Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Kama mawazo ya watanzania yamefikia kwenye udini, basi hii ni hatari.
 
Kuna mambo manne ambayo yananifanya nitofautiane na wengi ambao wamewatabiria akinamama wa bara Uraisi 2015 au hata mmbara mwingineyo yeyote yule. Kwa mtazamo wangu hili kamwe halitatokea. kwa maono yafuatayo.....

Matukio haya ndiyo yanayoniongoza kusema hivyo;-

a) Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi masuala ya Muungano, Mheshimiwa Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kulipiga hili baragumu kuwa hii sasa ni zamu ya Mzanzibari kuwa Raisi baada ya Kikwete...............Khatibu ni mtu ambaye yupo karibu sana na JK na kwa hiyo ni rahisi sana kujua kauli hiyo ilitokea wapi...............Kwa maoni yangu Khatibu alitumiwa na JK kupima upepo wa kisiasa unavuma vipi.............

b) Maamuzi ya makusudi ya kupendelea makundi maalumu yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM chini ya uongozi wa JK ndani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita..................Haya ni pamoja na kuwazibia wabara kugombea uenyekiti wa UVCCM na kumnufaisha mzenji....Masauni.ambaye hata hivyo alikwenda kuwadhalilisha kwa kukosa sifa za kuwa kijana wa miaka 35 au chini ya hapo na kuwa na vyeti vya kughushi vya umri wake wa kuzaliwa............................

Vile vile uteuzi wa wanawake watatu kugombea nafasi ya uspika na kuyaondoa majina yote ya wanaumme kwa visingizio vya gender-balance...........Matukio haya mawili yaashiria udikteta ndani ya CCM kuchukua sura ifuatayo mwaka 2015:-

Pamoja na kuwa CC ya CCM itaruhusu wagombea wote kutoka kila kona ya nchi kugombea Uraisi lakini majina yatakayorudi ni matatu tu kutoka visiwani kwa minajili ya kile ambacho JK atasema ni kuwaenzi wazanzibari..................na ya kuwa bila ya kuchukua hatua za makusudi hawatakuwa na nafasi za kutoa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....................

Usishangae kama nyuso mpya za visiwani zitaingizwa kwenye baraza la mawaziri litakalotangazwa hivi karibuni kwa minajili ya kuwajenga wazanzibari fulani fulani........kwa lengo la kuwaongezea sifa za kuukwaa uraisi.........na wengi wao watakuwa ni vijana ili huko mbele waseme tena hawa mbona ni vijana haswa na wengi tutakubali hizo ghiliba na kushangilia bila ya kujua malengo haswa nini............

Hivyo mkakati wa JK katika ni nani kumkabidhi nchi wabara andikeni mmeumia..................labda kura zisichakachuliwe na mmbara atatokea upinzani kuliongoza taifa hili..................

Lakini hilo nalo JK atahakikisha kamwe halitokei kwa sababu atakwamisha mabadiliko yoyote katika muundo wa NEC hadi baada ya uchaguzi wa 2015 ili kujenga mazingira ya mzanzibara aweze kutumia idara ya usalama wa taifa na NEC kutwaa madaraka isivyo halali na kinyume na sheria..............kama ambavyo yeye kajisimika madarakani bila ridhaa ya wapigakura na hivyo kuvunja katiba ya nchi hii.............

Habari njema ni kuwa CCM itagawanyika vipande vitatu vya kupinga maamuzi ya CC na upinzani utanufaika sana na wageni kutoka CCM.........na hapo kauli ya Baba wa taifa itakuwa imetimia ya kuwa ili CCM ishindwe kutwaa madaraka ni lazima ivunjike vipande vipande yenyewe.............................

Hivyo ukombozi wa kweli wa mtanzania unategemea sana JK afanye makosa haya comes 2015...................Eeeeeeeeeeeeeeehh mwenyezi Mungu mwongoze huko gizani nasi tupate unafuu wa kiuchumi na shida hizi zipungue za kudhulumiwa na mafisadi wa CCM......................

Haya ni maono yangu na ya kwako je..................waonaje mustakabali wa Taifa in 2015?

