Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Poa kuna wazee was kufukuzia boda boda hao nae VP, njaa mbaya jaman
 
Hata Singida Iguguno na mzani niliwakuta wapo wamejaa tele,
 
Daah trafic wameshawahi kunifanyia hivyo lakini namuonea huruma huyo mtu
 
Kwa Muda mrefu tulikuwa tunajua Polisi wa usalama barabarani ndio wenye jukumu la kusimamia sheria za barabarani,na ndio maana hata mavazi yao ni meupe ili madereva wawaone kwa urahisi.Lakini katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia karibu Polisi wote hata wale tito ndio wamekuwa wakiongoza magari au kuyakagua ilihali wakiwa hawajui hata sharia za barabarani.mimi nauliza wadau jambo hili wanalifanya kwa nia njema au kuna mabadiliko katika katika taratibu za kazi zao?

Nawasilisha
Tito ni nani?.
 
Kwa Muda mrefu tulikuwa tunajua Polisi wa usalama barabarani ndio wenye jukumu la kusimamia sheria za barabarani,na ndio maana hata mavazi yao ni meupe ili madereva wawaone kwa urahisi.Lakini katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia karibu Polisi wote hata wale tito ndio wamekuwa wakiongoza magari au kuyakagua ilihali wakiwa hawajui hata sharia za barabarani.mimi nauliza wadau jambo hili wanalifanya kwa nia njema au kuna mabadiliko katika katika taratibu za kazi zao?

Nawasilisha
Uonevu unaofanywa na traffic haukubaliki, hawajui sheria, wanapenda rushwa, wana mtandao wa rushwa mpaka kwa mabosi zao, hata ukifanyiwa uonevu usitegemee kwenda kulalamika ngazi ya juu hawa lao moja.

Jumamosi ndio siku yao hatari ukiingia mikononi mwao ni mawili tu utowe rushwa au upewe notification ukalipe TRA chaguo ni lako.

Tunaochukia rushwa sisi ni wahanga wakubwa wa uonevu wa traffic, maana watowa rushwa wote wakisimamishwa tu uandaa rushwa na kumfinyia traffic yanaisha.

Kazi kwetu tunaojifanya wajuaji kwanza hatushuki kwenye gari, traffic akija haoni dalili za mtonyo akikuomba leseni anakuandikia faini halafu ndio anakusomea makosa ya uongo, Mungu anawaona mlaaniwe na Mungu awachape kabisa wala rushwa wakubwa ninyi.

Pendekezo: Kikosi Cha traffic kivunjwe waletwe JWTZ wavae sare za traffic hawa ni waadilifu.

Traffic wengi hawana hata chembe ya uelewa wa sheria za barabani, hivi kuna dhambi gani ykinuelimisha driver fanya hivi usifanye vile?

Kuna vile vibanda vyao vipo kwenye kona mbalimbali za mji wenyewe huviita sijui dolia ngapi hapo ndipo genge la dhulma na uonevu lilipo.

Jamani tumewachoka hata sisi tuna maisha magumu, ni nani aliwadanganya kuwa na gari ndio una pesa za kugawa.

Cha msingi mkumbuke zile notification mnazotubambikia makosa zina majina yenu namba zenu za uaskari sasa tutaanza kuwaroga wala rushwa wote mgeuke vichaa, msidhani pesa zinaokotwa.

Polisi ni watu wa ajabu sana kila mwezi Polisi wote wanapewa posho ya shilling laki tatu bila kujari cheo na mshahara wao uko palepale, je hamjisikii dhambi kuja kuwaonea watu wanaopokea take home saraly ya laki moja na nusu kwa mwezi.

Hivi mmeshawahi nyinyi wala rushwa kukaa na kujiuliza ni kwa nini tangu muanze kula rushwa mpaka leo hamna maendeleo? mna laana hamna baraka za Mungu kwa dhulma zenu zilizokithiri.

Tumewachokaaaa.
 
Matola nimejikuta nacheka hadi wife anashangaa?
Usicheke mimi namaanisha, hawa huna uwezo wa kuwafanya lolote kwa sababu uhalifu wao una baraka kutoka kwa wakubwa zao.

Sasa kwakuwa majina yao tunayo kwenye notifications wanazotumbambikia hakuna namna nyingine ni kuwapiga kipapai tu mpaka tutakapoheshimiana.

Mtu anayeona mshahara wa Upolisi haumtoshi aache kazi wapo vijana wengi tu hawana kazi.
 
Hii ndo ile alisema ya kuburashia viatu au?
 
Ni mkoa gan au barabara gan mkuu, tukio la mtaa mmoja lisiwe la nchi nzima
Aisee upo nchi gani??? Siku hizi safiri barabara ya kati hadi Dar wapo waliovalia kiraia na kujificha na wale wenye mavazi ambayo sio rasmi kwa Polisi wa usalama barabarani! Unakuta mwingine kavaa vazi la FFU utadhani anatuliza fujo barabarani!
Dhana hapo ni makusanyo kwani na wao siku hizi ni Traei, japo haya makusanyo hayamfikii kamishna mkuu wa traei.
 
Ni mkoa gan au barabara gan mkuu, tukio la mtaa mmoja lisiwe la nchi nzima
Watu wengine mnashangaza sana, sasa wewe kama unaishi kijijini kero za traffic utazijulia wapi?

Maana kama unaishi mijini hata kama huna gari yako ukipanda daladala utaona tu manyanyaso wanayofanyiwa madereva na hawa wapenda rushwa.
 
Back
Top Bottom