Mzee Mwanakijiji,
Na wewe kwa upotoshaji kweli umekubuhu,
Well.. tuangalie upotoshaji wangu hapa kwani maneno yangu yote yapo hapa hapa. Kati ya mimi na wewe tutaona nani anayejaribu kupotosha watu licha ya ukweli kuwa mbele yetu.
ukija pewa nafasi sitashangaa nikiona unakuwa worse kuliko hata hao akina Rweyemamu.
Tofauti kati ya mimi na wewe ni kuwa sitaki nafasi yoyote ile. Sitoshangaa wewe ukijija kupata nafasi unaweza kuwa worse kuliko wale tunaoshindana na leo ambao hawako tayari kuukiri ukweli hata kama unawakodolea macho.
Katika mjadala wote huu sijaona mahali popote palipokufanya uje na conclusion kama hiyo unless kama lengo ni ku SPIN.
Hilo ndilo tatizo lako; kwa sababu hujaona basi unafikiri hakuna! Itakuwa furaha yangu kukumbusha tulikoanzia.
Mimi nilisema hivi kwenye ukurasa wa sita (6) wa thread hii (nimeweka msisitio wa point of contention):
Manji ameenda mahakamani amefanya jambo jema.. kwa sababu huko atatueleza kwanini yeye arudishe fedha za Kagoda ambazo zilichotwa kwa wizi? Mahakama itabidi iite ushahidi wa Kagoda.... na kutaka Mwanyika na wenzie wawe mashahidi upande wa Mengi..
Hili wala siyo gumu.. Hili siyo suala la Manji kama wengi wanavyofikiria ni katika kutaka kuifunua Kagoda....
that is whats up.. didn't I say time is up? It is.. Namshauri na Rostam afanye hivyo hivyo.. pleaaasse!!!
Hoja yangu hapo juu ilikuwa na msingi kuwa:
a. Mengi kwa vile amefikishwa mahakamani atatakiwa ajitetea. Katika kujitetea kwake atasema Manji anahusika na x,y. Mahakama itauliza unaushahidi gani? Mengi atasema ushahidi uko kwa b and c ambao walifanya uchunguzi na Manji alifanya m n katika uchunguzi huo na hivyo kumhusisha na wizi wa Kagoda! (Kampuni ya Kagoda haitaji familia ya Manji au jina la Manji).
b. Kwamba Mahakama ina nguvu ya kisheria ya kuita huo ushahidi au mashahidi wa upande wowote ule.
HIYO: ndiyo ilikuwa hoja. Hapo sijazungumzia uzito wa ushahidi au kwa namna yoyote kuhojia utaratibu wa kuendesha mashtaka. Nimezungumzia a specific legal issue. Kitu ambacho Dillunga alikielewa.
Alikielewa na ndiyo sababu kwenye ukurasa huo huo alikuja na kunijibu hivyo na akijibu the exact point of contention:
Kesi ya Mengi na Manji, mahakama haiwezi kuita shahidi aje kumsaidia Mengi ua Manji.
Manji akishatoa vielelezo vya vipengele vya madai (elements of the course of action) kwamba Mengi kanichafua, mzigo unahamia kwa Mengi, sio kwa mahakama, kwa Mengi, kuthibitisha uchafu wa Manji au kuthibitisha kwamba hakusema Manji fisadi papa.
Au unasemaje, ewe mkufunzi wa sheria wa jamvi, Mkuu Mwanakijiji?
Jibu la Dilunga linasema kuwa:
a. Mahakama haina uwezo wa kuita shahidi (ndiyo maana ya neno "haiwezi").
b. Mashahidi hao hawawezi kuitwa na mahakama kwa upande wowote kuusaidia upande huo.
Hapo ndipo mgogoro wote ulipo. Kitu ambacho bila ya shaka hukielewi kwa sababu kama ulivyosema hapa chini kuwa:
Kama nilivyosema mimi sio mwanasheria
Sasa licha ya kukiri kuwa wewe si mwanasheria unadai kujua kile ambacho sheria inasema kwa uhakika!
Inashangaza unajenga hoja nyepesi kama hii:
ila nimeona cases nyingi tu ambazo mashahidi wanaotakiwa na upande mmoja au mwingine hawafiki mahakamani na case inaendelea.
Kuona mashahidi hawafiki na kesi inaendelea mbona siyo jambo la kuishangaza dunia! si shahidi wa kesi ya Zombe kafa na kesi inaendelea? Kuna mashahidi ambao wanajitolea kuwa mashahidi lakini kuna mashahidi wanaoweza kuitwa na mahakama (summons) na watatakiwa kufika na wakigoma wanaweza kushtakiwa kwa kudharau mahakama (contempt of court). Kwa vile mashahidi wengi yawezekana uliowaona ni wale ambao kwa hiari yao wamejitolea kuwa mashahidi haina mahakama kama kuna shahidi mbishi (hostile witness) ambaye ni muhimu kwa kesi halafu akaitwa na mahakama na kesi ikaendelea!
