Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

Naona wageni wamesikia harufu ya Pilau na Pengine waheshimiwa ambao majina yao bado hayajatajwa wapo wanakula chabo kuona kama wamewekwa hewani. I love JF

"Currently Active Users Viewing This Thread: 181 (48 members and 133 guests)"
 
WanaJF,

Msishangilie kwa chochote, Mramba na Yona wamefunguliwa mashtaka ya Abuse of Power katika sakala ya Alex Stewart. Muda wowote kwanzia sasa wanaachiwa.

Not that easy... masharti waliyowekewa ni pamoja na kudeposit 3.5/- bilion in cash. Can they raise such amount?
 
Ni kweli, wameshafikishwa mahakamani na wanasheria wao wanahangaikia dhamana. wamekutwa na makosa zaidi ya 10.
 
Ni kweli, wameshafikishwa mahakamani na wanasheria wao wanahangaikia dhamana. wamekutwa na makosa zaidi ya 10.

Mh Rekebisha Mkuu...wametuhumiwa na makosa zaidi ya 10..sio "kukutwa" ni mapema mno.
 
Ni kweli, wameshafikishwa mahakamani na wanasheria wao wanahangaikia dhamana. wamekutwa na makosa zaidi ya 10.

Sahihisho! Wamesomewa mashtaka 10 na siyo wamekutwa maana bado hawajatiwa hatiani bado!
 
Not that easy... masharti waliyowekewa ni pamoja na kudeposit 3.5/- bilion in cash. Can they raise such amount?

Ninavyojua mimi dhamana sio lazima iwe Cash, hata mali isiyohamishika yenye dhamani hiyo. Sasa kama Hakimu kasisitiza ni dhamana ni Cash then hapo kazi itakuwa nzito kwa wao kutoka leo...kwa sababu hata kama hizo hela wanazo sidhani kama watakuwa tayari kujionyesha kuwa wanazo.
 
WanaJF,

Msishangilie kwa chochote, Mramba na Yona wamefunguliwa mashtaka ya Abuse of Power katika sakala ya Alex Stewart. Muda wowote kwanzia sasa wanaachiwa.

Wangefunguliwa Kesi ya Kuhujumu Uchumi, Ningefurahi zaidi.
 
Bubu Msemaovyo, hiyo presha anayokupa Mama Mdogo ni kuhusu hao vigogo au kitu kingine??!!??? Nimeingia wasiwasi.
 
Huyu Mramba na Yona wameifisadi nchi yetu kwa kiwango cha kutisha,nategemea mashitaka yao nayo pia yatakuwa ya kutisha. Abuse of Power isiishie Alex Stewart bali iende zaidi ya hapo,kuna hili suala Yona na yule mzee wa ukweli na uwazi kujiuzia mgodi wa Kiwira kwa bei ya kutupwa nategemea litawekwa kwenye mashtaka.
 
Wangefunguliwa Kesi ya Kuhujumu Uchumi, Ningefurahi zaidi.

Kesi ya "Kuhujumu Uchumi" inaweza pia kuzaliwa na hii kesi ya Msingi "Abuse of Power" ni kipimo kizuri kujua iwapo DPP ana nia ya kweli ya kufuata mkondo wa sheria kwa makosa yaliyotendeka au ni "Funika Kombe MWanaharamu Apite".

So far so good...at least something is happening..!!
 
Kuna habari kwamba wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana...
 
Mahakama zetu kama kweli ziko huru na mahakimu waliobobea kwenye fani yao hawawezi kuthubutu kutomwona Mkapa ndani ya sakata hili angalau aitwe kama shahidi!
Siwaingilii kwenye kazi yao hii lakini ni vigumu mno kutenganisha MAAMUZI ya MAWAZIRI na aliyewateua hasa kesi inapokuwa mahakamani na sio BUNGENI kama tulivyozugwa kwenye Richmond.
 
Ninavyojua mimi dhamana sio lazima iwe Cash sasa kama Hakina kasisitiza ni Cash then hapo kazi itakuwa nzito kwa wao kutoka leo...kwa sababu hata kama hizo hela wanazo sidhani kama watakuwa tayari kujionyesha kuwa wanazo.

Picha hii itakuwa kali! Ila nahofia mwisho wake maana haitatoa maana. JK angecheza kama Amitabachan tungekuwa na kaimani kidogo.

Wanaenda na luxury bus keko wanarudi benz usiku. Nyie mnatakaje, huyu mangi aende lupango amekosa fedha ya dhamana! Imposible, not Mramba! Kuna dream team nyuma yake wewe!
Tuache maskhara, hawawezi kumpeleka huyu lupango. kama aliachwa ili ahudhurie sendoff ya mwanae ni kuahiriswa kupelekwa keko? na yetu macho kodooooooooooooo!
 
Naambiwa JK amelazimika kwenda route hii maana kutofanya hivyo, serikali ijayo ingemsweka ndani yeye.

Japo hii yaweza kuwa sanaa, ni jambo jema sana kwamba wananchi sasa hawatayumba kuamini kwamba kuna watu wako juu ya sheria.

Tunachohitaji sasa ni Hakimu "mwenye kichaa" na ujasiri atakayebadili kesi kuwa ni ya kuhujumu Uchumi.

.
 
Serikali inaonekana kuwa serious.Watuhumiwa wa EPA awali nilikuwa nikidhani hawaguswi na sasa haooo....leo hii nasikia tena kina Mramba na yona wamefikishwa mahakamani ! I love this!
Yeah unajua kuna watu hujifanya wanapenda demokrasi lakini mentaly ni ma dikteta.watu walitaka ili mradi mtu kathumiwa akamtwe .lakini JK sio dikteta hupenda sheria ichukue mkondo wake na huwezi kumburuta mtu mahakamani bila kufanya uchunguzi wa kutosha vinginevyo iatakuwa suala la kuadhiriana tuu.
 
Mwenzangu mwenzio nasherekea kwa kula majani kama Pesambili alivyotutaka kipindi kile kwamba tupende tusipende ikiwezekana hata majani tutakula mradi ndege ya Rais inunuliwe. Leo sili.

Nimefika hapa Subway lakini sikio langu liko Kisutu na baada ya kusikia kuwa hawa mafisadi wameshindwa kutimiza masharti ya dhamana wanatayarishwa kwenda, nikajisikia nimeshiba ghafla. Najisikia kwenda cheza mdundiko pale mahakamani wakati wakienda Keko/Segerea ila taratibu haziniruhusu!!!! Basi sikio langu laendelea kubaki huko Kisutu nitawahabaribisha!!
 
Back
Top Bottom