Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

wazenj ni watu wa ajabu sana,wao Zanzibar ni yao Tanganyika ni yetu,mademu zao ni wao ,mademu wa Tanganyika wa wote......hii haikubaliki.kama wanataka haki hiyo sharti wawe na wajibu wa kukubali watanganyika nao kuwa na haki zao za msingi zenj na sio kupigwa risasi,kuchomemewa makanisa na mabar.

Punguza povu, mchakato wa katiba unaendelea. Maoni ya Wazanzibar ni waachiwe wapumuwe ikimaanisha kutoka kabisa katika muungano. Idadi ya wajumbe kwenye tume ya katiba ni sawa ZNZ na Tanganyika. Washawishini viongozi wa pande zote wakubali maoni ya raia ili kadhia hii iishe.
 
High time na nyie mkomae. I agree, rais atoke zbar. Na kama kweli jamhuri ni ya muungano basi na asijitokeze mtu bara wa ccm kucompete. What an easy way to kick nyinyiemu's butt?
 
Punguza povu, mchakato wa katiba unaendelea. Maoni ya Wazanzibar ni waachiwe wapumuwe ikimaanisha kutoka kabisa katika muungano. Idadi ya wajumbe kwenye tume ya katiba ni sawa ZNZ na Tanganyika. Washawishini viongozi wa pande zote wakubali maoni ya raia ili kadhia hii iishe.
Sasa kama mnaona tunawabana pumzi na hamtutaki,ya nn kulilia urais wa Muungano?
 
si ndo' nyie mnaopinga muungano? leo mnataka uraisi huku kwetu kumbe muungano mnaupenda ila mnaleta mbwembwe tu! tabia zenu reminds me demu wangu wa zamani tukigombana anasema i hate u ila kesho unaona sms i miss u baby!
 
Pelekeni maoni yenu katika Tume ya Katiba muda bado upo, hamjachelewa.
 
Sasa kama mnaona tunawabana pumzi na hamtutaki,ya nn kulilia urais wa Muungano?

hatutaki dhaifu wa tatu! Wa kwanza alikuwa mwinyi, wa pili jk, na wa tatu tena. Mbona tutakula mchanga maana hata nyasi zimeisha kwa namna magogo yanavyokatwa na mito inakauka.
 
Sasa kama mnaona tunawabana pumzi na hamtutaki,ya nn kulilia urais wa Muungano?

Kuna options nying sana kaka:

1) Waachiwe wapumuwe i.i vunja muungano. Wazanzibar wameshatoa mapendekezo yao na baadhi ya wa Tanganyika

2) Fanya mabadiliko makubwa kiutawala i.e Uongozi ugaiwe kwa formular maalum kulingana na misingi ya muungano ilivyokuwa.

3) Hutaki 1 and 2 above, kero za muungano na manungúniko havitakwisha.
 
Jamani tuna vyama vingi

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Naungana na wewe maana by that time tutakuwa na Tanganyika yetu na sisi!Huyo Rais wa Muungano kazi yake itakuwa ni kukata utepe tu kwenye ufunguzi wa miradi ya serikali kama anavyofanya makamu wa rais sasa hivi.

Hata mara zote akitokea Zanzibar wabara hatutakuwa na shida juu ya hilo.
 
Kuwa na rais wa JMT kutoka zenji ni ajabu la ulimwengu, kama kuna mtu kutoka Tanganyika atampigia kura mzenji awe rais basi dunia itakuwa sasa imegota ukingoni
 
  • Mnataka muachwe huru.....wakati huo huo, rais wa Muungano atoke Zanzbar, viwili hivi vinawezekanaje kwa wakati mmoja?
  • Kwakuwa Ali Hassan Mwinyi alishakuwa Rais wa Jamuhuri akitokea Zanzbar, nadhani sasa ni wakati wa rais wa Zanzibar naye atokee Bara....kama urais ni kwa zamu.
  • Na tabia ya ......changu chakwangu, chetu changu itawaisha lini Waznzbar?
  • Lini Mtanzania Bara ataruhusiwa kumiliki ardhi huko, kama wazanbar wanavyo miliki ardhi bara?
 