Mfano juzi tu hapa case ya Prof. Mahalu ambayo mashahidi mbalimbali wa serikali wameshindwa kwenda mahakani na hakimu akaamua case iendelee.
Ndiyo; siyo la kushangaza..
Angalia pia Milosovic naye alitaka mashahidi kibao lakini akaambiwa wao sio relevant kwenye cases husika.
of course.. mashahidi lazima wawe relevant! Itakuwa ni upuuzi kumlazimisha mtu ambaye hana relevance kwenye kesi aje kutoa ushahidi!
Mimi nakumbuka hata wakati wa case ile ya wale waliotaka kumpindua Nyerere, mashahidi wengi ambao waliomba waje mahakamani, hawakwenda.
Shahidi anayeomba hana ulazima wa kwenda mahakamani!
Sasa nitashangaa kweli kwenye case ya madai kama utaweza kumuita mtu yeyote unayemtaka bila kuonyesha sababu za msingi za kuwepo kwake.
Ndio maana naweza kuona upotoshaji wako hapa; ni wapi nimesema umuite mtu bila "sababu ya msingi za kuwepo kwake"?
Dillunga alisema madai haya ambayo yaliendelea mjadala wetu juu ya nguvu za mahakama za kuita mashahidi wanaohusiana na hiyo kesi kwa upande wowote.
Nimeeleza hivi, narudia:
Unakosea na kupotosha kutamka kwamba mahakama itajiingiza kuita mashahidi kuthibitisha madai ya Mengi. Ya yeyote, si ya Manji, si ya Mengi.
Manji akishatoa vielelezo vya vipengele vya madai (elements of the course of action) kwamba Mengi kanichafua, mzigo unahamia kwa Mengi, sio kwa mahakama, kwa Mengi, kuthibitisha uchafu wa Manji au kuthibitisha kwamba hakusema Manji fisadi papa.
Kesi ya Mengi na Manji mahakama haijiingizi kusaidia kuleta ushahidi wa Kagoda, wa Mwanyika, wa DPP, kusaidia kesi ya Mengi au Manji. Sasa Mkufunzi wa sheria wa jamvi, nifafanulie zaidi, wapi nakosea.
Hapa anarudia kile kile ambacho wewe unakiunga mkono; kuwa mahakama haijiingizi kwenye suala la kuleta mashahidi kuusaidia upande wowote ule unaoshindana. Akaniomba nimuoneshe ni wapi anakosea.
Jibu langu la ombi lake la kiungwana lilikuwa hili (kwenye Ukurasa wa 7 wa thread hii)
unakosea pale unaposema mahakama haijiingizi kama haijiingizi kwanini kwenda mahakamani? The whole purpose ya kwenda mahakamani ni kuihusisha mahakama. Lakini kosa lako linazidi kuonekana unaposema kuwa "mahakama haijiingizi kuleta ushahidi".. umewahi kusikia kitu kinachoitwa subpoena au warrant?
Hapa tukaingia kwenye suala la ushahidi; nikaendelea kwenye jibu langu pale-
Mengi atasema, "Mheshimiwa Jaji ushahidi upo na sehemu ya ushahidi huo unapatikana katika utendaji kazi wa tume ya Mwanyika ambapo Manji alirudisha fedha ambazo azieleze ametoa wapi na amerudisha kama nani, ndiyo maana nimemuita fisadi."
Akisema hivyo, Mahakama itasema nini "kawalete kina Mwanyika"? au Mahakama ina uwezo wa kucompel witness kutokea mahakamani? Sasa Mengi akisema Mahakama imuagize Mwanyika, DPP, Polisi n.k kuja mahakamani mahakama itakataa kwa sababu "haijingizi kuleta ushahidi"?
Utaona ninarudisha hoja kwenye point ya contention (hoja tunayobishania) ambayo inahusu nguvu au uwezo wa mahakama kucompel witness kuja mahakamani. Suala tulilolizungumzia toka awali hapa ni juu ya UWEZO WA MAHAKAMA KUITA MASHAHIDI AU USHAHIDI KWA UPANDE WOWOTE ULE NA KUWA MENGI ANAWEZA KUTUMIA HAKI HIYO KUWAITA MASHAHIDI ANAOWATAKA NA MAHAKAMA IKAWAITA UNDER THREAT OF PUNISHMENT.
