Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

alaa kumbe tunapeana zamu za urais na wazanzibari? i didn't know this - mmhh inawezekana hii kitu imo ndani ya katiba ya muungano somewhere!!
 
Wabara tumechoka kuonewa na Zanzibar safari hii tunataka Mbara agombee urais kwa kuwa 2015 ni zamu ya Wabara kuingoza Zanzibar
Kuna mambo manne ambayo yananifanya nitofautiane na wengi ambao wamewatabiria akinamama wa bara Uraisi 2015 au hata mmbara mwingineyo yeyote yule. Kwa mtazamo wangu hili kamwe halitatokea. kwa maono yafuatayo.....

Matukio haya ndiyo yanayoniongoza kusema hivyo;-

a) Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi masuala ya Muungano, Mheshimiwa Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kulipiga hili baragumu kuwa hii sasa ni zamu ya Mzanzibari kuwa Raisi baada ya Kikwete...............Khatibu ni mtu ambaye yupo karibu sana na JK na kwa hiyo ni rahisi sana kujua kauli hiyo ilitokea wapi...............Kwa maoni yangu Khatibu alitumiwa na JK kupima upepo wa kisiasa unavuma vipi.............

b) Maamuzi ya makusudi ya kupendelea makundi maalumu yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM chini ya uongozi wa JK ndani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita..................Haya ni pamoja na kuwazibia wabara kugombea uenyekiti wa UVCCM na kumnufaisha mzenji....Masauni.ambaye hata hivyo alikwenda kuwadhalilisha kwa kukosa sifa za kuwa kijana wa miaka 35 au chini ya hapo na kuwa na vyeti vya kughushi vya umri wake wa kuzaliwa............................

Vile vile uteuzi wa wanawake watatu kugombea nafasi ya uspika na kuyaondoa majina yote ya wanaumme kwa visingizio vya gender-balance...........Matukio haya mawili yaashiria udikteta ndani ya CCM kuchukua sura ifuatayo mwaka 2015:-

Pamoja na kuwa CC ya CCM itaruhusu wagombea wote kutoka kila kona ya nchi kugombea Uraisi lakini majina yatakayorudi ni matatu tu kutoka visiwani kwa minajili ya kile ambacho JK atasema ni kuwaenzi wazanzibari..................na ya kuwa bila ya kuchukua hatua za makusudi hawatakuwa na nafasi za kutoa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....................

Usishangae kama nyuso mpya za visiwani zitaingizwa kwenye baraza la mawaziri litakalotangazwa hivi karibuni kwa minajili ya kuwajenga wazanzibari fulani fulani........kwa lengo la kuwaongezea sifa za kuukwaa uraisi.........na wengi wao watakuwa ni vijana ili huko mbele waseme tena hawa mbona ni vijana haswa na wengi tutakubali hizo ghiliba na kushangilia bila ya kujua malengo haswa nini............

Hivyo mkakati wa JK katika ni nani kumkabidhi nchi wabara andikeni mmeumia..................labda kura zisichakachuliwe na mmbara atatokea upinzani kuliongoza taifa hili..................

Lakini hilo nalo JK atahakikisha kamwe halitokei kwa sababu atakwamisha mabadiliko yoyote katika muundo wa NEC hadi baada ya uchaguzi wa 2015 ili kujenga mazingira ya mzanzibara aweze kutumia idara ya usalama wa taifa na NEC kutwaa madaraka isivyo halali na kinyume na sheria..............kama ambavyo yeye kajisimika madarakani bila ridhaa ya wapigakura na hivyo kuvunja katiba ya nchi hii.............

Habari njema ni kuwa CCM itagawanyika vipande vitatu vya kupinga maamuzi ya CC na upinzani utanufaika sana na wageni kutoka CCM.........na hapo kauli ya Baba wa taifa itakuwa imetimia ya kuwa ili CCM ishindwe kutwaa madaraka ni lazima ivunjike vipande vipande yenyewe.............................

Hivyo ukombozi wa kweli wa mtanzania unategemea sana JK afanye makosa haya comes 2015...................Eeeeeeeeeeeeeeehh mwenyezi Mungu mwongoze huko gizani nasi tupate unafuu wa kiuchumi na shida hizi zipungue za kudhulumiwa na mafisadi wa CCM......................

Haya ni maono yangu na ya kwako je..................waonaje mustakabali wa Taifa in 2015?
 
Kuzungumzia uzanzibari ni sawa na kuzungumzia uchaga,umakonde n.k.Tunataka serikali moja pekee tanzania na rais tumchague kwa utanzania wake FULL STOP!
 