Mtu anayefaa kuwa Rais wetu ni yule mwenye uwezo wa kuiheshimu, kuilinda na kuitetea Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa moyo wake wote, akili zake zote na nguvu zake zote bila kujali anatoka Tanganyika au Zanzibar!
 
Marekani yenye nchi 50 na marais zaidi ya 40 kuna state zimetoa marais 7 na kuna dtate zaidi ya 5 hazijawahi kutoa rais. Wanajali zaidi uwezo na kukubalika. Urais wa nchi sio kama uongozi wa jumuia kama afrika mashariki au UN au AU ambapo wanapokezena kwa vile jakuna popular vote na huna executive power mf kuamuru vita zaidi ya sifa ya kuitwa kwenye mikutano ya kimataifa kuwazungumzia wenzako na kutatua mgogoro wa kisiasa. Urais wa nchi ni kwa popular vote lazima uwe umekubalika na wapiga kura na sio umewekwa kwa vile ni zamu yenu. Wapiga kura humchagua mtu wanaueona anafaa. Ili kumpata rais lazima ajijenvee imani kwa wapiga kura kuwa anaweza.
 
Ni kweli ifikapo 2015 Tanzania kwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania itakuwa na uchaguzi mkuu. Ni jambo la busara kuanzia sasa kujadili agenda mbalimbali zihusuzo namna mzuri ya kufanya uchaguzi wetu, namna ya kumpata Mgombea bora wa nafasi ya Uraisi. Lakini wakati tukijiandaa kufanya uchaguzi huu lazima tujipange vizuri kwa kuorodhesha Agenda zetu kabla hatujafika kupendekeza jina la mgombea na sehemu anayotoka.
  1. Agenda ya kwanza ingekuwa " tunachangamoto gani"
  2. Ni nani miungoni mwetu sisi sote wananchi wa Tanzania atakayeweza kutuongoza katika kuyafikia malengo yetu kitaifa.
  3. Hoja ya mahali anapotoka Mgombea wa Uraisi ni hoja, ndiyo, lakini haina maana hivyo haiwezi kuwekwa mbele ya hoja zinazopaswa kuwa ndiyo mwongozo wa kutufikisha kwenye lengo. Hoja hiyo inatupeleka kwenye ubaguzi. Tunachohitaji kama watanzania ni maendeleo sio kutambuana asili zetu kama wazanzibar, wapemba wasukuma au wanyakyusa au wahaya. Uzanzibar au Ubara hautatuongezea shibe wala heshima. Kiongozi bora ataleta maendeleo kwa watanzania wote bila kujali anakotoka mtu wala kabila lake, mkoa
  4. Mtanzania mwenzetu huyu ajue kuwa watanzania hatuhitaji Uzanzibar wala Utanzania bara wake ili kumchagua kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapana! Tunahitaji sifa zake kama kiongozi. Kama kuna wanasiasa wanataka kiongozi achaguliwe kwa misingi ya kuangalia anakotoka hawa tuwakatae pasipo kuwaonea haya kwa sababu watatufanya tuchague kiongozi asiye na sifa za uongozi. Tutapata madhara makubwa kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni. Watanzania karibu wote watakuwa mashahidi wangu nikisema" Watanzania tumepita vipindi tofautitofauti vya uongozi. Kuna kipindi tulipita uchumi wa nchi ulikuwa mbaya sana. Wananchi walioiuzia serikali huduma mbalimbali hawakulipwa fedha zao. Wafanyakazi wa serikali walichelewa kulipwa mishahara yao. Kipindi kingine cha uongozi uchumi ulikuwa kinyume cha ule wa kwanza" Sitaki kuvisema vipindi hivyo, lakini hata nisipotaja watanzania wanayo majina ya viongozi hao. Sifa za kiongozi namba mbili ni kusimamia utekelezaji wa mipango ya serikali. Matunda ya uongozi wa aina ya pili kila mtanzania alifaidika nayo bila kujali anakotoka.