Mimi nadhani wazanzibar wangetulia na urais wa visiwani huko tuu.. hivi unategemea nini marais wote wawe WAZANZIBAR katika karne hii bila Nyerere?! Si wote tutakwenda kuiji!!? Maamuzi ya mambo yasioya Muungano yawe mikononi mwa Mzanzibari?! KWELI?! Na wabara tupo wengi tuu tunaangalia UAMSHO ukiingia na kucross boda Bara?! Hapo kwa kweli sijaelewa! Wazenj si watajiona wa maana sana kutoa marais kote kote... Watasema na gas na mafuta vipelekwe Vuga/Mnazi mmoja!!!? LOl I CAN'T WAIT TO SEE THIS MESS!!
 
Mimi nadhani wazanzibar wangetulia na urais wa visiwani huko tuu.. hivi unategemea nini marais wote wawe WAZANZIBAR katika karne hii bila Nyerere?! Si wote tutakwenda kuiji!!? Maamuzi ya mambo yasioya Muungano yawe mikononi mwa Mzanzibari?! KWELI?! Na wabara tupo wengi tuu tunaangalia UAMSHO ukiingia na kucross boda Bara?! Hapo kwa kweli sijaelewa! Wazenj si watajiona wa maana sana kutoa marais kote kote... Watasema na gas na mafuta vipelekwe Vuga/Mnazi mmoja!!!? LOl I CAN'T WAIT TO SEE THIS MESS!!

zethumb unachungulia mbali sana...........
 
Last edited by a moderator:
Hii kali kama ndo hivyo zamu kwa zamu tuna kazi kubwa sana yakufanya tutoke tulipo.
 
Kama mawazo ya watanzania yamefikia kwenye udini, basi hii ni hatari.

Mangaline udini haukwepeki.....ukizingatia dhehebu moja sera yao ni kukamata dola tu na wala siyo vinginevyo...........
 
Last edited by a moderator:
zethumb unachungulia mbali sana...........

Rutashubanyuma unajua kuna vitu vingine wazanzibar wangetulia tu na kuendelea na maisha kama kawaida huku wakipata hivyo vyoooote wasivyostahili kupewa... Bara tuna wasomi kibao tena wenye upeo mkubwa wa kutuongoza na si kukalia issue zisizo na tija za Kizenj kama....KUJIUNGA OIC, KADHI na kadhalika ukiachilia mbali ishu yao ya UAMSHO...
 
Wazenj wanajiita ni nchi na rais wanae, kwa nn wanawaza urais wa nje ya nchi yao? Nadhani hawako serious.
 
Zanzibar walivurunda wenyewe! Zamu yao ilikuwa mwaka 2005 (Salim) lakini wakamkataa.! hii laana itawaandama maisha. By the way kama Kikwete 2005 alisema ni zamu ya waislam, ni nini kitakachowazuia wakristo kusema 2015 ni zamu yao? Nakuhakikishia hata Muddy atoke kaburini 2015 wakristo hawatakubali tena mwislam apewe urais!

Kweli wazanzibari wataikumbuka hiyo nafasi waliyoichezea...
 
Vipi kuhusu wapagani na freemasons?
Hawapo kwenye ratiba?

Mkuu freemasons anaweza akawa mkristo ama muislamu... Kuhusu wapagani hatuwapi nchi...ila kutokana na trend inafaamika wazi rais lazima awe mkristo...awe chadema ama ccm...trend ipo tayari tangu zamani....
 
Mtanganyika ampigie kura Mzanzibari kuwa RAIS wa JMT. Amini usiamini CCM nao wanafahamu fika, mgombea kutoka Zanzibar is UNELECTABLE (read sio MTAJI WA KISIASA). Kutokana chokochoko za Wazanzibari kuhusu muungano, tayari U-NATIONALIST umejengeka miongoni mwa Watangayika ndiyo maana tunahoji Bi Kidudue kupewa NISHANI ya UHURU wa Tanganyika. Dr. Hussein Mwinyi kuongoza wizara ya Afya ambayo siyo ya muungano.