Wabara tumechoka kuonewa na Zanzibar safari hii tunataka Mbara agombee urais kwa kuwa 2015 ni zamu ya Wabara kuingoza Zanzibar

Kikwete kweli anaweza kuhakikisha anapeleka wazazibar watatu mkutano mkuu ...Kama livyofanya issue ya spika......mkumbuke wazazibar ndio waliombeba 2005 ,na wakamtosa mzanzibar mwenzao...Salim.....
Inawezekana kuwa Kikwete aliwaahidi kitu....Kama hiki......But ni lazima ajuwe akiweka mgombea Mzazibar basi amewapa ushindi Chadema....

Nyerere alisema tuchague Rais Mtanzania kwanza kwa kuwaza na kutenda.....Ukiondoa Salim hakuna mzanzibar aliyedhubutu kuinua mdomo wakati muungano unachezewa kuutetea utanzania.....wote wanaogopa......
 
Rais anayekuja ni mtanzania anaishi diaspora.
 
Serikali moja,raisi mmoja,waziri mkuu mmoja,bunge moja,bendera moja,wimbo mmoja wa taifa na utaifa mmoja.Haya mambo sijui ya Udini,Ukanda,Rangi hayana mashiko kwa maskini walio matajiri wa rasilimali na wanaoleta mambo haya ndio haswa wanaonufaika nayo.Ikiwezekana kabisa ni kufunga midomo ya watu kwa miaka mitano weka serikali ya mseto kuondoa U-CCM,U-CDM na U-CUF na kujenga utaifa wa kweli.
 
kuwa ni zamu ya mzanzibari hilo sio tatizo ila huyo mzanzibari awe mkristo maana ni zamu ya wakristo pia
 
kuwa ni zamu ya mzanzibari hilo sio tatizo ila huyo mzanzibari awe mkristo maana ni zamu ya wakristo pia


ukiristo utakusaidia nini wewe? Cha msingi ni muundo wa serikali na si imani ya mtu.
 
kama wao wenyewe wanataka muungano uvunjike.....watatuongozaje jee wakituvunja na sisis....?
 
Napenda sana mungu amuongoze jk akosee 2015 ili ss nasi tuende sambamba kati ya umri wa nchi yetu na umri wa akili wa nchi yetu.
 
