Ni nani aliyemuua Komando Muhammad Tamimu🤔? (Sehemu ya 3️⃣)

Abdul S Naumanga

JF-Expert Member
Jan 28, 2024
353
620
"Kuepusha kuwachosha wasomaji, Swali pekee linalobakia katika mkasa huu ni Je, ni hatua gani za kisheria zilichukuliwa baina ya wahusika?. Jibu la swali hili tutakua nalo katika sehemu ya tatu ya mkasa huu. Kama ni embe, basi hapa tumefika kwenye kokwa, ndo kwanza utamu wa simulizi hii unaenda kuanza". Haya yalikua ni maneno ya jioniii katika sehemu ya pili ya mkasa huu wa kusisimua na wakihistoria wa mapinduzi dhidi ya Mwl. Nyerere, unaomuhusisha aliyekuwa nguli wa maswala ya soka nnchini mzee wetu marehemu Zacharia Hans Poppe.

Nikukaribishe mdau tuliokuwa wote kwanzia sehemu ya kwanza. Katika sehemu hii ya tatu ya mkasa huu wenye mengi yaliyojificha ama yasiofahamika na wengi. Lakini kwa ambae ndio mara yakwanza anafatilia mkasa huu, ni ushauri wangu kwako kufatilia kwanza sehemu zilizopita kwa kugusa link hapo chini👇 ili iwe rahisi kuelewa plot (mpangilio wa story.​
As always, background first.
Katika sehemu iliyopita, tulishuhudia matukio ya kusisimua yaliyojawa na njama zilizopangwa na kusukwa kwa siri na Pius Mtakubwa Lugangira, maarufu kama 'Uncle Tom', akishirikiana na Captain Hatty Macghee (Hatibu Gadhi) na Komandoo Muhammed Tamimu, ili kuipindua serikali ya Nyerere mnamo tarehe 9 Januari, 1983.

Wakati huo, watu hawa walikuwa wameingia nchini kisiri kutoka nje ya nchi, na kuanza kuajiri na kushawishi watu mbalimbali hasa wanajeshi kujiunga na njama zao. Wapo walikataa, lakini wapo wengine, kama vile Lieutenant Zacharia Hans Poppe, Captain Christopher Kadego na Lieutenant Eugene Maganga, walikubali kushiriki katika mpango huo wa uhaini.

Nyumba mbili, moja iliyopo Kinondoni na nyingine Masaki, ziligeuka kuwa viwanja vya kupanga njama hizi. Huku Hatibu Gandhi akiwa mstari wa mbele katika maandalizi haya, na Uncle Tom akijificha nyuma ya pazia la biashara, katika mpango huu.

Lakini, kama ilivyo kwa njama nyingi, kulikuwa na wale waliokuwa tayari kuzisaliti. Captain Albert Ballati na Staff Sergeant Boniface Temu walijifanya kuwa sehemu ya mpango huo, wakati kwa siri walikuwa wakitoa taarifa kwa usalama wa taifa. Ushahidi uliotolewa na watu mbalimbali, kama vile Abdullah Mhando na Iddi Mushi Stambuli, uliweka wazi mipango hiyo na hatimaye kuzuia mapinduzi yaliyokuwa yamepangwa.

Sasa, tunaelekea katika sehemu ya tatu, ambapo tunazungumzia zaidi kuhusu matokeo ya njama hizi na athari zake kwa wahusika. Je, ni nini kilifata baada ya kufichuka kwa mipango hii?
KUKAMATWA KWA WAHUSIKA NA KIFO CHA MUHAMMAD TAMIMU.
images (59).jpeg
Wengi husema; moja ya mafanikio makubwa ya intelijensia ya mwalimu Nyerere ni kufanikiwa kuzuia mipango hii ya mapinduzi. Ilikua hivi, baada ya kena Temu na Ballati kuwa wanawasilisha taarifa ya mpango huu katika idara ya usalama wa taifa. Tarehe 6 January, 1983 ikiwa ni siku mbili kabla ya mpango huu wa mapinduzi kufanyika, maamuzi yalifanywa na mamlaka kuanzisha zoezi la pamoja la Jeshi, Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa kukamata wahusika wa njama za kuipindua Serikali ya Jamhuri ya Muungano na kumuua Rais wake.

Katika zoezi hilo, Mohamed Tamim maarufu kama 'Martin Tamim' aliuwawa kwa kupigwa risasi na mtu wa usalama wa taifa (hili lina story yake, tutairudia) alipojaribu kukwepa kukamatwa alipokuwa katika nyumba ya Kinondoni Mkwajuni. Baadaye, watu mbalimbali, wanajeshi na raia, walikamatwa katika zoezi hilo la pamoja.

Kwenye zoezi hili wahusika wote t​
isa (ukimtoa Tamimu aliye uwawa) pamoja na wengine kumi walikamatwa na kushtakiwa kwa makosa matatu ya uhaini, kinyume na kifungu cha 39(2)(a) cha Kanuni ya Adhabu, na kosa moja mbadala la kuficha uhaini, kinyume na kifungu cha 41(b) cha Kanuni ya Adhabu.

Mwishoni mwa kesi ya mashtaka (committal proceeding), watu watano kati ya walioshtakiwa wahakuwa na kesi ya kujibu (No case to answer) na hivyo wakaachiwa huru. Kesi iliendelea na washtakiwa kumi na nne waliokutwa na kesi ya kujibu (Case to answer).

kwakutambua na kuwathamini wasomaji ambao si wanasheria, hapa kuna somo kidogo;​
committal proceeding ama kama wengi tulivyozoea kuita kukaa rumande ni hatua ya kisheria ambapo kesi ya mtuhumiwa inapelekwa mahakama ya chini kabla ya kwenda Mahakama Kuu. Hii inatokea pale ambapo kesi inayomkabili mtuhumiwa ni ya aina ambayo haiwezi kusikilizwa na kusikilizwa na mahakama za chini, kama vile mahakama za mwanzo au za wilaya. Kesi hizi ni kama za mauaji na uhaini.​

Katika hatua hii, hakimu wa mahakama ya chini atamsomea mtuhumiwa mashtaka yanayomkabili, lakini mtuhumiwa hahitajiki kujibu mashtaka hayo wala kutoa utetezi. Lengo la committal proceeding ni kujiridhisha kama ushaidi unaoletwa mahakamani unajitosheleza kwaajili ya kufungua kesi zidi ya mtuhumiwa, pia kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapata fursa ya kuelewa mashtaka dhidi yake kabla ya kesi kupelekwa Mahakama Kuu ambako itasikilizwa.​

Kwa hiyo, committal proceeding ni muhimu kwa sababu inatoa nafasi kwa mtuhumiwa kujua mashtaka yake na kujiandaa kwa ajili ya kesi inayokuja Mahakama Kuu, lakini pia inaweza kuwa na changamoto kwa sababu ya ucheleweshaji unaoweza kutokea katika mchakato huo.


Kwahiyo kesi hii ilichukua takriban mwaka mmoja kuhitimishwa. Upande wa mashtaka uliita jumla ya mashahidi tisini na saba, wakati upande wa utetezi uliita mashahidi arobaini na watatu ikiwa ni pamoja na washtakiwa wenyewe. Mwisho wa kesi ndefu mahakama kuu, washtakiwa tisa tu ndio walipatikana na hatia kwa makosa matatu ya uhaini na kila mmoja akahukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Washtakiwa wengine watano akiwemo aliyekuwa msaidizi wa Mwl Nyerer, bwn Christopher Pastor Ngaiza waliachiwa huru kwa mashtaka yote.

Turudi kwenye story ya Tamimu sasa, Kifo cha Muhammad Tamimu kimekua kikimuhusisha zaidi aliyekua mwenyekiti wa CHADEMA mashariki na wakili mbobezi, Mh. Mabere Marando. Haya yote yalitokana na yali aliyodai kuwa kuchafuliwa kisiasa na TISS pamoja na serikali ya CCM chini ya Mwalim. Hata hivyo, Marando amewahi kujitoteza hadharani na kupinga uvumi huu, japo naye alikiri kuwa umemtesa na kumuathiri kwa miongo kadhaa ikiwemo kukosa baadhi ya nyadhifa kutokana na uvumi huu. Kufatilia interview hiyo unaweza gusa hapa.
IMG_20240430_173648.jpg

Je ilikuaje? Kukamatwa kwa washukiwa wa jaribio la mapinduzi tarehe 6 Januari 1983, kulikuwa na matukio ya kutisha na ya kusikitisha. Washukiwa walipanga kukutana katika nyumba ya Kinondoni na kisha kuendelea hadi nyumba ya masaki kwaajili ya maelekezo ya mwisho. Siku hii baada ya TISS na askari polisi kufika katika nyumba ya Kinondoni walimkuta Tamimu pekeyake na baada ya Tamimu kujua hilo, aliruka ukuta wa nyumba hiyo na kurukia katika gari la mizigo kwa nia ya kutoroka.

According to Hans Poppe, anasema yeye alipokaribia nyumba ya Kinondoni, alimwona Tamim akikimbizwa na watu watatu. Muda mfupi baadaye, alisikia milio ya risasi na Tamim akaanguka kutoka kwenye gari la kubebea mizigo alilokuwa amerukia katika jaribio lake la kutoroka. Hans Poppe alifuatilia kwa karibu kuona kilichotokea baadaye wakati mwili wa Tamim ulipopelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti. Hata hivyo, japo Poppe anatajwa kama moja ya mashuhuda wa tukio hili, mpka unafariki dunia hakuwai kumtaja Marando wala mtu yeyote kama muhusika wa kifo cha Tamimu.

Alipomwona mhudumu wa chumba cha maiti akichukua mwili, Poppe alimpa pesa na kuomba kuona mwili huo. Mhudumu alimwambia jambo lililomtisha sana; alisema kwamba watu hao (TISS) walichukua karatasi kutoka mfukoni mwa Tamim iliyokuwa na orodha ya majina pamoja na vyeo vya kijeshi.

Poppe alirudi haraka kwenye nyumba hiyo huko Kinondoni, na kwa masikitiko makubwa alikuta imezingirwa na polisi waliovaa sare na wale wa kiraia. Pia, alikuta baadhi ya wenzake wamekamatwa na baadhi walikuwa wakizunguka uzio wa nyumba hiyo (Mind you, nyumba hii ndo ilikua sehemu ya kukutania kabla ya kwenda masaki kwaajilk ya maelekezo ya mwisho, hivyo wengi walikamatiwa hapa).

Alienda na kuwajulisha kilichotokea. Ilikuwa saa mbili usiku na hakukuwa na chochote cha kufanya ili kuokoa hali hiyo. Kwa wakati huo, kila mtu alikuwa anajitafutia njia ya kujinusuru, kwani mambo yalikuwa yameharibika kabisa! Wengine waliamua kukimbilia Kenya ambako walipewa hifadhi. Hans Poppe, ambaye alikuwa ameoa na alikuwa na binti wa mwaka mmoja, aliamua kubaki na kukabiliana na hali iliyokuwa inaendelea.

Hata hivyo, Hans Poppe alikamatwa usiku huo huo. Na katika mazungumzo yake na The Citizen, Poppe alisema yafuatayo.​
"Nilikamatwa saa tisa usiku na kupelekwa kituo cha polisi cha kati ambapo nilimkuta kaka yangu Harry ambaye alikuwa kapteni na rubani. Kwa kuwa jeshini tunaitana kwa majina ya ukoo, tulikuwa wawili wenye jina hilo. Kaka yangu alikamatwa kwanza kwa sababu alikuwa akiishi katika kambi ya anga. Hawakujua nilipoishi hadi walipomuuliza kaka yangu. Asubuhi iliyofuata nyumba yangu ilipekuliwa nikiwepo lakini hakuna kitu cha maana kilichopatikana. Tulikwenda ofisini kwangu tena hakuna kilichopatikana."
Katika jilida jilo la The Citizen, Hans Poppe anasimulia kwamba hakuteswa kimwili ingawa kulikuwa na vitisho vingi vya kufanya kutisha na kuumiza familia yake.​
"Haturuhusiwi kutembelewa hadi uvumi ulipoanza kusambaa kwamba baadhi yetu tulikuwa tumekufa. Ili kuthibitisha kwamba tulikuwa hai, waliruhusu ndugu zetu kututembelea na kutuletea chakula." - Alisema Hans Poppe.
Unaweza kusoma jalida hilo,hapa
Gwaride la utambuzi lilifanyika na wiki tatu baada ya kukamatwa kwao walishitakiwa rasmi. Jumla ya watu ishirini na tatu (23) walishitakiwa awali kama tulivyokwisha ona awali na wanajeshi wote walipelekwa Ukonga wakati raia walipelekwa Keko.

Wale waliofikishwa mahakamani pamoja na Zacharia Hans Poppe, walijumuisha Luteni Kanali Martin Ngalomba, Kapteni Suleiman Metusela, Luteni Kanali Martin Peter Msami, Luteni, Meja Reverian Bubelwa, Kapteni Vitalis Gabriel Mapunda na Kapteni Dietrich Oswald Mbogoro. Wengine walikuwa Kapteni Rodric Roshan Roberts, Kapteni Abdul Feshi Mketto, Kapteni Harry Hans Poppe, Kapteni Manyama Athumani Kazukamwe, Luteni Badru Rwechungura Kajaja, Luteni Pascal Christian Chaika na Luteni John Alphonce Chitungui. Pia kwenye orodha hiyo walikuwepo Luteni Mark Augustine Mkude, Luteni John Simon Mbelwa Mzimba, Luteni Gervas B. Rweyongeza, Luteni Othar Thomas Haule, Luteni Nimrod Theophil Faraji na Luteni Michael Mwigulu.

