Watumishi 11 wa Manispaa ya Kigoma akiwemo Mkurugenzi wa Igunga wapandishwa kizimbani na kusomewa Mashtaka 11

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Jumla ya watu 11 wakiwemo watumishi saba wa manispaa ya Kigoma Ujiji na maafisa wawili wa Wizara ya Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) wamefikishwa mahakamani katika mahakama ya hakimu mkazi Kigoma na kusomewa mashitaka 11 ikiwemo shitaka la uhujumu uchumi na utakatishaji fedha kiasi cha shilingi milioni 463.5.

Waliopandishwa kizimbani na kusomewama mashitaka ambao walikuwepo mahakamani hapo ni Pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Athumani Msabila ambaye amehamishiwa halmashauri ya wilaya Igunga akiwa mshitakiwa wa kwanza

Mashtaka hayo yamesomwa mbele ya hakimu Mkazi Kigoma, Hassan Momba ambapo mwendesha mashtaka Wakili, Anonisye Erasto aliieleza mahakama hiyo kwamba washitakiwa hao walitenda makosa hayo kwa kati ya Juni 1 2022 hadi Juni 5 2023.

Pamoja na hayo washitakiwa hao ambao hawakutakiwa kujibu chochote pia walisomewa mashtaka ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kugushi nyaraka, kutakatisha fedha, kuisababishia Serikali hasara ya shilingi milioni 463.5 na matumizi mabaya ya madaraka.

Wengine ni washitakiwa saba watumishi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji ambao ni Pamoja na Afisa mipango wa halmashauri hiyo,Ferdinand Filimbi, Mweka Hazina wa manispaa hiyo, Salum Saidi, Kombe Salum Kabichi , Frank Nguvumali, Jema Mbilinyi, Moses Zahuye, Joel shirima na mtumishi kutoka ofisi ya Mkuu wa mkoa Kigoma, Bayaga Ntamasambilo.

Aidha washitakiwa wawili watumishi wa Wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa waliofikishwa mahakamani hapo ni pamoja na Aidan Mponzi na Tumsifu ambao walisafirishwa kutoka Dodoma kuletwa Kigoma kwa ajili ya kusomewa mashitaka yao wakielezwa ndiyo waliohusika kupelekwa kwa fedha hizo Kigoma Ujiji kuwa ni Aidan Zabron na Tumsifu Kachira.

Kesi hiyo namba 3 ya mwaka 2023 imeahirishwa mpaka Novemba 20, 2023 kwa ajili ya kutajwa sambamba na kutoa uamuzi mdogo kwa washitakiwa watano kama wanaweza kupata dhamana ambapo washitakiwa wote walirudishwa rumande.
 
Kaka ni kamba tu hata kama ndefu au nyembamba ni kamba yako
 
Kwanza hiyo pesa wairudishe kisha mambo mengine yaendelee,WARUDISHE HIYO PESA NA WAPIGWE MVUA TUH SHENZ HAO
 
Exactly mkuu sijui tuna laana gani?!

Hakuna sehemu yoyote serikalini ambako hakuna upigaji. Ni utamaduni kabisa wa watanzania.
Siyo utamaduni ni uroho wa ubinafsi wa viongozi, kiongozi mkuu kama haibi wewe utaweza kuiba? madokezo yanapitishwa na wateule wa Rais yote(Accounting Officers)
 
Nikia galia tuu hayo maelezo naona watuhumiwa wakishinda hasa hao watamisemi
 
Back
Top Bottom