Miaka mitatu kutoka sasa, Tanzania itafanya uchaguzi wake mkuu utaohitimisha miaka kumi ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete. Tanzania kama nchi nyengine duniani, inafata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katika mfumo wa vyama vingi, na iwapo kuna demokrasia ya kweli, basi ni matarajio yetu kuwa chama chchote kitakachoshinda kitapewa haki yake na ridhaa ya kuongoza nchi.
Lakini pamoja na hayo, suali la uwiano wa Ugombea wa kiti cha Urais kwa pande mbili za Muungano, limekuwa likipuuzwa sana kuanikwa katika mijadala mbalimbali nchini. Suali la makubaliano ya mapokelezano ya wadhifa huu mkuu wa nchi baina ya sehemu mbili za Muungano, haujawekwa sawa na ni moja kati ya changamoto kongwe zinazoungana na mkururo wa kero za Muungano hapa nchini.
Tangu tuungane, ni miaka takribani 49 sasa. Wakati Zanzibar ikiwa na marais saba tangu 1964, Jamhuri ya Muungano ndio inatimiza nusu tu ya wale waliokwisha tawala Zanzibar, ikiwa na marais wane tu hadi sasa. Mara baada ya Muungano, Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalim Julius Nyerere, alishika hatamu ya kuiongoza Jamhuri hadi pale ‘alipong’atuka’ madarakani kwa hiari yake mwaka 1984/85.
Katika kipindi hichi cha miaka 20, Mwalimu hakuwahi kueleza wala kufafanua lolote kuhusu mpokezano wa madaraka kwa zamu baina ya nchi zetu hizi mbili. Naamini alifanya hivi sio kwa kutojua umuhimu wa kitendo hicho muhimu. Kitendo ambacho kingeashiria usawa mkubwa na haki inayosimamiwa na Muungano wetu. Mwalimu hakulijadili hili kwa sababu alijua wazi kufanya hivyo kungeviza ajenda yake binafsi ya kuimeza Zanzibar ndani ya matumbo ya Tanganyika na kuiondoa kabisa katika ramani ya dunia. Hili ndio lililokuwa lengo lake, bila shaka.
Mungu akikupangia nakama, huna ujuzi wala ujanja. Kwani hayati Sheikh Abeid Karume, ambae ndie aliyekuwa Rais pekee wa Zanzibar aliekuwa akithubutu kumhoji na kumjibu Mwalimu lolote, lakini lakuvunda halina ubani, Sheikh Karume alikufa mapema mno. Tena wakati huo anakufa, bahati mbaya zaidi, ilikuwa Muungano huu haujawa na sura mbaya iliyo wazi wazi kama sasa, japo kiwingu cha dalili hizo mbaya kilianza kuonekana kwa mbali. Sheikh Karume akauwawa, na sababu ya kifo chake, ikafikichwa fikichwa, kisijulikane cha ukweli hadi leo.Ni begeje tu. Na kwanini, watu washuhulike na hili wakati, kufa kwa panzi ni neema ya kunguru? Aliekufa ndio kafa!
Rais Jumbe, alijaribu kwa sana kuhoji hali kama hii. Lakini alichelewa mno.Na kwa jinsi Mwalimu alivyokuwa amejipanga kikazi kiulinzi na kiusalama, juhudi za Sheikh Jumbe zikawaka na moto. Zikaunguwa na kusakatuka kama kijungu cha dagaa tonge, kilichosahauliwa na mpishi aliekwenda kujisuka akisahau kuwa moto hauna sumile. Sheikh Jumbe akang’oka kama Mbuyu uliopigwa halbadiri ya mbayana. Akakunguzuka na mashina yake yote! Njia nyeupe!
Baada ya majaribio haya mawili ya kujitokeza kwa Wazanzibari waliowakijifanya hawaogopi kumuhoji Nyerere, kilichofata ni mpango wa kudhibiti nani awe Rais wa Zanzibar. Ikawa Rais anaewekwa huku kwetu si katika yoyote anaeweza kuuhoji wala kuujadili Muungano, ‘imma faimma’ Nyerere awe hai, au awe ameshakufa. Na hili likafanikiwa. Bahati nzuri tu ‘Mtu si mbwa’. Hawa unaowaona walihoji kidogo wakaitwa ‘samaki’ na wavyele wao, ni matokezeo tu. Kwani haki haizami na dhulma haidumu.
Viongozi wetu wa Zanzibar, ni watu waliopangwa maalum kufuata utaratibu waliopangiwa na wakubwa zao kule bara. Na kwa maana hii hakuna aliyewahi tena kuhoji kuhusu mgawano wa nafasi ya Urais wa Muungano. Ambapo, penye Uungwana na haki ndani ya Muungano huo, bila shaka tulikuwa tupokelezane zamu. Hata kama tuko katika mfumo wa vyama vingi kiasi gani.
Kwa upande wa CCM bara, hili walikuwa walione pia. Hasa wao wakiwa kama chama chenya nguvu na chenye kushika hatamu. Ipo haja, tena bila kuzozana, kuipa nafasi Zanzibar kuongoza katika Jamhuri ya Muungano, tena katika wadhifa wa Urais, jambo ambalo linaonekana kuwa zaidi ya ndoto ya ‘Alinacha’ kwa sasa.
Suali la kumpa Mzanzibari Urais wa Muungano ni ndoto ya Alinacha kwa sababu nyingi. Kwanza tuchukulie chama cha CCM kiwe na matumaini makubwa ya kushinda. Ukweli ni kwamba CCM na Muungano ni mtu na mama yake mzazi. Nasema ni mama kwa sababu hutokea watoto wasio baba kabisa, wala watu wengine, lakini hakuna mtoto asie na mama. Na mapenzi ya mama kwa motto hayana kifano chake. Na tunategemea vivyo hivyo kwa mtoto na mama yake. Kama haya ni kweli, na dhamira ya Muungano ni ile ile ya kuelekea nchi moja. Tena wakati ambao Wazanzibari wanahitaji ‘kupumuwa’ kwa nguvu zote. Hili ni gumu.
Isitoshe, ukiwauliza zamu ya Zanzibar lini, wanakujibu kuwa Mwinyi alikuwepo hapa. Hivi Mwinyi ni Mzanzibari? Kwa kigenzo kipi? Na haya naawe huyo Mzanzibari kama ataamuwa kujinadi hivyo, lakini sula linabaki kuwa Marais wawili sasa, yaani miaka 20, Urais uko bara. Kuna ubaya tena gani wakitupa tena kumi, kama kweli tuna nia njema?Hapa panahitajika tuwe wakweli wadadisi kidogo juu ya hili.
Ama kwa upande wa CHADEMA, naona wazo hili si mahala pake hata kidogo. Ingawa CCM na chadema lao moja, na ndio ukaona CHADEMA iliibuka tu kutoka katika ombwe, na kuja kuwa chama chenye nguvu hata kuliko CUF kule bara ambayo ilikuwa inaimarika vizuri siku hadi siku. Lengo, ni kuiondoa na kuizima nyota ya CUF kule wakiamini kuwa, kuanguka kwa CUF bara ni mafanikio makubwa ya kuzima nguvu ya wazanzibari kutaka kujitawala na ‘kupumuwa’. Na hili wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Kuna kila dalili kuwa CHADEMA, hawana mpango na Zanzibar zaidi ya kuimaliza zaidi. Na kama hili linasomeka hivyo katika ajenda zao za siri, hawana mpango wa kumpa Mzanzibari nafasi yoyote ile hata ya Ubunge sembuse Urais. Na hii ni kwa sababu moja kuu: CHADEMA ni wabaya zaidi kuliko CCM, kwani ubaya wao haujifichi. Isitoshe, mfungamano wao mkubwa na kanisa ambalo kwa kiasi kikubwa ndio linaloipa kiburi CHADEMA, unaifanya hali ya uwezekano wa Zanzibar wa kuwa na nafasi kubwa kama hio katika Muungano kuwa ya tembo kupenya tundu ya sindano.
Pamoja na hayo, tusikate tamaa. Ipo haja kwa kila mmoja wetu wakiwemo viongozi kuhoji nafasi ya Zanzibar katika uongozi wa juu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano. Ijapokuwa tunaonekana kukubaliana na kuridhika kabisa na kitazonge, na changa la macho la kupewa kwetu Umakamo wa Rais. Nafasi ambayo haina athari yoyote kwa taifa zaidi ya kufunguwa vikao, kujulia wagonjwa na kuhutubia mikutano ya mazingira na Ukimwi.
Pia tumeridhika na suala la Rais wetu kuwa Waziri katika Jamhuri ya Muungano, jambo ambalo haliingia akilini kabisa. Maana naamini wazi Makamo wa Rais bara, kiitifaki ni mkubwa zaidi kuliko Waziri, ambae pia ni Rais akiwa Zanzibar. Huu ni mchezo wa kitoto au wa kuku lala, tustiane majivu ya macho. Ukweli tunatakiwa tusitosheke na hapo. Tuhoji, tudai, na tutoe kauli moja, ‘Mara hii Urais wa Muungano, ni Zamu ya Zanzibar’. Tuwatazame na pumzi zao!
Natoa hoja......Source ni Mzalendo.net
 
