Father of All
JF-Expert Member
- May 30, 2026
- 360
- 624
Kihisitoria, Makamu wa rais wa kwanza kujiuzulu nchini alikuwa Aboud Jumbe.
Alirubuniwa na wachoyo na walafi wa madaraka hasa vijana wakiongozwa na marehemu Seif Shariff Hamad ili wamuondoe wachukue ukanda wakaisha kuishi na kufa kwa upanga kama walivyoishi kwao. Nchimbi kaondolewa. Tunajua ni nani wako nyuma ya umbea kwa mama kama vile Bashite na Madelu wasijue nao waweza kuishia kama Maalim Seif.
Je, kwanini Nchimbi hakukabidhi ofisi kwa Ndejembi?
Jumbe aliitwa Dodoma na kufukuzwa.
Kwanini Nchimbi amefukuzwa in absentia?
Yuko wapi?
Kwanini amekuwa kimya hivyo?
Yu hai au marehemu?
Yuko huru au korokoroni?
Yuko nchini au ughaibuni na ni wapi nchini au nchi gani ughaibuni?
Je makosa yake ni yapi na adhabu zake ni zipi kikatia?
Je, barua ya kujiuzulu aliandika au aliandikiwa na kwanini?
Kunani kinafichwa kama hakuna namna na mizengwe na usanii?
Nani anamdganya nani na ili iweje kati ya watawala, watawaliwa, hata Nchimbi mwenyewe?
Je, Nchimbi angependa ajitokeze ila amezuiliwa au amejiuzuia?
Je, kuna machezo tumechezewa ili akiibuka aonewe huruma na awe rais ajaye?
Jumbe alifukuzwa kwa sababu ya kutaka mabadiliko ya muundo wa muungaono sawa na Nchimbi kuunga mkono madai ya katiba mpya inayotaka kuwepo muundo mpya wa muunagnao.
Tusaidiane kujua kinachoendelea.