Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Mwenzangu mwenzio nasherekea kwa kula majani kama Pesambili alivyotutaka kipindi kile kwamba tupende tusipende ikiwezekana hata majani tutakula mradi ndege ya Rais inunuliwe. Leo sili.

Nimefika hapa Subway lakini sikio langu liko Kisutu na baada ya kusikia kuwa hawa mafisadi wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana wanatayarishwa kwenda, nikajisikia nimeshiba ghafla. Najisikia kwenda cheza mdundiko pale mahakamani wakati wakienda Keko/Segerea ila taratibu haziniruhusu!!!! Basi sikio langu laendelea kubaki huko Kisutu nitawapa habari zaidi!!
 
2940d1227607835-yona-na-mramba-kufikishwa-mahakamani-mramba-na-yona.jpg






Picha inatoa habari kwa umakini zaidi. Hebu oneni wenyewe wanavyopendeza...!!!
 
Ninavyojua mimi dhamana sio lazima iwe Cash, hata mali isiyohamishika yenye dhamani hiyo. Sasa kama Hakimu kasisitiza ni dhamana ni Cash then hapo kazi itakuwa nzito kwa wao kutoka leo...kwa sababu hata kama hizo hela wanazo sidhani kama watakuwa tayari kujionyesha kuwa wanazo.

Hakimu amesisitiza cash.... Na huo ndio mtego
 
Nimefika hapa Subway lakini sikio langu liko Kisutu na baada ya kusikia kuwa hawa mafisadi wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana wanatayarishwa kwenda, nikajisikia nimeshiba ghafla. Najisikia kwenda cheza mdundiko pale mahakamani wakati wakienda Keko/Segerea ila taratibu haziniruhusu!!!! Basi sikio langu laendelea kubaki huko Kisutu nitawapa habari zaidi!!

Kula japo kidogo, unaweza ukasikia tamko lingine wakati wowote kuanzia sasa na njaa ikakubana ghafla! Itabidi ule chakula cha baridi ama makombo. Utawaweza hawa ma-actors wa TZ? Bado wako juu ya sheria! Kula Mama Mdogo! shauri yako!
 
nimesikia eti wamepigwa na Uhujumu Uchumi.....kuna kampuni ya Yona alianzisha ya madini nayo imehusishwa
 
mawaziri wa zamani mh. daniel yonah (shoto) na mh. basil pesambili mramba wakiwa katika mahakama ya hakimu mkazi ya kisutu jijini dar baada ya kusomewa mashtaka yao muda mfupi uliopita.
wote wamewekewa masharti ya dhamana kwamba kila mmoja atoe bilioni 3.9 keshi, wasalimishe hati za kusafiria, wasitoke nje ya dar na kila mmoja awe na wadhamini wawili ambao mahakama inabidi iridhike kuwa ni wa kuaminika.
hadi globu hii ya jamii inaingia mitamboni juhudi za kupata dhamana zilikuwa zinaendelea.
stori kamili inaandaliwa.
stay tuned

Source: MICHUZI BLOG.
 
Kuna mawili hapa Watanzania wenzangu; tuahirishe angalau kwa muda tofauti zetu na JK ili tumuunge mkono kwenye juhudi zake hizi mpya au tuwe upande wa hawa WAHUJUMU wa UCHUMI wa NCHI yetu.
 
Hapa nilipo ni Alfajiri lakini naifuatilia kesi hii kwa karibu kabisa. Inavyo onekana ni kwamba dhamana yao ni 3.9 Billion Cash MONEY, lazima waache mikoba yao kwa pillato na lazima kuwa na two citizen walio jitolea kuwasimamia.

Kama ingekuwa Football ningesema JK hit a first down, BUT I NEED TOUCHDOWN. Sababu first down doesn't count. I know watu mtasema kwamba we demand a lot. I think all this SUCKERS need to stand infront of pilato na kujibu mashitaka. Kisha wahukumiwe miaka na miaka kwenye jella za huko makutupolla shinyanga.

Nadhani kama muendesha mashtaka ana roho mbaya basi muda kama huu ni kufile kama between 5 and 10 counts kwa kila mmoja. Includes kuhujumu uchumi, wizi wa mali ya umma, kuchangia kuongezeka kwa umaskini. Just throw everythinhg and see what will stick.

I am smile, but i need more baby. I wanna Mkapa to be infront of Judge, I wanna Rostam, Lowassa. JK make me proud of you once again since nilipokupigia kampeni 2005.
 
Bubu Msemaovyo, hiyo presha anayokupa Mama Mdogo ni kuhusu hao vigogo au kitu kingine??!!??? Nimeingia wasiwasi.

Nilimwambia ananitia presha kwa sababu ilionekana kama hakuna kesi kama hiyo. Hakika ninapenda sana hawa jamaa wapate haki yao maana walipokuwa madarakani walijifanya miungu watu wakataka kutulazimisha tule majani.
 
Nasikia wao walikuwa wanachukua 1% kwenye dili ya Alec Stewart,wakati serikali nzima ilikuwa inapata 3%
 
Kuna mawili hapa Watanzania wenzangu; tuahirishe angalau kwa muda tofauti zetu na JK ili tumuunge mkono kwenye juhudi zake hizi mpya au tuwe upande wa hawa WAHUJUMU wa UCHUMI wa NCHI yetu.


Utakuwa mwendawazimu kufikiria namna hii at this stage!!!!!!!
 
Hivi ni kweli au mmewafananisha?Kwasababu kama ni kweli ina maana kwamba Benjamin W.Mkapa lazima ashitakiwa pia;tofauti na hivyo ni kuwaonea hao walioshitakiwa,ukizingatia yeye(Mkapa) ndiye aliyechangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa vimeo katika nchi hii mojawapo ya kimeo hicho ni EPA.
As general rule,nafikiri Mkapa katiba ya nchi inamlinda asishitakiwe!Lakini kisheria wherever there is a general rule there must be an exceptions.Hivyo basi,kwa kanuni hii ya kisheria binafsi kwa maslahi ya Taifa hili maskini la Tanzania ni naamuru B.W.Mkapa ashitakiwe haraka iwezekanavyo.
Tuombe uhai tu na tutaona ni nini kinaendelea kwa maslahi ya umma au ya wachache katika nchi hii yenye uongozi corrupt ili hali watu wake wengine ni maskini na Taifa pia eeeehhhh eebwanaeeeehhh duuuuhhh!!!
 
Acheni kufurahia maigizo yaliyoandaliwa kwa makini. Watafunguliwa mashitaka, mahakimu na majaji wa kuzisimamia walishaandaliwa na hukumu zinajulikana, kesi zitaendelea wao wakiwa nje kwa dhamana mpaka baada ya ucgaguzi 2010, hii ni pamoja na wale wa EPA nk, wait and see!
 
Nasikia wao walikuwa wanachukua 1% kwenye dili ya Alec Stewart,wakati serikali nzima ilikuwa inapata 3%

Kwenye 3% iliyotakiwa iingie serikalini wao (alex stewart) walikuwa wanalamba 1.9% na serikali kubaki na 1.1% tu
 
Back
Top Bottom