Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Zanzibar: Askari Polisi ajidhalilisha, apokea rushwa mbele ya Camera

Jeshi pendwa kwa kutuliza mikutano ya hadhara na maandamano ya kisiasa
 
Huyu mleta uzi lazima AKAMATWE kwa kulidhalilisha jeshi la polisi visiwani Zanzibar. ARREST HIM!
Hiyo video ni ya kutunga?wafanyie kazi udhaifu wa watu wao,hiyo ni changamoto inetolewa na ujumbe ulionyooka kuwa rushwa inaliwa.
Kwa akili kama zako hata mtu akiona uhalifu hawezi kuliambia jeshi la polisi maana watamuuliza"ulijuaje',ilijuwaje ukaona,badala ya kuchukua taarifa na kufanyia kazi,unamuumiza mtoa taarifa.
 
Am just saying lakini...don't misquote me...Mimi ningekuwa RPC wake huyu askari simfukuzi kazi hata kidogo!!!!
 
Nafikiri amekasirika kwa kitendo cha huyo askari kuchukua hizo pesa halafu anataka kutoa mkono wa shukrani.

Pathetic!


Kuna kila sababu kuwa na masomo ya uadilifu kwenye mtaala wetu, unakumbuka kuna yule askari mwingine alipwe lift na waxungu wa kike kama sijakosea akaanza kubwabwaja akadhani wanamfurahia kumbe wanamchora tena nadhani ni hukohuko kwenye marashi ya zao adimu
 
Simlaumu huyu polisi sababu mtukufu malaika aliwaruhusu wapokee rushwa ili wagharamie kupiga kiwi viatu vyao
 
No hana shida alorecord hii ishu haiwez kua kbwa ka ya Jerry M. Sema afande ndo baaas tena[emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Anasema "You are educated man" [emoji38] [emoji38] [emoji38] [emoji87] [emoji87] [emoji87]
Hahahahaaaa Mr educated man!!! Hata mutoto ndogo ya muzungu ni educated! Si inaongea kizungu!halafu muzungu yenyewe ako na pesa kwa mkono! Lazima ulainishe lugha mazee
 
You spoil our holiday and tryna shake hand with me?
Waziri mwenye dhamana ya utalii na maliasili kuhusiana tozo ya Vat katika utalii alishasema "hatutaki watalii maskini"

Sasa tsh 60,000 tu kwa afande Alli mnachonga sana
 
Waliruhusiwa kupokea 5,000 za soda yeye amezidisha. Asali haifahamu kuchovya kidogo !!!!!

Swali ni je 5,000 walioruhusiwa kupokea si rushwa?
 
Uonevu unaofanywa na traffic haukubaliki, hawajui sheria, wanapenda rushwa, wana mtandao wa rushwa mpaka kwa mabosi zao, hata ukifanyiwa uonevu usitegemee kwenda kulalamika ngazi ya juu hawa lao moja.

Jumamosi ndio siku yao hatari ukiingia mikononi mwao ni mawili tu utowe rushwa au upewe notification ukalipe TRA chaguo ni lako.

Tunaochukia rushwa sisi ni wahanga wakubwa wa uonevu wa traffic, maana watowa rushwa wote wakisimamishwa tu uandaa rushwa na kumfinyia traffic yanaisha.

Kazi kwetu tunaojifanya wajuaji kwanza hatushuki kwenye gari, traffic akija haoni dalili za mtonyo akikuomba leseni anakuandikia faini halafu ndio anakusomea makosa ya uongo, Mungu anawaona mlaaniwe na Mungu awachape kabisa wala rushwa wakubwa ninyi.

Pendekezo: Kikosi Cha traffic kivunjwe waletwe JWTZ wavae sare za traffic hawa ni waadilifu.

Traffic wengi hawana hata chembe ya uelewa wa sheria za barabani, hivi kuna dhambi gani ykinuelimisha driver fanya hivi usifanye vile?

Kuna vile vibanda vyao vipo kwenye kona mbalimbali za mji wenyewe huviita sijui dolia ngapi hapo ndipo genge la dhulma na uonevu lilipo.

Jamani tumewachoka hata sisi tuna maisha magumu, ni nani aliwadanganya kuwa na gari ndio una pesa za kugawa.

Cha msingi mkumbuke zile notification mnazotubambikia makosa zina majina yenu namba zenu za uaskari sasa tutaanza kuwaroga wala rushwa wote mgeuke vichaa, msidhani pesa zinaokotwa.

Polisi ni watu wa ajabu sana kila mwezi Polisi wote wanapewa posho ya shilling laki tatu bila kujari cheo na mshahara wao uko palepale, je hamjisikii dhambi kuja kuwaonea watu wanaopokea take home saraly ya laki moja na nusu kwa mwezi.

Hivi mmeshawahi nyinyi wala rushwa kukaa na kujiuliza ni kwa nini tangu muanze kula rushwa mpaka leo hamna maendeleo? mna laana hamna baraka za Mungu kwa dhulma zenu zilizokithiri.

Tumewachokaaaa.
Peleka malalamiko yako moja kwa moja juu kabisa kwa RPC isiwe bosi aliyeko kitengo cha traffic kwa DSM mwone mtu anaitwa Awadh Mkuu wa traffic kanda maalum hakika huyo askari atawajibishwa na kukomesha kabisa tabia hii.

Naamini ni kweli madereva mnapata sana kero inayowaumiza pole sana Mkuu
 
Waziri mwenye dhamana ya utalii na maliasili kuhusiana tozo ya Vat katika utalii alishasema "hatutaki watalii maskini"

Sasa tsh 60,000 tu kwa afande Alli mnachonga sana
Point. ''HATUTAKI WATALII MASKINI.''
 
Back
Top Bottom