unaofanywa na traffic haukubaliki, hawajui sheria, wanapenda rushwa, wana mtandao wa rushwa mpaka kwa mabosi zao, hata ukifanyiwa uonevu usitegemee kwenda kulalamika ngazi ya juu hawa lao moja.

Jumamosi ndio siku yao hatari ukiingia mikononi mwao ni mawili tu utowe rushwa au upewe notification ukalipe TRA chaguo ni lako.

Tunaochukia rushwa sisi ni wahanga wakubwa wa uonevu wa traffic, maana watowa rushwa wote wakisimamishwa tu uandaa rushwa na kumfinyia traffic yanaisha.

Kazi kwetu tunaojifanya wajuaji kwanza hatushuki kwenye gari, traffic akija haoni dalili za mtonyo akikuomba leseni anakuandikia faini halafu ndio anakusomea makosa ya uongo, Mungu anawaona mlaaniwe na Mungu awachape kabisa wala rushwa wakubwa ninyi.

Pendekezo: Kikosi Cha traffic kivunjwe waletwe JWTZ wavae sare za traffic hawa ni waadilifu.

Traffic wengi hawana hata chembe ya uelewa wa sheria za barabani, hivi kuna dhambi gani ykinuelimisha driver fanya hivi usifanye vile?

Kuna vile vibanda vyao vipo kwenye kona mbalimbali za mji wenyewe huviita sijui dolia ngapi hapo ndipo genge la dhulma na uonevu lilipo.

Jamani tumewachoka hata sisi tuna maisha magumu, ni nani aliwadanganya kuwa na gari ndio una pesa za kugawa.

Cha msingi mkumbuke zile notification mnazotubambikia makosa zina majina yenu namba zenu za uaskari sasa tutaanza kuwaroga wala rushwa wote mgeuke vichaa, msidhani pesa zinaokotwa.

Polisi ni watu wa ajabu sana kila mwezi Polisi wote wanapewa posho ya shilling laki tatu bila kujari cheo na mshahara wao uko palepale, je hamjisikii dhambi kuja kuwaonea watu wanaopokea take home saraly ya laki moja na nusu kwa mwezi.

Hivi mmeshawahi nyinyi wala rushwa kukaa na kujiuliza ni kwa nini tangu muanze kula rushwa mpaka leo hamna maendeleo? mna laana hamna baraka za Mungu kwa dhulma zenu zilizokithiri.

Tumewachokaaaa.
Ujumbe umewafikia nilishawai kugongwa kwa nyuma traffic kahongwa,msajili Wa kesi kahongwa adi hakimu kaongwa nilivyokundua inshu kilichofuata walijuta wote na kunipigia magoti na mpaka mahakama kinondoni wahendesha mastaka walihamishiwa kwenye ukumbi sababu ya kesi yangu walinidharau eti mwanamke hakimu mzembe jina kapuni kisa mchaga mwenzake .najua wanaikumbuka kesi hii
 
Jamani mkuu wetu wa nchi Mtakatifu sana alisema wanatafuta hela ya kiwi na mkumbuke yule ni amiri jeshi mkuu so kauli yake kwa jeshi lolote ni amri so jamaa katekeleza amri sahihi ya mkuu wa jeshi!
 
Nimejaribu kuitizama hii clip kwa umakini Mkubwa....

Nimegundua Askari wetu hakuomba Rushwa isipikuwa hawa jamaa walidhamilia kumpa pesa na kutegesha mapema ili ionekane Askari anaomba Rushwa....Sijaona sehemu yoyote akisema wampe Hiyo pesa......Askari hana kosa
 
Back
Top Bottom