  5. Wenzetu Marekani wametoka hapo na ndiyo maana wakati wa kesi ya Rais Clinton na Lewinsky wamarekani walisema tunachohitaji ni kiongozi anayeinua uchumi Clinton ametimiza jukumu hili mambo ya uzinzi hayatuhusu sana. Pia wakati wa kumpata Raisi Obama kuna wahafidhina waliojali rangi, kama kawaida walisema rangi sio issue. Mawazo ya kufiria zamu ama ya Zanzibara ama Zanzibar ni mazuri kwa jamii isiyojua nini inakitafuta katika kuchagua raisi kwa maana wahenga wanasema " USIPOJUA UNAKOKWENDA NJIA YOYOTE INAWEZA KUWA CHAGUOA SAHIHI KWAKO, LAKINI KAMA UNAJUA, NJIA MOJA MAALUM NDIYO ITAKAYOKUFIKISHA.
    Miaka mitatu kutoka sasa, Tanzania itafanya uchaguzi wake mkuu utaohitimisha miaka kumi ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Tanzania kama nchi nyengine duniani, inafata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katika mfumo wa vyama vingi, na iwapo kuna demokrasia ya kweli, basi ni matarajio yetu kuwa chama chchote kitakachoshinda kitapewa haki yake na ridhaa ya kuongoza nchi.
Lakini pamoja na hayo, suali la uwiano wa Ugombea wa kiti cha Urais kwa pande mbili za Muungano, limekuwa likipuuzwa sana kuanikwa katika mijadala mbalimbali nchini. Suali la makubaliano ya mapokelezano ya wadhifa huu mkuu wa nchi baina ya sehemu mbili za Muungano, haujawekwa sawa na ni moja kati ya changamoto kongwe zinazoungana na mkururo wa kero za Muungano hapa nchini.
Tangu tuungane, ni miaka takribani 49 sasa. Wakati Zanzibar ikiwa na marais saba tangu 1964, Jamhuri ya Muungano ndio inatimiza nusu tu ya wale waliokwisha tawala Zanzibar, ikiwa na marais wane tu hadi sasa. Mara baada ya Muungano, Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalim Julius Nyerere, alishika hatamu ya kuiongoza Jamhuri hadi pale ‘alipong'atuka' madarakani kwa hiari yake mwaka 1984/85.
Katika kipindi hichi cha miaka 20, Mwalimu hakuwahi kueleza wala kufafanua lolote kuhusu mpokezano wa madaraka kwa zamu baina ya nchi zetu hizi mbili. Naamini alifanya hivi sio kwa kutojua umuhimu wa kitendo hicho muhimu. Kitendo ambacho kingeashiria usawa mkubwa na haki inayosimamiwa na Muungano wetu. Mwalimu hakulijadili hili kwa sababu alijua wazi kufanya hivyo kungeviza ajenda yake binafsi ya kuimeza Zanzibar ndani ya matumbo ya Tanganyika na kuiondoa kabisa katika ramani ya dunia. Hili ndio lililokuwa lengo lake, bila shaka.
