Yupo wapi dereva teksi alyefichua njama za kumpindua Nyerere mwaka 1982? Je, alilipwa chochote kama ‘asante’?

Tamim alikuwa anakaa hananasif/stereo kwenye zile kota vikao vingi walikuwa wanafanya pale kwao
Kwq tuliyokulia mitaa hiyo wazee wetu
Washatupa sana mikasa hiyo

Madereva wengi wa taxi ni mainformer

Ova
 
Watu wanachukulia mapinduzi kama kulala kitandani mume na mke.Kwa mwenye wazazi (watu wazima) na watoto hawezi kukaa na kufikiria hii takataka ya mapinduzi ni mbaya kuliko ubaya wenyewe.
Njaa ikimsumbua sana mtu anakuwa akidhani kuwa anaweza kuimaliza kwa kuanzisha mapinduzi. Tunasahau kuwa yapo maisha tena marefu mbele ya safari.
 
Masikini huwa hakosi sababu za kuhalalisha umaskini wake!. Una uhakika upi kuwa mabadiliko ya mfumo wa kuendesha hii nchi yangekuja na neema kwa mtu wa kawaida?.
Wewe una uhakika kwamba mabadiliko hayo hayangeleta neema unayoiwaza? Nisome upya:-
Kwani nchi zote zenye amani Nyerere alizaliwa humo?. Hata asingezaliwa Tanzania huyo nyerere, nchi hii ingekuwa imesimama ilivvyo, pengine ingekuwa bora zaidi. Inawezekana kuwepo Nyerere ktk nchi hii ndio chanzo cha matatizo yote tuliyonayo Leo. Alizima ndoto/mawazo mbadala ya akina Tuntemeke Sanga, Oscar Kambona, Edwin Mtei etc. Mawazo ya hawa wazalendo na wengineo yangepokelewa, yawezekana leo Tanzania ingekuwa mbali. Ila kwa udikteta/uroho wa madaraka wa Nyerere hawa waliishia kizuizini au kutoroka nchi.
(Kumbuka pia wakulaumiwa kwa hiki 'kijitabu ha 1977' ni Nyerere huyo)
 
Nyerere aliwezesha kuwa na umoja na hiyo ni sifa inayoliweka taifa hili kama lilivyo leo hii. Asingehubiri umoja kwa nguvu kama alivyofanya pengine leo hii tungekuwa na mgawanyiko wa ajabu sana.

Awamu ya JK ambayo Lowassa alikuwa waziri mkuu, palitokea uonevu wa hali ya juu, watu kuporwa mali zao bila ya kupata mwokozi, tamaa za wapenda mali zikaanza kuwa chanzo cha uonevu kwenye jamii zetu.

Hawa hawa waonevu wangepewa nafasi tangu mwaka 1961 tungekuwa na taifa lenye nyufa za ajabu. Hivyo Nyerere hakuwa mkamilifu lakini angalau alikuwa na maono ya kupunguza uonevu ambao ungeweza kuzaliwa iwapo asingekuwa mwasisi wa Taifa.
 
Mapinduzi yakitokea Kila mtu anataka kuwahi fursa ndio maana JPM alivyofariki wakatamani wachukue kiti ila hawakuweza sababu katiba ndio ilikua inafuatwa ila yangekua mapinduzi ungesikia Bashiru kajitangaza Rais, mara Mabeyo naye kapindua, ghafla Samia naye anaunda jeshi la waasi inakua vurugu tupu.

So mapinduzi sio ya kushabikia hata kama tulimchoka Nyerere hali ingekua mbaya zaidi maana madaraka yangebaki bado CCM ila Kwa Wezi zaidi.
Mabeyo hapa alifanya kazi kubwa sana, maana nasikia Mama alikuwa amepangiwa ziara huko Tanga na alikuwa huko, na huku watu walikuwa wanataka kupindiua Katiba
 
Ndio MAANA bas nyerere alitoa kauli ile kuhusu chadema kama chama makini KUMBE alikua anamaanisha kuwa kipo chini ya pot jasusi sio!!?

Ndio maana chadema ipo imara aiseh ina mizizi mirefu sana!

Nasikia hata kikwete alitishia kuwa akikatwa ataenda chadema na atashinda KUMBE alijua chadema ni kitu gani Aiseh!

Kama mambo yapo hivyo Bas nachelea kusema mnywaji Mkuu wa konyagi wa chadema sio mtu wa kawaida atakua pot huyo!!!
Na ndiyo sababu hawezi kutoka kwenye ile nafasi pale juu...doing damage control kwa niaba ya.....

Scratch my back, I will scratch yours!
 
Comment yako imenifikirisha mno...

Kweli sisi vijana ni watu wa muhemko...

Yaani umepata "likes" 19?!!!

It's terrible

Tunalijenga taifa la aina gani ?!!!

Ni kutopenda umaana wa SOMO LA URAIA?!!!

Sijui ni kipi haswa?!!

Watu 19 wanashabikia MAPINDUZI YA KIJESHI ?!!! HAVOC HAVOC HAVOC

Hivi unadhani salama ya nchi ni kupinduana kijeshi?!!!! wanajeshi unawajua kwa kuwaona tu wamevaa sare huku mitaani ?!!! (

Kuiondoa "status quo" kijeshi ni kujiingiza katika "Moto wa duniani"...kwani "wakionja" huwa inafanywa ADA....

Wacha maskhara wewe
Kuna pahala nilisoma: tough times create strong men; strong men create easy times, easy times create soft men, soft men create tough times....

Ukiangalia vijana wa sasa hawa waliozaliwa nyumba zenye TV, they're soft and take things for granted....wakiachwa bila udhibiti watengeneza tough times!

Kirahisi tu kijana anaona bora mapinduzi yaje....nilikuwa dodoma wakati wa vita ya Uganda na niliona heka heka za kuchimba mahandaki...

....you don't think properly kama unaona ni sawa tu kuwa na chaos kwenye nchi!
 
Nyerere simkubali tu kwa issue za ujamaa na kwenda kupambana vita ambayo haikuwa na umuhimu sana kwa wakati ule hivi viwili ndio ilikuwa mwanzo wa mdororo wa kiuchumi na umasikini kwa Tanganyika.

Oscar Kambona naamini angetuvusha mbali sana kwa wakati ule , he is the president we never had.
 
Historia ya Serikali ya nchi hii ina Mengi na Mengi hayo hatuyajui.

Kina Hanspope, Maganga, Tamimu na wengine wengi walipanga kumuua na kuipundua Serikali ya Mwl Nyerere.

Inadaiwa dereva teksi aliyekuwa akiwasafarisha wapanga mapinduzi kuhudhuria vikao vyao vya Siri alibaini mpango wao na kuripoti kwa vyombo vya usalama.

Muda umeenda Sasa, huyu dereva teksi ni nani? Yupo wapi Sasa? Alilipwa nini na Serikali Kama shukurani ya kuinusuru nchi?
FaizaFox anadai ni hekima na busara za waislam ndio walizima mapinduzi hayo. Anawataja Kitwana Kondo na Col. Kashmir ndio walizima mpango mzima wa kumpindua Nyerere. Kumbe kuna aliyesanua mpango mzima? Huyo dereva ajulikane tu maana historia haitamuacha katika kadhia hiyo. Si siri tena iwekwe wazi tu aliko huyo dereva umma ufahamu
 
Hayo mapinduzi yaliyozimwa na waislamu ni yale ya mwaka 1964. Nyerere kanusurika majaribio Mengi mno.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom