Yona na Mramba: Mashtaka na yatokanayo

....well, this is at least a step ah........ wacha wapate kukalia viti vya kisutu na kuonja mshangao wa binadamu wema kwa watuhumiwa.

natumai itakuwa na impact fulani katika vichwa vyao na jamaa wanaowazunguka, hasa waroho wenzao wa mali za umma.
 
Acheni kufurahia maigizo yaliyoandaliwa kwa makini. Watafunguliwa mashitaka, mahakimu na majaji wa kuzisimamia walishaandaliwa na hukumu zinajulikana, kesi zitaendelea wao wakiwa nje kwa dhamana mpaka baada ya ucgaguzi 2010, hii ni pamoja na wale wa EPA nk, wait and see!

You need the holy spirit
 
Kuwafikisha watu wa "hadhi" hii katika jamii yetu mahakamani wakakalia dawati kavu kama hilo huku wakilindwa na askari hivyo inavyoonekana, ni hatua moja mbele kwenye mapambano haya ambayo yalionekana kutushinda tangu enzi ya Mzee Mwinyi.
 
2940d1227607835-yona-na-mramba-kufikishwa-mahakamani-mramba-na-yona.jpg






Picha inatoa habari kwa umakini zaidi. Hebu oneni wenyewe wanavyopendeza...!!!

Jamaa wanaonekana hawakutegemea,lakini ni mapema mno kushangilia isijeikawa ni aina nyingine ya ufisadi tunafanyiwa wadanganyika.
 
Na inahitajika akili ya "kiuendawazimu" hivi kuziona juhudi anazofanya RAIS wetu.

Ni raisi wako huyo huyo alimteua Mramba kuwa waziri wa miundo mbinu pamoja na manung'uniko mengi kutoka ndani ya serikali na kwa wananchi ile reshuffle ya kwanza alimwacha akipeta. Wewe kama ni mpiga debe wake kumbuka watanzania si mabwege hizo unazoziita juhudi ni kazi ya serikali kusimamia maadili na kuwashtaki wote wanaoenda kinyume na sheria.

Just another note for u, katikla utendaji wowote ule:

100% < = underperforming

100% = compliance

greater than 100% = Performing
 
Hawa jamaa ni kweli wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka yanayohusiana na masuala ya madini. Kwa mujibu wa MICHUZI picha yao wakiwa kizimbani na polisi karibu yao inathibitisha ukweli wa habari hii.
The net is closing down to BWM - Hana kinga kwa wizi alioufanya kama BMW. Kinga ni kwa masuala aliyofanya in his capacity as president Mfano akiamuru mtu aliyehukumiwa kunyongwa anyongwe na baada ya hapo ikadhibitika kuwa mtu huyo hakluwa ametenda kosa; au predident akiamuru mali za mtu zitaifishwe kwa manufaa ya umma na baadae ikaonekana ilikuwa ni makosa kufanya hivyo.
 
Nasikia wao walikuwa wanachukua 1% kwenye dili ya Alec Stewart,wakati serikali nzima ilikuwa inapata 3%

Hapana, walikuwa wanachukua 1.8% ya mrahaba wote, halafu Serikali ikawa inaambulia 1.2% inayobaki. Eti hiyo 1.8% ndio "Audit Service Fees" ya ku-audit "quantities and values" za dhahabu zinazozalishwa na migodi yote kabla haijasafirishwa nje ya nchi.

Pia kampuni hiyo ya Alex Stewart, ambayo inasemekana ni ya mtoto wa Mramba, ilikuwa imesamehewa kodi karibu zote za serikali ikiwemo hata ile ya wafanyakazi wake PAy As You Earn (PAYE). Barua ya kusamehe kodi hizo ilitolewa na kusainiwa na Mramba mwenyewe akiwa Waziri wa Fedha. Iliwahi kuchapishwa kwenye magazeti ya This Day au The Citizen kama sikosei.

Pia Mramba huyu huyu aliwahi kusema kwamba ndege ya Rais lazima itanunuliwa hata kama ikibidi Watanzania kula nyasi........!!! Malipo ni hapa hapa duniani!
 
Nimetokea Mahakama ya kisutu na taarifa ni kuwa wanatakiwa kuwa na wadhamini wawili na wote kwa pamoja wanatakiwa kuweka bondi ya Tshs. 4 bn.......So mpaka now jamaa wamekosa hiyo pesa na wamepelekwa rumande kama kawa....
Kosa lao ni ABUSE OF OFFICE
 
Ni raisi wako huyo huyo alimteua Mramba kuwa waziri wa miundo mbinu pamoja na manung'uniko mengi kutoka ndani ya serikali na kwa wananchi ile reshuffle ya kwanza alimwacha akipeta. Wewe kama ni mpiga debe wake kumbuka watanzania si mabwege hizo unazoziita juhudi ni kazi ya serikali kusimamia maadili na kuwashtaki wote wanaoenda kinyume na sheria.

Just another note for u, katikla utendaji wowote ule:

100% = underperforming

100% = compliance

greater than 100% = Performing

Nakubaliana na wewe. Lakini ni RAIS huyuhuyu ambaye sasa ameruhusu wakalie dawati lile leo. Mramba na Yona hawatarudi kwenye hadhi na heshima waliokuwa nayo hadi jana hata kama watashinda kesi hii.
 
Raia Mwema - Mawaziri kushitakiwa kwa tuhuma za ufisadi

SERIKALI inakamilisha taratibu za kuwashitaki mawaziri wa zamani wawili wanaotuhumiwa kwa ufisadi, Raia Mwema imefahamishwa.
Habari za uhakika zilizopatikana na kuthibitishwa na maofisa waandamizi wa Serikali zinaeleza kwamba mawaziri hao (majina tunayo) walihojiwa na vyombo vya dola kwa mara kadhaa na sasa mchakato wa kuwashitaki uko katika hatua za mwisho.
Wote wawili walipata kuongoza Wizara ya Fedha, chini ya utawala wa Rais Benjamin Mkapa na mmoja aliteuliwa katika serikali mpya ya Rais Jakaya Kikwete kabla ya kuachwa katika mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni.


Mhe. Pesambili Mramba
Kwa mujibu wa habari hizo, mmoja amekuwa akichunguzwa kufanya maamuzi kadhaa yenye utata, ikiwamo kutoa misamaha ya kodi ambayo kisheria hakuwa na mamlaka nayo akiwa anatuhumiwa kuvuka mipaka ya mamlaka yake katika kutoa misamaha.
Mwingine anaelezwa kuchunguzwa kuhusika na maamuzi kadhaa akiwa Waziri katika Wizara ya Fedha na Wizara ya Nishati na Madini, lakini haikuweza kufahamika mara moja ni eneo gani hasa ambalo mwanasiasa huyo mstaafu amechunguzwa.
Mawaziri wote wawili wanatajwa sana kuwa karibu na Mkapa katika masuala kadhaa ya kiutendaji na hata katika masuala kadhaa binafsi na inaelezwa kwamba baadhi ya mambo yaliyochunguzwa yanaweza kumgusa moja kwa moja Rais huyo mstaafu.
Mkapa anatajwa kuhusika moja kwa moja na mradi mkubwa wa mkaa wa mawe wa Kiwira, akiwa na maslahi binafsi katika kampuni ya Tanpower Resources, ambayo iliuziwa hisa za kampuni ya Kiwira Coal Mines Limited iliyokuwa ikimilikiwa na serikali kabla ya ubinafsishaji.


Mhe. Daniel Yona
Pamoja na Mkapa kutajwa katika maeneo mengi, bado kumekuwa na maelezo ya kutaka “aachwe apumzike”, huku baadhi wakitumia kinga ya kikatiba ambayo rais mstaafu anakuwa nayo pamoja na kupingwa na baadhi ya wanasheria.
Haikuweza kufahamika mara moja mawaziri hao walichunguzwa katika maeneo gani mengine zaidi lakini kuna uhakika kwamba uchunguzi huo uligusa pia misamaha ya kodi iliyofanywa katika kipindi mawaziri hao wakiwa madarakani.
Miongoni mwa mambo ambayo yaliguswa ni mkataba kati ya Serikali na wakaguzi wa Alex Stewarts waliokuwa wakifanya ukaguzi wa mapato katika sekta ya madini.
Eneo jingine tata ambalo linatajwa kuguswa ni mkataba wa Serikali na kampuni ya Tanzania International ContainerTerminal (TICTS) wa kukodisha eneo la bandari ya Dar es Salaam, mkataba ambao hadi sasa umekuwa ukipigiwa kelele na wadau mbalimbali wa sekta ya bandari.


RAIS Mstaafu Mkapa
Hata hivyo, mawaziri wote wawili walikuwa ama na mahusiano ya karibu na Mkapa kikazi na hata kibinafsi mambo ambayo yanazidi kuonyesha ni jinsi gani Serikali italazimika kumtaja ama kumgusa rais huyo mstaafu katika uchunguzi na hatimaye mashitaka.
Ikiwa wanasiasa hao watafikishwa mahakamani, itakuwa ni mara ya pili kwa Serikali ya Kikwete kuwashitaki watendaji wake wa zamani ikianzia na aliyekuwa Balozi wa Tanzania Italia, Profesa Costa Mahalu, anayeendelea kujitetea katika mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, akituhumiwa kuiibia Serikali Sh bilioni 2 kutokana na ununuzi wa jengo la ubalozi, Rome.
Hata hivyo, kiu kubwa ya Watanzania kwa sasa iko kwa watu wanaotajwa kuhusika katika upotevu wa mabilioni ya fedha za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na wale waliohusika na mradi tata wa umeme wa dharura wa Richmond Development LLC.
Pamoja na Rais Kikwete kuagiza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuongoza timu ya wataalamu akisaidiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa (Takukuru), Edward Hosea, kulikuwa na kazi iliyokwisha kuanza kufanywa na vyombo hivyo ndani ya BoT na maeneo mengine nyeti kiuchumi.
 
Power to the People. JF Idumu.


Currently Active Users Viewing This Thread: 332 (118 members and 214 guests)


Yebo Yebo, 911, Al, allse, Alnadaby, August, August_Shao, BelindaJacob, Belo, Bi Tarabushi, Bint, Bonnie1974, bulugu, Chuma, dedee, djwalwa, Domo Kaya, Edo, Fatuma, fikiri2, Franc, Gamba la Nyoka, Gashle, Gembe, Halisi, Heri, Idimi, Invincible, Iteitei Lya Kitee, Jibaba Bonge, Jmpambije, Jobjob2, kajoro, Kaka Mdogo, Kakulwa, kamakabuzi, Kandambilimbili, kapuchi, KatuleJ, KGM, Kibunango, Kichwangumu, Kijunjwe, Kilinzibar, Kinyau, Kisambayende, kiuyajibu, Koba, Komavu, Kuntakinte, Kwayu, LadyMzuri, Lione, Liz Senior, Lyampinga, macinkus, Majita, Mama Lao, Mama Mdogo, mambo, mamiso, Mbassa, MC, MegaPyne, Mfamaji, Mgoyangi, Mkora, MKUDE WA MGETA, Mkuu, Mlalahoi, Mnyonywaji, Mnyoofu, Mong'oo, Morani75, MpiganajiNambaMoja, mpingo, Mr. Zero, Mrembo, MROSSO, Mtanzania, mTz, Mukubwa, mutua12, MwakyJ, Najikopa Mwenye, nat867, Ngongo, Nono, Nyadundwe, Nyambala, Opaque, ram, Safari, SaidSabke, Sally, semjato, share, Shiduki, sir leem, Sober, Sra, sunilv00, tandala, tapeli, think BIG, TooGood, Tshala, Ushirombo, vstdar, watu, WildCard, WomenofSubstanc, ygjunior, Zion Train
 
Jamani JK ni kiboko, lile tabasamu lake lina maana nyingine kabisa, kitendo cha hawa jamaa kukalia madawati ya hapo Kisutu si kitu cha kidogo. Mramba na Yona wanakiburi cha kufa mtu tuone mwisho wake, lakini kwa hili kwa kweli JK umenikosha moyo. Nadhani Manji na Rostam wapo njiani hiwezekani Mramba na Yona watie timu hao Magabacholi wasifike Kisutu. Heko msanii wetu JK
 
Nakubaliana na wewe. Lakini ni RAIS huyuhuyu ambaye sasa ameruhusu wakalie dawati lile leo. Mramba na Yona hawatarudi kwenye hadhi na heshima waliokuwa nayo hadi jana hata kama watashinda kesi hii.

Sijakuelewa mkuu kwenye hili Lakini ni RAIS huyuhuyu ambaye sasa ameruhusu wakalie dawati lile leo

Ina maana kuna watu mpaka raisi aruhusu ndio tunawashtaki. Na nchi hiyo yenye mwenendo huo ina raisi unayetaka kutukomvisi kwamba ni mchapakazi?

Safari bado ndefu!
 
Back
Top Bottom