Mungu akikupangia nakama, huna ujuzi wala ujanja. Kwani hayati Sheikh Abeid Karume, ambae ndie aliyekuwa Rais pekee wa Zanzibar aliekuwa akithubutu kumhoji na kumjibu Mwalimu lolote, lakini lakuvunda halina ubani, Sheikh Karume alikufa mapema mno. Tena wakati huo anakufa, bahati mbaya zaidi, ilikuwa Muungano huu haujawa na sura mbaya iliyo wazi wazi kama sasa, japo kiwingu cha dalili hizo mbaya kilianza kuonekana kwa mbali. Sheikh Karume akauwawa, na sababu ya kifo chake, ikafikichwa fikichwa, kisijulikane cha ukweli hadi leo.Ni begeje tu. Na kwanini, watu washuhulike na hili wakati, kufa kwa panzi ni neema ya kunguru? Aliekufa ndio kafa!
Rais Jumbe, alijaribu kwa sana kuhoji hali kama hii. Lakini alichelewa mno.Na kwa jinsi Mwalimu alivyokuwa amejipanga kikazi kiulinzi na kiusalama, juhudi za Sheikh Jumbe zikawaka na moto. Zikaunguwa na kusakatuka kama kijungu cha dagaa tonge, kilichosahauliwa na mpishi aliekwenda kujisuka akisahau kuwa moto hauna sumile. Sheikh Jumbe akang'oka kama Mbuyu uliopigwa halbadiri ya mbayana. Akakunguzuka na mashina yake yote! Njia nyeupe!
Baada ya majaribio haya mawili ya kujitokeza kwa Wazanzibari waliowakijifanya hawaogopi kumuhoji Nyerere, kilichofata ni mpango wa kudhibiti nani awe Rais wa Zanzibar. Ikawa Rais anaewekwa huku kwetu si katika yoyote anaeweza kuuhoji wala kuujadili Muungano, ‘imma faimma' Nyerere awe hai, au awe ameshakufa. Na hili likafanikiwa. Bahati nzuri tu ‘Mtu si mbwa'. Hawa unaowaona walihoji kidogo wakaitwa ‘samaki' na wavyele wao, ni matokezeo tu. Kwani haki haizami na dhulma haidumu.
Viongozi wetu wa Zanzibar, ni watu waliopangwa maalum kufuata utaratibu waliopangiwa na wakubwa zao kule bara. Na kwa maana hii hakuna aliyewahi tena kuhoji kuhusu mgawano wa nafasi ya Urais wa Muungano. Ambapo, penye Uungwana na haki ndani ya Muungano huo, bila shaka tulikuwa tupokelezane zamu. Hata kama tuko katika mfumo wa vyama vingi kiasi gani.
Kwa upande wa CCM bara, hili walikuwa walione pia. Hasa wao wakiwa kama chama chenya nguvu na chenye kushika hatamu. Ipo haja, tena bila kuzozana, kuipa nafasi Zanzibar kuongoza katika Jamhuri ya Muungano, tena katika wadhifa wa Urais, jambo ambalo linaonekana kuwa zaidi ya ndoto ya ‘Alinacha' kwa sasa.
Suali la kumpa Mzanzibari Urais wa Muungano ni ndoto ya Alinacha kwa sababu nyingi. Kwanza tuchukulie chama cha CCM kiwe na matumaini makubwa ya kushinda. Ukweli ni kwamba CCM na Muungano ni mtu na mama yake mzazi. Nasema ni mama kwa sababu hutokea watoto wasio baba kabisa, wala watu wengine, lakini hakuna mtoto asie na mama. Na mapenzi ya mama kwa motto hayana kifano chake. Na tunategemea vivyo hivyo kwa mtoto na mama yake. Kama haya ni kweli, na dhamira ya Muungano ni ile ile ya kuelekea nchi moja. Tena wakati ambao Wazanzibari wanahitaji ‘kupumuwa' kwa nguvu zote. Hili ni gumu.
Isitoshe, ukiwauliza zamu ya Zanzibar lini, wanakujibu kuwa Mwinyi alikuwepo hapa. Hivi Mwinyi ni Mzanzibari? Kwa kigenzo kipi? Na haya naawe huyo Mzanzibari kama ataamuwa kujinadi hivyo, lakini sula linabaki kuwa Marais wawili sasa, yaani miaka 20, Urais uko bara. Kuna ubaya tena gani wakitupa tena kumi, kama kweli tuna nia njema?Hapa panahitajika tuwe wakweli wadadisi kidogo juu ya hili.