Baada ya watu hao kukamatwa walipelekwa mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kaajili ya Committal proceeding. Mahakamani, ilidaiwa kwamba Hans Pope na mwenzake walipanga njama za kumuua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania. Walishutumiwa kwa kupanga njama za kuipindua serikali kati ya Juni 1982 na Januari 1983. Kesi hiyo, ambayo ilikuwa kesi ya pili ya uhaini katika historia ya Tanzania Bara baada ya nyingine katika miaka ya 1970 (hapa namaanisha kesi rasmi zilizofikishwa mahakamani, achana na yale mapinduzi ya 1964),

Hata hivyo, kesi hiyo, ambayo awali iliwahusisha watu 23, ilisimama Ijumaa, Juni 17, 1983, siku chache baada ya mshtakiwa wa kwanza, Pius Mutakubwa Lugangira maarufu kama Father Tom na mshtakiwa wa pili, Hatty McGhee au Hatibu Gandhi, kutoroka wakiwa rumande katika gereza la keko Dar Es Salaam.

Baada ya mwaka mmoja (1984), Kenya na Tanzania zilibadilishana wahalifu ambapo, Hatibu Gadhi na wengine wachache waliotoroka wakati wa kukamatwa kwa mara ya kwanza walirudishwa kwa njia ya kurejeshwa wakati Tanzania ilimrudisha Hezekia Rabata Ochuka aliyekuwa anaongoza mapinduzi Kenya dhidi ya President Daniel Moi mwaka 1982.​
images (60).jpeg


Kesi ya kena Hans Poppe ilipelekwa mahakam kuu kutoka katika mahaka ya kisutu siku ya Jumatatu mnamo Septemba 17, 1984 safari hii ikiwa na watuhumiwa 14 pekee. Baada ya kusikilizwa kwa miezi saba katika mahakama kuu, watuhumiwa watano wali​
achiwa huru, watuhumiwa hao walikuwa L

uteni Mark Augustine Mkude, Luteni Gervas Rweyongeza, Luteni Paschal Chaika


na

Luteni Nimrod Theophil Faraji.Hata hivyo, Washitakiwa wote walikua wakijitetea kwa utetezi kwamba kesi hii ni ya kubuni, iliyotengenezwa kwa pamoja na polisi na Idara ya Usalama wa Taifa ya Serikali ili kuficha kifo cha Mohamed Tamimu. Ijumaa, Desemba 27, 1985, Jaji Mkuu Nassor Mzavas, aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, aliamua kwamba kulikuwa na njama za kuipindua serikali, kama ilivyodaiwa na upande wa mashtaka. Jaji Mzavas aliwahukumu watuhumiwa 9 waliobaki (kama nilivyokwisha wataja vizuri katika sehemu zilizopita) kifungo cha maisha gerezani.

Baada ya hukumu hiyo ya Jaji Mzavas, washtakiwa wote 9 waliokutwa na hatia kama tulivyokwisha kuona, wakiongozwa na Hatibu Gadhi hawakuridhika na kifungo hiko hali iliyopelekea kukata rufaa katika mahakama ya rufani. Rufaa hiyo ilisikilizwa na majaji watatu wakiongozwa na aliyekuwa Jaji mkuu kwa kipindi hiko (Nyalali).
IMG_20240430_194902.jpg


Lakini pia, hata baada ya rufani hiyo kusikilizwa. Mwaka 1986 mahakama ya rufani ilitoa maamuzi yake na kena Hans Poppe waligonga mwamba kwa kushindwa rufaha hiyo. Hii iliwafanya kena Hans Poppe kutumikia kifungo chao cha maisha jela. Hata hivyo, baada ya miaka 10 ya hukumu kupita wakiwa gerezani, mnamo mwaka 1995 katika kipindi cha lala salama cha aliyekuwa Raisi wa awamu ya pili wa Tanzania, mzee wetu hayati Mwinyi ama mzee wa ruksa kama wengi tulivyozoea kumuita. Aliwaachia wahukumiwa wote 9 wa kesi hii ya uhaini na kuwafanya wawe huru kwa msamaha wa Raisi, that's why tukaendelea kumuona mzee wetu Hans Poppe uraiani.
images (67).jpeg


Nadhani hapa tutakua tumejibu maswali yote tuliyoanza nayo kwanzia sehemu ya kwanza ya mkasa huu mpaka hii ya mwisho, swali pekee ambalo limekua gumu kujibika ni lililopo katika title; Ni nani aliyemuua Tamimu?🤔. Swali hili labda niliache kwenu wadau kwa ambae analifahamu vizuri zaidi atusaidie, na vipi maelezo ya Marando alipojitokeza hadharani kuongea na waandishi wa habari miaka 10 iliyopita, yanatija kujinasua katika uvumi huu🤔?. Unaweza tazama interview hiyo hapa 👇

View: https://youtu.be/6MuEqbRje_g?si=_W0Q17fwvnl5OIiS
 

Attachments

  • images (68).jpeg
    images (68).jpeg
    16.6 KB · Views: 4
Back
Top Bottom