Pamoja na CCM kujivunia kulindwa na NEC (uchakachuaji) lakini wakifanya makosa hayo kimbunga cha Dr. Slaa cha kura watashindwa kuchakachua because itakuwa beyond thresh hold ya UCHAKACHUAJI. Kama muungano uataendelea mark my words haitatokea tena RAIS wa JMT atokee ZNZ. Alikuwa Mwinyi na hatakuwa mwingine tena.

I pray JK afanye makosa hayo kwani ukombozi wa nchi hii utakuwa umepatikani in SILVER PLATE.
 
Sidhani kama Slaa anatoka Zanzibar,maana ndiye Rais 2015!!!

Kama zanzibar ni nchi iweje tumchague raisi raia wa nchi nyingine atuongoze?? Si Zanzibar ni nchi sio mkoa...basi wacha wajitawale nasi watanganyika tuchague raisi raia wa nchi yetu...
 
Baada ya kupitia maoni ya wengi nakubaliana na watu wanaom-rank Shein kama chaguo sahihi kwa chama cha mapinduzi!Shein ni mtu makini,mpole anapotakiwa kuwa mpole na mkali akiona upuuzi!Hakuwa na makucha ya kutosha alipokuwa VP lakini akipewa anaweza kuleta uwajibikaji!Hana makundi,hana udini ni mkweli kwa anachosema, anajiamini kwa nafasi yake!Lakini tatizo ni kuwa huku mitaani hakuna anayemuongelea!Katika survey yetu ya mwezi wa 9 hakuna hata respondent mmoja aliyemuongelea!LKN mie namuona ni kati ya viongozi wachache wa ccm (kutoka zanzibar,na muislam) ambaye anajua nchi hii haina dini bali wananchi!Kwa CCM Huyu naweza kumpa kura yangu!Naweza kumnadi kwa wenzangu na kumtetea mbele za watu pasipo kujali dini yake,kabila lake wala rangi yake!Kwani huyu namuona ni mtanzania wa kweli anayeamini Tanzania!cjui wenzangu mnaonaje!

Umenena kka...ila bahati mbaya sasa hatutaki ccm tena, labda aje Chadema
 
Kwani Zanzíbar Ilishawahi kutoa rais wa muungano ? ninavyojua Mwinyi alizaliwa bara na kwenda Zanzíbar akiwa mtoto , kwa hiyo yeyé ni Mtanganyika halisi.......................
 
Wazanzibar Zamu Yao ilikuwa hii....Kama sio kura za Wazanzibar JK asingeshinda uteuzi Dodoma ....Salim, alipata kura 600, JK 900 na mwandosya kura 300..in average..
Zanzibar walikuwa na kura 500 ...wakapiga kura za Yamini...zote kwa Kikwete...kisa ,Salim Hizbu!...kura za Zanzibar zikampa ushindi JK ....la sivyo angepata kura 400 ..estimate....so Kama Rais mzamzibar Zamu Yao ndio hiii wailitoa kwa hiari.

Huyo Hussein Mwinyi ...ni mtanganyika kwa wazazi watanganyika...tutakuja kumpa urais...Babu yake Mzaramo wa Mkuranga...na Kalala pale...,Hussein Mwinyi amepata Kuwa mbunge wa Mkuranga ....
 
mzanzibari kutawala Tanzania (Tanganyika) ni ndoto za Mchana! Tuwaache wajitawale wenyewe , tusiwaibie kama wanavyodai. Wana mafuta , gesi na karafuu nadhani watakuwa Jamhuri tukufu ya Zanzibar itakayokuwa na uchumi imara!
 
Official name ya Zanzibar is ......Republic Of Zanzibar And Pemba. Nafikiri wapemba wamekuwa wapole but inatakiwa neno Pemba liwemo......Rais wa Zanzibar na Pemba Dr Ali Mohamed Shein.
 
Umenena kka...ila bahati mbaya sasa hatutaki ccm tena, labda aje Chadema

kweli bongo akili zipo kwenye mifuko ya rambo; yaan huyu dr shein kawa makamu wa raisi wa JMT kisha kaenda kuwa raisi wa zanzibar bado unamfikiria kuja kuwa rais wa JMT miaka yote hiyo yeye tu ndio anafaa! Acheni ujinga
 
Back
Top Bottom