Najiuliza inakuwaje Muungano hawautaki na huku wanataka Rais wa muungano atoke kwao?si maajabu haya?
 
Hakuna Ibara hata moja katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoelezea Urais wa zamu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar.Kinachoelezwa wazi kabisa kwenye Katiba hiyo ni kuwa iwapo Mgombea wa Urais atatoka upande mmoja wa Muungano,Mgombea Mwenza(ambaye atakuwa Makamu wa Rais) atatoka upande mwingine. Labda suala hilo liletwe na Katiba mpya...
 
Hakuna Chama chochote makini including CCM kitamsimamisha mgombea URAIS wa JMT kutoka Zanzibar. Mtaji mkubwa wa kisiasa uko Tanganyika, with NATIONALISM growing in both Tanganyika and Zanzibar hakuna Mtanganyika yeyote makini atakayempgia kura mgombea kutoka Zanzibar.

Therefore Mgombea URAIS kutoka ZNZ is UNELECTABLE. Kama Muungano utaendelea with multipartisim on the helm haitatokea tena RAIS wa JMT akatoka ZNZ Mark my words. Huo ndio UKWELI mchungu kwenu Wazanzibari.
 
Mkuu, umelalamika sana ila sijajua Mzanzibari halisi ni yupi/nani.
 
Hakuna shida, Urais wa Zanzibar ni zamu ya Tanganyika!

Na vipi kuhusu madai ya kupumua, uhuru kamili?
 
Hakuna Chama chochote makini including CCM kitamsimamisha mgombea URAIS wa JMT kutoka Zanzibar. Mtaji mkubwa wa kisiasa uko Tanganyika, with NATIONALISM growing in both Tanganyika and Zanzibar hakuna Mtanganyika yeyote makini atakayempgia kura mgombea kutoka Zanzibar.

Therefore Mgombea URAIS kutoka ZNZ is UNELECTABLE. Kama Muungano utaendelea with multipartisim on the helm haitatokea tena RAIS wa JMT akatoka ZNZ Mark my words. Huo ndio UKWELI mchungu kwenu Wazanzibari.

Kwa nini unafikiri mgombea kutka ZNZ is unelectable? Nini kitatokea kama hilo likiwa ni mojakati ya mapendekezo kwenye katiba mpya ya Tanzania?
 
wazenj ni watu wa ajabu sana,wao Zanzibar ni yao Tanganyika ni yetu,mademu zao ni wao ,mademu wa Tanganyika wa wote......hii haikubaliki.kama wanataka haki hiyo sharti wawe na wajibu wa kukubali watanganyika nao kuwa na haki zao za msingi zenj na sio kupigwa risasi,kuchomemewa makanisa na mabar.
 
Back
Top Bottom