Kwa mfano ili uweze kusema Manji ndiye alirudisha pesa za Kagoda lazima uwe na ushahidi kuonyesha hivyo, ushahidi ambao umepatikana kwa njia halali. Hapo ni bank iliyopokea au wale waliokuwa wanapokea hizo pesa, vinginevyo mahakama itakataa kumwita shahidi huyo.
Ndiyo; Rais aliunda tume ya kuchunguza wizi wa EPA. Tukaambiwa kuwa watu fulani wamerudisha fedha walizoiba. Kwa upande wa Kagoda fedha zilirudishwa na mtu fulani. Mtu huyo anajulikana kuwa ni Manji. Manji karudisha fedha za wizi anayejua juu ya kurudishwa huko ni Mwanyika na watumishi wengine wa hiyo timu.
Ili kufikia kiwango cha kukubalika kisheria, Mahakama itamuita Mwanyika aje na ripoti ya wale wote waliorudisha fedha za wizi na kiasi cha walichorudisha. Akikataa, (kumbuka ni relevant witness) Mengi hana kesi, huwezi kumdai mtu wakati unamnyima nafasi ya kuleta mashahidi watakaoprove utetezi wake.
Huo ni mfano mmoja tu.
Mkorogo wa hoja ya awali ulitokea pale ambapo WoS alipoingiza element nyingine kabisa kwenye mjadala huu: Yeye alisema hivi:
Asante Mkuu kwa kufafanua nami niongezee kuwa Kesi hii siyo kama za jinai ambapo serikali ( republic) inatakiwa kuthibitisha pasina shaka, bali ushahidi ni on a balance of probability baina ya mdai na mdaiwa.
Kukusaidia ni kuwa element nyingine iliyoletwa hapa ni uzito wa ushahidi unaotumika kumkuta mtu na hatia katika kesi za madai. Hii haikuwa hoja yangu toka awali. Hoja yangu ilikuwa kwenye uwezo wa mahakama kuiita ushahidi au mashahidi. WoS alionesha kwa usahihi na wala sikubishana naye kwenye hilo kwani ni kweli kuwa kiwango cha uzito wa ushahidi kwenye kesi za madai (daawa) ni cha chini kulinganisha na kesi za jinai.
BUT THAT WAS NOT THE ISSUE. Hatukuwa tunazungumzia ni ushahidi gani unaweza kumsaidia Mengi au Manji..
Nilimuuliza WoS a point blank question: Je mdaiwa ana haki ya kuita mashahidi au kutaka ushahidi uletwe mahakamani?
JIbu lake ni hili:
Anayo haki na ni juu yake kuwaleta yeye mwenyewe.
Hapa ndipo nikagongana naye na nikaenda kwa kirefu kugusa sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Madai (CPC 49/1966).
Nikaonesha Ibara ya 25 inaposema:
"25. Subject to such conditions and limitations as may be prescribed,
the court may, at any time, either of its own motion or of application
of any party-
(a) make such orders as may be necessary or reasonable, in all
matters relating to the delivery and answering of interrogatories,
the admission of documents and facts, and the discovery, inspection,
production, impounding , and return of documents or other,
material objects producible as evidence;"
Nikaonesha kuwa mahakama ina uwezo hata bila kuombwa na upande wowote ule kuita ushahidi au kuagiza urudishwe. Na nikaonesha kuwa hata ibara ya 26 na 27 inayohusu mashahidi inawafunga mashahidi hao na ibara ya 25. Kwani ibara hiyo inasema:
26. The Provisions of sections 23 and 24 shall apply to summonses
witness to give evidence or to produce documents or other material objects.
27. The court may compel the attendance of any person to whom
a summons has been issued under section 25 and for that purpose may-
Penalty for
default
(a) issue a warrant for his arrest;
(b) attach and sell his property;
(c) impose a fine upon him not exceeding one thousand shillings;
(d) order him to furnish security for his appearance and in default
commit him as a civil prisoner.
Sasa hiyo ndiyo ilikuwa issue. Pamoja na hayo watu bado wakaendelea kudai (na bado wewe unaendelea kudai) kuwa mahakama haina uwezo wa kusema nilichosema. Na wengine nao wamekukubalia huu upotoshaji mkubwa wa sheria. NI kwa sababu ya kugundua kuwa ni ubishi usio na tija nikaamua kukubaliana nanyi kuwa nilikuwa nimekosea kwenye point of contention.
Je mahakama katika kesi za madai kwa kuangalia sheria za Tanzania ina uwezo wa kuita ushahidi au mashahidi. Kutokana na utaalamu wa nyinyi jibu ni kuwa hapana.. mashahidi wataenda kwa kujitolea tu na wakijisikia hawawezi kulazimishwa na mahakama kutokea. Nikawakubalia!!!!
Sasa kati ya mimi na wewe ni nani mpotoshaji mkuu wa hoja? Nitawaacha wengine waamue.