Ama kwa upande wa CHADEMA, naona wazo hili si mahala pake hata kidogo. Ingawa CCM na chadema lao moja, na ndio ukaona CHADEMA iliibuka tu kutoka katika ombwe, na kuja kuwa chama chenye nguvu hata kuliko CUF kule bara ambayo ilikuwa inaimarika vizuri siku hadi siku. Lengo, ni kuiondoa na kuizima nyota ya CUF kule wakiamini kuwa, kuanguka kwa CUF bara ni mafanikio makubwa ya kuzima nguvu ya wazanzibari kutaka kujitawala na ‘kupumuwa'. Na hili wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kuna kila dalili kuwa CHADEMA, hawana mpango na Zanzibar zaidi ya kuimaliza zaidi. Na kama hili linasomeka hivyo katika ajenda zao za siri, hawana mpango wa kumpa Mzanzibari nafasi yoyote ile hata ya Ubunge sembuse Urais. Na hii ni kwa sababu moja kuu: CHADEMA ni wabaya zaidi kuliko CCM, kwani ubaya wao haujifichi. Isitoshe, mfungamano wao mkubwa na kanisa ambalo kwa kiasi kikubwa ndio linaloipa kiburi CHADEMA, unaifanya hali ya uwezekano wa Zanzibar wa kuwa na nafasi kubwa kama hio katika Muungano kuwa ya tembo kupenya tundu ya sindano.
Pamoja na hayo, tusikate tamaa. Ipo haja kwa kila mmoja wetu wakiwemo viongozi kuhoji nafasi ya Zanzibar katika uongozi wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Ijapokuwa tunaonekana kukubaliana na kuridhika kabisa na kitazonge, na changa la macho la kupewa kwetu Umakamo wa Rais. Nafasi ambayo haina athari yoyote kwa taifa zaidi ya kufunguwa vikao, kujulia wagonjwa na kuhutubia mikutano ya mazingira na Ukimwi.
Pia tumeridhika na suala la Rais wetu kuwa Waziri katika Jamhuri ya Muungano, jambo ambalo haliingia akilini kabisa. Maana naamini wazi Makamo wa Rais bara, kiitifaki ni mkubwa zaidi kuliko Waziri, ambae pia ni Rais akiwa Zanzibar. Huu ni mchezo wa kitoto au wa kuku lala, tustiane majivu ya macho. Ukweli tunatakiwa tusitosheke na hapo. Tuhoji, tudai, na tutoe kauli moja, ‘Mara hii Urais wa Muungano, ni Zamu ya Zanzibar'. Tuwatazame na pumzi zao!
Natoa hoja......Source ni Mzalendo.net
 
......... Kama wagombea wenyewe ndo hawa na makundi yao... bora Rais aqwamu ya 5 atoke Zenji...
 
Urais sio kwa zamu ni uwezo na kukubaliwa na wapiga kura
 
mpo 1.3M sisi 43.6M halafu mtutawale hilo halipo nawasihi msahau kabisaaaa
 
Yaani jana mnaomba muachwe mpumue leo mnataka uraisi wa JMT nyinyi watu wa ajabu sana,
 
Urais sio kwa zamu ni uwezo na kukubaliwa na wapiga kura
mambo ya ajabu kabisa haya eti sasa mtupe nafasi ya Urais

Wao wanapaswa kujitokeza kugombea waonyeshe sifa zao badala ya kutaka kuwa empowered kama wanawake ambao sasa wameamka wana - compete na wanashinda

hawa jamaa vipi yaani sisi tunyamaze eti sasa ni zamu yao kwa kutumia sheria ipi kama hawatendewi haki waseme ni wapi taratibu zimekosewa ili zirekebishwe
 
Mleteni tu mgombea ila kumbukeni

tanganyika watu ni milioni 43 na zanzibar ni watu milioni 1.
 
Back
Top Bottom